2018-06-12 16:33:00

Watoto lazima wacheze na kusoma, ole wao wanaowafanya watumwa!


Katika kuadhimisha siku ya kupinga ajira kwa watoto duniani kila ifikapo tarehe 12  Juni ya kila mwaka, Baba Mtakatifu Francisko amesema ajira ya watoto ni janga la kuzuia matumaini. Katika ujumbe wake  Baba Mtakatifu Francisko kwenye tukio kama hili,  mwaka 2013 alisema, watoto ni lazima wacheze na kusoma, wasali na kukua katika familia zao na ole wao, wanaowafanya watumwa”. Na mara nyingi amekuwa akisistiza juu ya jumuiya ya kimataifa kuweza kuingilia kati juu ya janga hili baya duniani.

Vilevile alikumbusha juu ya manyanyanyaso ya watoto kwenye ajira za nyumbani na kwamba ni  mada nyeti, hasa inayozidi kuongezeka katika nchi zilizo maskini. Ni zaidi ya milioni moja ya watoto na zaidi watoto wasichana ambao ni  waathirika wa ajira na manyanyaso ya siri ambayouwapelekea watoto kuteswa, kubaguliwa na kuwa kweli watumwa. Kutokana na janga hili, anasema, watoto wanayo haki ya kukua vema katika maisha yao. Inatia uchungu kuona kwamba, badala ya watoto kukua vema, watu wengi wanawafanya watumwa na watoto watulivu wana uwezo wa kuishi na kutazama maisha endelevu.

Kadhalika Baba Mtakatifu alitumia maeneo makali sana dhidi ya manyanyaso kwa ajili ya ajira za watoto wadogo, ikikumbukwa siku ya Katekesi yake ya tarehe 11 Juni 2014 kuelekea katika maadimisho ya siku hii, kwani  aliamsha mkono wake wa kushoto utafikiri ni refa wa mpira akiwa na kadi nyekundu, akinyoshea aliye chafua mchezo na kwamba ni kuchafua haki za watoto wadogo, lakini kilikuwa ni kijitabu kidogo cha Shirika la Kazi duniani (ILO),na aliwaomba  wote kwa sauti moja ili kupinga ajira kwa watoto wadogo.

Baba Mtakatifu Francisko alisema, mamilioni ya watoto wanalazimishwa kufanya kazi katika hali isiyo ya kibinadamu na aina nyingine za utumwa. Kwa njia hiyo aliwaalikwa mahujaji wote na waamini kusali kwa mama Maria ambaye aliweza kumpata na kumkumbatia mwanae Yesu Kristo mikononi mwake, kwa ajili ya watoto wanao nyanyaswa katika ajira na mateso yote.

Bado akisisitizia juu ya watoto, tarehe 7 Juni 2015, baada ya sala ya Malaika wa Bwana, Baba Mtakatifu Francisko alikumbushia, tukio hilo la tarehe 12 Juni,  kwamba watoto wengi duniani hawana uhuru wa kucheza na kwenda shuleni, badala yake wanaishia kunyonywa kama vifaa vya kutumia. Na hivyo aliwataka jumuiya za kimataifa kwa ajili ya kuhamasisha utambuzi wa haki za mtoto!

Watoto milioni 152 ulimwenguni wanalazimika kufanya kazi badala ya kwenda shule.  Umoja wa Mataifa (UN),  ulitangaza idadi hiyo ili kujenga uelewa juu ya ajira ya watoto  hasa tarehe 12 Juni Siku ya Kimataifa ya Kupambana na Ajira kwa Watoto. Kutokana na idadi kamili ya watoto wafanyakazi imezua wasiwasi mkubwa. Kwa mujibu wa ripoti ya Novemba 2017 ya Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF), karibu moja kati ya watoto wanne katika nchi zilizoendelea zaidi wanalazimika kufanya kazi zinazoathiri afya zao na maendeleo. 

Shirika la Kazi la Kimataifa (ILO) linaelezea kazi ya watoto kama "jambo linalozuia utoto wao, linaharibu uwezo wao, maendeleo yao ya kimwili na ya akili."Kulingana na ripoti ya ILO ya 2017, kuna wafanyakazi watoto milioni 152 kati ya umri wa 5-17. Ingawa kiwango cha ajira kwa watoto kinapungua kila mwaka, ni muhimu kutambua kuwa kiwango hicho hakipungua kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Hata hivyo tarehe 1 Mei wakati dunia duniani kote wanaadhimisha sikukuu ya wafanyakazi. Shirika la Kazi duniani ILO lilisema katika ripoti yake kuwa, watu Bilioni 2, sawa na asilimia 61 ya watu walioajiriwa, wapo katika ajira zisizo rasmi. Ripoti ya ILO ilieleza pia kuwa, watu hao wanatoka katika mataifa yanayoendelea kiuchumi, huku wanawake wakiwa ni Milioni 740.

Barani Afrika, asilimia 85.8 ya ajira sio rasmi huku Asia ikiwa katika nafasi ya pili kwa silimi 68.2. Aidha, ripoti hii, ilieleza pia kuwa idadi kubwa ya watu wanaojihusisha katika ajira hizo sisizo rasmi ni wanaume, huku wanawake wakiwa ni asilimia 58.1. Inaelezwa kuwa, kazi nyingi zilizo rasmi zinafanywa na watu wanaoishi katika maeneo ya vijijini. Pamoja na hilo ukosefu wa elimu kwa watu wengi pia inachangiwa pakubwa kutokana na hali hii. Watoto waendelea kufanyishwa kazi duniani: Baaada ya miaka mingi ya kupungua, sasa ajira ya watoto katika kilimo imeanza kuongezeka tena ikichochewa na migogoro na majanga yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi.

Hayo yameelezwa tarehe 12 Juni 2018  na shirika la chakula na kilimo FAO , katika kuadhimisha siku ya kupinga ajira kwa watoto duniani na kusema mwenendo huu hautishii tu mustakhbakli wa mamilioni ya watoto, bali pia unatishia juhudi za kutokomeza njaa na umasikini duniani. Kwa mujibu wa FAO siku ya mwaka huu inajikita kwa watoto milioni 73 kote duniani wanaoshiriki kazi zinazo hatarisha afya na usalama wao, iwe ni katika shughuli za uvuvi, kilimo, kukausha samaki kwa moshi, kazi za kuchomelea magari zinazowaweka watoto hao katika hatari kubwa. Akihojiwa na vyombo vya habari  Jacqueline Demeranville afisa wa FAO anayehusika na ajira zenye hadhi vijijini, amesema “Ushirikishaji wa watoto katika kazi zenye madhara ni ukiukawaji dhahiri wa haki zao, pia kuna athari za muda mrefu za mustakhbali wao , ajali moja tu inaweza kusambaratisha uwezekano wa kipato katika maisha yao yote , hivyo tunapoteza miaka mingi ya uzalishaji, uwekezaji katika elimu na mafunzo bila kuasahau athari binafsi” na kuhusu  athari hizo amesema, “Watoto sio vijana, miili na ubongo wao bado vitnakua na hivyo kuwaweka hatarini zaidi kwa madawa kama ya kilimo na pia wanakuwa na kiwango kikubwa cha kujeruhiwa kuliko wafanyakazi watu wazima, hivyo ulinzi maalum unahitajika”.

Hata hivyo amesisitiza kuwa: “Kipato kizuri na maisha yenye mneno kutawezesha wazazi kuwapeleka watoto wao shuleni badala ya kazini, pia tunahitaji kuhakikisha shule na mafunzo vipo katika maeneo yote na tunahitaji kufanya kazi na familia zinazojihusisha na kilimo, masula ya misitu na uvuvi ili kuelimisha zaidi kuhusu hatari zinzowakabili watoto na hatua za kuweza kuwalinda.”

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News








All the contents on this site are copyrighted ©.