2018-06-04 13:27:00

Ninyi mtakuwa mashahidi wangu ndiyo mada inayoongoza mkutano wa CEC!


Tarehe 31 Mei hadi 6 Juni unafanyika Mkutano mkuu wa   XV wa Baraza la Makanisa Ulaya (CEC) huko, Novi Sad nchini Serbia katika wakiongozwa na kauli mbiu ya maneno ya Yesu:  ninyi mtakuwa mashahidi wangu, ambao unawashirikisha zaidi wawakilishi 400 kutoka katika makanisa 116 wanachama wa Baraza la Makanisa ya Ulaya (CEC), ambao ni Makanisa ya kiorthodox, katoliki, kianglikani na makanisa yote ya kiinjili yaliyopo bara zima la Ulaya, ambao wanajukumu la kujiuliza jinsi gani ya kushuhudia imani ya kikristo leo hii barani Ulaya.
 
Wakati wa kuwakilisha mkutano huo kwa vyombo vya habari, Mwenyekiti wa Baraza la Makanisa Ulaya , Askofu wa kianglikan Christopher Hill, amesema Ulaya ni tajiri ya Makanisa makuu, makanisa mengine, na mamonasteri, lakini wanagundua kuwa katika makanisa hayo hakuna watu. Kutokana na hilo, suala la kujiuliza, ni jinsi gani ya kuweza kupeleka Habari njema ya Injili Barani Ulaya leo hii , kwa wale ambao wanajikuta pembezoni mwa jamii, maskini  na yule anayehisi kuacha upweke na serikali.

Hali kadhalika mkutano utajikita kutafakari juu ya mada ya haki, makaribisho, ushuhuda, kwa njia hiyo, Askofu Hill amethibitisha kwamba, mambo hayo ndiyo kama ufunguo utakao zungukia mkutano wao mkuu. Kwa maana hiyo,  wataalam, na wawakilishi kutoka katika makanisa mbalimbali, wawakilishi wanaweza kukabiliana kuhusu haki ya uchumi kati ya juhudi za kweli za nchi, na namna ya uendeshaji katika kipindi cha kipeo kinachoikumba karibu nchi nyingi Barani Ulaya.

Hata hivyo kushirikiana na mantiki ya ushirikikishwaji katika suala kubwa la wimbi la wahamiaji kutoka Kaskazini ya Afrika na Nchi za Mashariki pia linazungumzwa kwa kina. Mkutano huo wa makanisa ya Ulaya wanataka kujikita kwa dhati kusikiliza wakristo wa Mashariki, ndiyo maana kati ya  watoa hutuba  wametoa fursa ya kuanza  kusikiliza ripoti ya Patriaki Mor Ignatius Aphrem II, wa Kanisa Kiorthodx  la Antiokia na Mashariki yote. 

Aidha Askofu Hill anasisitiza kwamba, hiyo ni kujiuliza maswali jinsi gani Ulaya inatoa jibu kuhusu janga la kusisimua la nchi za mashariki na Afrika Kaskazini. Pamojna na hayo ameonesha kuwa, si suala la kuhukumu, lakini ni kuona jinsi gani Ulaya inakabilia hata changamoto kubwa katika mantiki hiyo,  hivyo ni imani yao kuwa Ulaya ya Kaskazini na Magharibi wanaweza kweli kufungua mikono yao, kuwa wakarimu kukaribisha na kushirikishwa kila mgeni anayeingia, kumwona hawali ya yote kama ndugu na fursa ya pamoja katika maendeleo ya mwanadamu kamili na siyo usumbufu au mzigo katika dhana ya walio wengi wasiopenda kufungua milango yao.

Hata hivyo Kardinali Angelo Bagnasco, Mwenyekiti wa Mabaraza yaa Maaskofu Ulaya katika fursa hiyo amemwandikia ujumbe wake, Askofu Christopher Hill wa kianglikani ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Makanisa Ulaya (Cec,) kwamba, katika dunia hii ambayo daima inaonesha utofauti kwa upende wa mtazamo wa Mungu na ambaye wakati mwingine anageuka, kushuhudia Yesu ndiyo kweli moyo wa utume na nyenzo kuu katika ulimwengu mambo leo. Yesu yupo leo hii na atakuwapo siku zijazo za uekumene, katika mazungumzo kati ya Makanisa ya kikristo. Ka njia hiyo anamalizia kwamba, watu wote wanaalikwa kufuata Yesu bila kusita na kuwa mitume wake. Aidha  kutokana na kutokuwapo kwake, Kardinali Angelo Bagnasco katika mkutano huo, kwa niaba yake, ameshiriki Padre Martin Michalicek, Katibu Mkuu wa Mabaraza la maaskofu wa Ulaya.

Na sr Angela Rwezaula 
Vatican News








All the contents on this site are copyrighted ©.