2018-06-04 14:29:00

Mahubiri ya Kard. Filoni kwa wajumbe wa Baraza la Kipapa la Kimisionari


Neno la Mungu lililosomwa katika Liturujia ya Mtakatifu Justin shahidi, linatualika kutafakari juu ya uhusiano kati ya imani kwa Mungu, sala na utume katika maisha yetu. Katika safari kuelekea Mwezi Maalum wa Kimisionali 2019 tunahitaji kurudisha uwazi huo ambapo lazima kukua na kuongeza imani kwa  kuamini daima Bwana. Ndiyo utangulizi wa maneno ya mahubiri aliyoanza nayo Kardinali Fernando Filoni Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Unjilishaji wa watu wakati wa Misa ya hitimisho la kufunga mkutano  Mkuu wa Mwaka wa Shughuli za Kipapa za Kimisonari mjini. Ni katika misa iliyofanyika tarehe 1 Juni 2018 saa 11 Jioni Saa za Ulaya kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican.

Kardinali Filoni akiendela na mahubiri yake amesema, Bwana Yesu aliwafundisha mitume wake kwa njia ya maneno wazi na nyenye nguvu ambayo yalitangazwa wakati ule, ikiwa na maana ya utume wake kama mwana wa Mungu, Masiha na Mwokozi wa binadamu. Injili iliyosomwa leo hii, lakini katika mntiki ya  maneo ya Yerusalem,katika eneo la ukamilisho wa Pasaka ya Bwana. Injili inaonesha makutano ya Yesu katka hekalu mahali ambapo  ni pa sadaka ya shukrani na nyumba ya sala  ambayo inaendelea kuwaka shauku ya Wayahudi kukutana milele! Vilevile Yesu anapeleka kuoneshwa mji mwingine huko Betania, kijiji ambacho ni karibu na Yerusalem, mahali ambapo tunakutana na rafiki zake, Lazaro, Marta na Maria; nyumba yao Anaongeza Kardinali Filoni  ni mahali pa utulivu, urafiki na kushiriki furaha na uchungu wa kila siku. Lakini siku iliyofuata Yesu alirudia huko Yerusalemu.

Lakini katika hekalu anakuta wametengenza soko la kuuza na kubadilishana fedha, ndipo anajibu nyumba yangu itakuwa ni ya sala kwa ajili ya watu. Kwa maana hiyo  Kardinali anabainisha umuhimu kuonesha umakini wa mafundisho hayo juu ya nyumba yake iwe ni kwa ajili ya kusali watu wote,kwa kusisitiza mambo matatu. Kwanza Yesu amezungumza juu ya nyumba ambayo anatoka yeye. Je hiyo ni nyumba gani. Kwa kipindi hicho labda ilikuwa anaelezea  kwamba ni Hekalu la Yerusalemu, lakini siyo muhimu kusimama hapo anasema Kardinali badala yake ni kufikiria zaidi juu ya  neno la wakati ujao alilotamka kwamba, nyumba yangu itaitwa, kwa maana hiyo Yesu alifikiria nyumba nyingine. Yaani nyumba ya kiroho ambayo inajengwa na Roho Mtakatifu. 

Yeye alifikiria tayari Kanisa litakuwa na mwanzo kwa njia ya Roho Mtakatifu siku ile ya Pentekoste na ambaye  ataongoza Kanisa hilo hadi  miisho  ya dunia, ili katika nyumba yake, wote wanaweza kusikiliza Injili na kupata huruma. Jambo la tatu tatu la kukumbuka ni lile ambalo  Yesu anasema kwamba enendeni ulimwenguni yaani  ukatoliki, kwa maana nyumba yake ni katika  eneo la sala mahali ambapo wanaalikwa wote. Na ndiyo maana watu wote watatangaziwa Injili, Habari Njema na kuwalikwa kuingia katika nyumba hiyo iliyo wazi kwa ajili ya kupunzika, kwa ajili ya  sala, wema, neema, msamaha, mapatano na matumaini; mahali ambapo ni kukutana na Yesu anaye onesha Baba na Roho Mtakatifu katika sakramenti na kuwafanya watu wote wawe kweli wana wa Mungu. 

Kadhalika Karidina Filoni ameonesha juu ya tukio la mti ambao haukutoa matunda kwa wakati wake na kwamba hiyo ni ya hukumu ngumu ya mwisho, kutokana na kukisa  matunda kwa wakati wake. Ni mfano uli bora ambao unatolewa kwa wa mitume 12 kama ufunguo kwa wafuasi kwa maana ya kusema ndiyo wote na ambao wamaitwa kubatiza, kutangaza na kushuhudia Kristo. Iwapo mambo hayo yanakwenda kinyume Kardinali anathibitisha, ni ishara ya kuonesha utasai wa kutozaa  matunda na maisha yetu yanakuwa ya bure katika utume wa kimisionari.
Kardinali Filoni amesisitiza juu ya kufuata kwa hakika ushauri wa Yesu na kumwomba kila wakati bila kusita, wakati huo huo, wakumbuke kusamehe yote kwani Baba wa Mbingu anafanya hivyo kwanza. 


Amehitimisha akiwakumbusha kuwa wapo katika Kanisa Kuu na juu ya Kaburi la Mtume Petro  wakiadhimisha liliturujia Kumbukumbu ya Mtakatifu Justine shahidi. Mashuhuda wawili Petro na Jastine wa imani katoliki ya  Kristo na Kanisa ambalo leo duniani kote kutangaza Injili ambayo ni kwa ujasiri, kuteseka kwa ukimya, mateso , ubaguzi , kuchekwa, kudharauliwa hadi kufikia kifo dini. Lakini kwa msaada wa Yesu hatawacha kamwe washindwe na uvivu hadi kukosa matunda. Wawe walimu wa kimisionari na wajasiri, waamini na wajenzi wa nyumba ya kiroho kwa ajili ya watu wote katika hekalu la Mungu katika ulimwengu ambao unamdaharau au kumweka pembeni.
Na Sr Angela Rwezaula 
Vatican News








All the contents on this site are copyrighted ©.