Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baba Mtakatifu Francisko \ Mahubiri

Papa: ibilisi anaharibu hadhi na kusababisha njaa na utumwa!

Binadamu leo hii anaendelea kuteswa kwa njia za ukoloni wa utamaduni, vita na utumwa unaotokana na ibilisi

01/06/2018 15:53

Tarehe 1 Juni 2018, Baba Mtakatifu Francisko ameadhimisha Misa Takatifu katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican, ambapo wakati wa mahubiri yake amejikita kutafakari juu ya kuteswa kwa wakristo ambao kila mwanaume na mwanamke wa leo wanaendelea kuteswa kwa njia za ukoloni wa utamaduni, vita na utumwa unaotokana na ibilisi, kwani leo hii uharibifu wa kina ni ule wa ulimwengu uliotawaliwa na utumwa, kwa maana hiyo, Baba Mtakatifu  anaomba Bwana ili aweze kutoa neema ya kupambana kwa njia ya nguvu ya Yesu Kristo, sura na mfano wa Mungu ambao upo ndani mwetu!
 
Baba Mtakatifu akitazama somo la kwanza kutoka, Mtakatifu Petro anayeelezea jinsi gani wakristo walikuwa wanateswa, hata kutumia moto, amethibitisha kwamba, karne hiyo ni sehemu ya maisha ya kikristo na kama ilivyo hata heri na hivyo Yesu aliteswa kwa ajili ya imani na kukiri Baba yake. Kuteswa huko lakini ni sawa na hewa inayovutwa na mkristo wa leo hii katika kuishi  maana hata leo hii kuna mashahidi wengi wanaoteswa kwa sababu ya upendo wa Kristo,  katika nchi nyingi, wakristo hawana haki. Hata ukivaa msabala utapelekwa mahabusu, watu wangi sana wamekamatwa na  waimeshia mahubusu, watu wengi wanahukumiwa kufa kwa sababu ni wakristo. Wapo watu wengi na idaidi kubwa ya mashahidi inazaidi kuongeza zaidi ya karne za kwanza. Pamoja na hayo, Baba Mtakatifu anabainisha kuwa habari hizo hazitangazwi, iwe ni luninga na magazeti hayaandiki mambo hayo, japokuwa  wakristo wengi wanateseka!

Halikadhalika, Baba Mtakatifu ametaja kuwa, leo hii kuna teso jingine kwa sababu ya kila binadamu kuwa sura ya Mungu aliye hai. Kila anayeteswa nyuma yake awe mkristo au maisha ya binadamu, yupo ibilisi anayetafuta kuharibu imani ya Kristo  sura na mfano wa Mungu. Tangu mwanzo alitafuta kufanya hivyo, katika historia ya kitabu cha Mwanzo, kwa maana alitaka kuharibu umoja kati ya mwanaume na mwanamke ambaye Bwana alimuumba, umoja ambao  unatokana na  sura na  mfano wa  Mungu. Alifanikiwa kufanya hivyo, kwa ulaghai na hila zake ambazo ni  silaha mbili anazotumia ibilisi. Pamoja na hayo leo hii kuna nguvu nyingine zinazo endelea dhidi ya mwanume na mwanamke, kwa sababu huwezi kupata sababu ya maelezo juu ya ongezeko la namna hii ya  uharibifu wa binadamu,ikiwa mwanaume na mwanamke.

Kadhalika Baba Mtakatifu amefikiria njaa ambayo inaharibu binadamu kutokana na ukosefu wa chakula japokuwa chakula kipo duniani. Unyonyaji wa kibanadamu na kila aina ya utumwa akikumbuka kuwa,  hivi karibuni aliona filam  moja iliyotengenezwa kwa maficho  ikielezea juu ya wafungwa wahamiaji ambao wanateswa, na  aina za uharibu na watumwa.  Ni wasiwasi wake hasa akikumbuka kwamba, utumwa huo unaendelea hata leo hii baada ya miaka 70, tangu kutiwa sahini ya mkataba wa haki za Binadamu. Kwa njia hiyo ametafakari hata juu ya koloni za kiutamaduni  kutokana na matafia fulani kuwapeleka  utamaduni mwingine na kuwondolewa utamaduni wa watu asilia  kwa kupendekezo mambo ambayo siyo ya kibinadamu. Baba Mtakatifu amesema, kazi hiyo ndiyo anataka ibilisi kuharibu hadhi ya binadamu na mateso.

Mwisho amejikita kutazama vita, ambavyo vinatumika kama zana ya uharibifu wa watu, sura na mfano wa Mungu. Lakini pia hata watu wenyewe ambao wanapanga mipango ya kufanya vita, kuwa na nguvu juu ya wengine. Wapo watu wengi wanaomiliki viwanda wa kutengeneza  silaha kwa ajili ya kuharibu binadamu, mfano na sura ya Mungu, mwili, madili  hata utamaduni. Wote wanaofanya hivyo ni sura na mfano wa Mungu, japokuwa ibilisi yupo nyuma yao. Nchi nyingi  leo hii zinaendelea kutesa watu wengi  kwa njia hiyo. Baba Mtakatifu anathibitisha kwamba hatuwezi kuruhusu kutazama hili. Leo hii mateso si kwa wakristo tu bali,  hata kwa watu wengine kwasababu ya uwepo wa wengine ambao pamoja kuwa sura na mfano wa  Mungu wanapendelea kuharibu sura hiyo, jambo ambalosiyo rahisi kutambua bila kuwa na sala, kwa maana hiyo inahitaji sala nyingi Baba Mtakatifu amehitimisha.

Na Sr Angela Rwezaula 
Vatican News

01/06/2018 15:53