Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Kanisa \ Kanisa Ulimwenguni

Utetezi wa utofauti, Indonesia ndiyo wito uliotolewa na viongozi wa dini !

Viongozi wa dini tofauti nchini Indonesia wameungana kutetea umoja wao wakati wa mfungo wa ramadhani - REUTERS

08/06/2018 11:36

Kutetea utofauti nchini Indonesia ndiyo wito ulio tolewa na viongozi wa madhehebu mbalimbali na utamaduni walio unganika hivi karibuni  wakati wa fursa ya mwezi wa Ramadhani katika Kanisa Kuu katoliki la Jakarta, ikiwa ni siku ya maadhimisho ya Pancasila ambayo ni kadi ya misingi mitano na kiini cha Katiba ya nchi ya Indonesia. Moja ya misingi mitano ya Pancila nchini Indonesia ni kuamini Mungu mmoja, kwa maana hiyo serikali inatambua rasmi waislamu, madhehebu ypte ya kiinjili ya kilutheri, wakatoliki, wabudha, wahindu, wa-Confucianism pia wazalendo wote wako huru kukiri imani yao.

Paroko wa Kanisa Kuu la Jakarta katika vyombo vya habari vya Kimisionari, Padre Hani Rudi Hartoko amesema, wao walipatwa  na mshangao wa mashambulizi ya kigaidi huko Surabaya na kwa maana hiyo mkutano huo wanajaribu kushona kwa upya ule mpasuko  na kuimarisha roho moja ya mshikamano.  Hiyo ina maana kubwa kwa waamini waislamu wa Indonesia ambao wanawakilishwa karibia asilimia 90% kati ya milioni 260 ya wakazi ambao wametaka kuadhimisha mwaka huu, ramadhani pamoja na waamini Wakristo na wabudha, ili kuonesha shauku ya kuishi pamoja kwa amani na kupinga mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea hivi karibuni katika mji wa Surabaya, katika wilaya ya Giava Mashariki na kusababisha vifo karibia 23 vya watu na wengine kujeruhiwa kwa njia ya mikono ya kikundi cha kigaidi cha kiislam.

Kati ya walioudhuria mkutano huo pia alikuwapo Alissa Wahid mtoto wa Rais Mstaafu wa Indonesia Abdurrahman Wahid, maarufu kama “Gus Dur”. Tukio hilo, amesema lilifikiriwa na kuanzishwa mara baada ya mashambulizi ya Surabaya, ili kuonesha kuwa Kanuni kuu a Pancasila bado inabaki yenye kuwa na nguvu. Naye James Smith Carrington mjumbe wa Nahdlatul Ulama, ambacho ni chama cha utamaduni wa kissuni na Baraza la Ulema la Indonesia amesema, dini ya kiislamu daima umekuwa ikiheshimu utofauti, sambamba na  Pancasila, kwa maana hiyo, kukutana katika Kanisa  Kuu Katoliki la Jakarta ni kuonesha kwa nguvu zote thamani hiyo. Aidha amesisitiza kwamba, nchi ya Indonesia inaishi kipindi cha dharura kwa ajili ya uvumilivu na wote wanaamini, lakini siyo sababu ya kuanza tena kutoa hukumu na kushutumiana au kupinga kile ambacho kilitokea wakati uliopita kwa Mtume Muhammad na Kadi ya Medina.

Kadi ya Medina, kama inavyojulikana, ni makubaliano yaliyoanzishwa hasa katika mji wa Oasis ya Yathrib, baadaye ukaitwa Medina, katika karne ya saba (VII). Katika tukio hilo, Muhammad aliwakaribisha watu wa dini nyingine, kama vile Wayahudi na Wakristo, ili waweze kuishi na kuendelea kwa uhuru wa dini yao katika eneo la Kiislamu.

Na Sr Angela Rwezaula 
Vatican News
 

08/06/2018 11:36