2018-06-15 16:02:00

Shirikisho la Walimu wa Kazi Italia ni chombo cha thamani ya kijamii


Tarehe 15 Juni 2018, baba Mtakatifu Francisko amekutana na wajumbe wa Shirikisho la Walimu wa Kazi nchini Italia na kuwakaribisha wote, waliofika wakiwa katika fursa ya Mkutano wa Kitaifa ambao unawakilisha fursa ya thamani kubwa ya kushirikisha, zaidi na kutafakari juu ya mada msingi kwa ajili ya jamii na ulimwengu mzima. Baba Mtakatifu Fracisko katika hotuba hiyo anasema, ni muhimu mchango wa Walimu wa Kazi nchini Italia, na katika kufuata nyayo wamewezesha ukuaji wa mantiki ya kijamii ya pamoja hasa zaidi katika hadhi kwa ajili ya wote. Shirikisho lao linawakilisha kwa namna ya pekee mfano wa wajibu na huduma ya pamoja. 

Tangu Historia ya Waraka wa Rerum Novarum yaani “ mambo mapya”, waraka wa kijamii uliotangazwa mnamo tarehe 15 Mei 1891 na Papa Leone XIII ikiwa ni  kwa mara ya kwanza Kanisa Katoliki lilichukua nafasi ya kwanza kujikita katika masuala ya kijamii na kuanzisha Mafundisho kijamii ya Kanisa.Ilipata kuweka na nafasi ya kazi kama kitovu cha masuala yanayo itazama jamii. Kazi kwa dhati, Baba Mtakatifu anathibitisha ipo ndani ya  moyo wa utume uliotolewa na Mungu kwa binadamu na ili kupanua matendo yake ya uumbaji na kuyatimiliza kwa njia ya uhuru wa ubunifu na shauku yake, kutawala juu ya kila kiumbe ambayo inajionesha si katika kuhudumiwa badala yake katika umoja na heshima. 

Wote tunaalikwa kutafakari uzuri wa mpango huo wa Mungu, aliutengeneza juu ya mapatano kati ya bibadamu na kila aina ya kiumbe na asili. Wakati huo huo ni kutazama hasa katika wasiwasi wa hali ya sasa ya kibinadamu na kazi ya uumbaji ambayo imegubikwa kwa kina na ishara za dhambi, ishara za uadui, ubinafsi, upofu wa fadhila binafsi. Baba Mtakatifu anauliza ni watu wangapi bado wameachwa nyuma ya maendeleo kiuchumi. Ni ndugu wangapi wanateseka kwa sababu wamekanyagwa na vurugu, vita au matatizo ya majanga ya asili. Ni watu wangapi bado  wameachwa pembezoni mwa jamii  na wanazidi kuteseka kwa ukosefu wa matarajio chanya ya wakati endelevu, kwa maana hiyo matumaini!

Anawahimiza wasidharau suala hili au kuwa tofauti na udhaifu na mateso yanayo wagusa watu wengi hivi, badala yake wote wanaweza kugeuka daima wenye uwezo wa kuwatambua katika nyuso zao na kutafuta kuwasaidia. Aidha ni vema kuendelea kutafuta daima wale ambao wanapotea, ili kuwapa matumaini wanayo hitaji kwa ajili ya kuishi; wao kwa hakika wanawakilisha kwa namna moja haki msingi ya kwanza ya kibinadamu na hasa hasa vijana! Matumaini ya wakati endelevu iliyo bora inapitia daima katika shughuli binafsi na kujikita katika kazi, haitegemei zana peke yake tu zinazo wekwa mbele.Na hakuna  usalama wa uchumi  wa uhakika, ikiwa pia na aina zozote za mageuzi ya msaada, ambao unaweza kuhakikisha ukamilifu wa maisha binafsi. Huwezi kuwa mwenye furaha bila kuwa na uwezo wa kutoa mchango, uwe mdogo au mkubwa wowote katika kujenga wema wa wengine. Kwa maana hiyo kila mtu anaweza kutoa mchango wake  ili usibaki bila kuwa na faida au kuhisi tofauti na maisha ya kijamii.

Kwa sababu hiyo jamii ambayo haina msingi wa kazi haiwezi kuhamasisha kwa dhati, na  zaidi kujihusisha hata wale waliobaguliwa pia hata kuhukumu wagonjway ina roho ya ushirikishwaji, inatafuta kuweka matunda ya nguvu ya kila mtu, rangi na rika ili apate kupumia kwa mapafu yote na kushinda vizingiti zaidi vikubwa, kadhalika na kuchota mtaji wa kibinadamu usioelezeka  kwa kumweka kila mmoja aweze kutambua hatma yake kwa mujibu wa mpango wa Mungu. Katika majadiliano ya mkutano wao,Baba Mtakatifu amewakumbusha ya kwamba, wameweza kujikita katika mahusiano ya mantiki ya kazi kwa utajiri wa urithi wa mazingira, kisanaa na utamaduni wa Italia ambao wao waanawalikisha kwa nchi, wema wa pamoja na msingi. Tunu ya wakati uliopita kwa hakika ni kuishi kupitia katika kipindi cha neema ya kutunza wale ambao wamekabidhwa, usawa wa urithi wa sanaa na utamasishaji wa thamani ya Italia unajengwa na nguvu moja ya kuweka matunda ya kisiasa na mkakati wa muda mrefu. Kwa namna hiyo Baba Mtakatifu amesema, wao kama Walimu wa Kanisa, wanasubiriwa na zoezi la kimaadili na kiraia kusambaza, kuhamasisha na kuongeza utunzaji na ulinzi wa nchi nzuri, ” (cfr F. PETRARCA, Canzoniere, CXLVI, v. 13).

Katika kuendeleza malengo hayo ndipo inatokea masuala ya kwanza ya kimaadili. Hayo hawali ya yote ndiyo kiini cha maisha ya msingi ambayo yanapumua thamani kamili, uwajibikaji na uwazi ( Gombo la Maadili n1) na kupendekeza kuishi, kushuhudia na kusambaza misingi hii yote kwa mantiki ya kijamii, kwa namna ya pekee ile ya kazi, Kupyaisha kazi kwa maana ya maadili, ina maana ya kupyaisha jamii nzima, kwa kupinga dhuluma na ulaghai ambao unatia sumu katika masoko, namna ya kuishi kiraia na maisha yenyewe ya mtu zaidi wali wadhaifu. Ili  kushuhudia hili, yaani thamani ya kibinadamu na kiinjili kwa kila mantiki na kila wakati ni lazima kuwa makini na uangalifu wa maisha binafsi. Na ipo haja ya ya kutambua maisha yako kamili kama utume ( taz. Wosia Gaudete et exsulate, 23).

Ni kwa njia ya roho hiyo ya kuchotaupendo wa ndugu unao choma ndani ya moyo kama petroli ya kitasaufi ambayo ni tofauti na mafuta yanayochimbwa katika ardhi,  kwa maana mafuta ya tasaufi hayaishi kamwe, badala yake yanaongezeka wakati yanatumika katika maisha yetu ya ushuhuda  ambayo yanaweza kuwa ya dhati , yenye uwezo wa kuwaka, kwa njia ya matendo ya huruma na upendo katika dunia yetu. “Nimekuja kutupa moto duniani”, anasema Yesu kwa mitume wake na kuongeza; “jinsi gani natamani moto huo uwe tayari umewaka! (Lk 12 49). Kwa maana hiyo, hata leo hii moto huo umekabidhiwa kwetu; na  sisi sote tumepewa Roho wa Bwana, Roho wa nguvu ambaye anajikita katika utakatifu na huruma: tazama,wakati uliokubalika ndiyo sasa; tazama siku ya wokovu ni sasa ! (2 Kor 6,2).

Baba Mtakatifu amesema kuwa, tumeongozwa katika hija hiyo lakini kwa shauku ya heri za Yesu katika Injili (Mt 5,3-11; taz Wosia. Gaudete et exsultate, 67-94): inatupeleka kutazana daima kwa upendo wa Yesu mwenyewe ambaye alitwaa mwili; inatuonesha kuwa, utakatifu hautazami roho tu, bali hata miguu ili kwenda kwa ndugu, na mikono kwa ajili ya kushirikishana nao. Tufundishwe sisi na dunia kutoamini au kuachwa kupelekwa na mawimbi ya upepo ambayo yanatuacha ardhini tukiwa na njaa ya mkate  na haki; utupeleke zaidi, si katika kuishi kwa kusazwa na kutumia hovyo, badala yake kuhamasisha kwa wote na kuinama kwa huruma juu ya wadhaifu. Bila kubaki katika starehe za uongo, kama zile za meza ya matajiri walio wachache, ili kuweza kupata mvua bila kutegemea ya ustawi kwa wote. Baba Mtakatifu amewatakia safari njema ya shirikishano na zaidi kazi njema.

Na sr Angela Rwezaula, 
Vatican News








All the contents on this site are copyrighted ©.