Tarehe 1 Juni 2018, Saa 4.30 za asubuhi, Baba Mtakatifu Francisko alikutana na Rais Markus Söder wa nchi huru ya Baviera na wajumbe wake alioambatana nao mjini Vatican. Baada ya mazungumzo na utamaduni wa kubadilishana zawadi, Rais Soder amekwenda katika Monasteri ya Mater Ecclesiae ili kumsalimia Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI.
Aidha taarifa zinasema kuwa, mapema wiki hii, imezinduliwa kwa afla Picha ya Bikira Maria wa Rosari wa Guatemala kwa ushriki wa viongozi wa Vatican, wa Kanisa la Guatelana na viongozi wa Kidiplomasia waliopo Vatican, katika Bustani za Vatican. Mwenyekiti wa Utawala wa Serikali ya Mji wa Vatican Kardinali Guseppe Bertello, ndiye aliye adhimisha ufunguzi huo katika Bustani za Vatican ambapo pia ametoa shukrani kwa Rais wa nchi ya Guatemala na baadaye kubariki picha ya Bikira Maria baada ya kuifunua na kuizindua rasmi katika bustani za Vatican.
Picha ya Bikira Maria wa Rosari, ambaye ni msimamizi wa nchi ya Guatemala, inaingia kufanya historia ya kumbukumbu ya miaka 50 tangu madhabahu ya Mama Yetu wa Rosari, kutabarukiwa katika nchi ya Guatemala barani Amerika ya Kusini kwa utashi wa Mwenyeheri Papa Paulo VI.
Sr Angela Rwezaula
Vatican News
All the contents on this site are copyrighted ©. |