Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Kanisa Barani Afrika \ Amani

Zambia:Maaskofu wako tayari kutoa mchakato wa mazungumzo kitaifa!

Maaskofu wa Zambia wako tayari kutoa machango wa mazungumzo ya kitaifa kati ya rais Lungu na mpinzani wake kwa ajili ya amani kuleta amani kamili ya nchi - AFP

31/05/2018 08:59

Katibu mkuu wa Baraza la Maaskofu nchini Zambia (ZCCB, Padre Cleophas Lungu amethibitisha juu ya  uwezekano wa Maaskofu kushirikiana katika mazungumzo ya kitaifa yaliyo anzishwa na Jumuiya ya Madola (Commonwealth) ili kuweza kuondoa mivutano ya kisiasa mara baada ya uchaguzi wa kisiasa mwaka 2016.

Jumuiya ya madola  (Commonwealth), imemtaja msomi na mwana dipolomasia kutoka Nigeria, IBrahimu Gambri ili kurahisisha mazungumzo kati ya Rais Edgar Lungu na kiongozi wa upinzani wa chama cha  Cha Maendeleo Kitaifa (United Party for National Development (UPND), Hakainde Hichilema aliyetolewa kifungoni mnamo tarehe 16 Agosti. Bwana  Hichilema alikamatwa na Polisi mwezi Aprili kwa sababu ya kutaka kufanya mapinduzi kwa kuzuia msafara wa rais. Kukamatwa kwake kulisababisha maandamano makali na hata kwa viongozi wa dini, hasa ile namna mbaya ya serikali iliyotumiwa wakati wa kumakata.

Maaskofu wanasema, wako tayari kushiriki katika kikundi cha mchakato wa mazungumzo, kwa mijubu wa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Zambia  kwa kujibu wito wa Rais Edga Lungu. Padre Lungu pia amethibitisha kwamba, Kanisa liko tayari kujihusisha na vyama vyote vya kisiasa katika mchakato na kutoa mwongozo wa kiroho kwa taifa.

Licha ya hayo Caritas ya Zambia pia imewaalika pia sehemu zote mbili katika mchakato wa mazungunzo yenye msingi wa thamani ya kikristo, kwa maana ya kuongozwa na ukweli, huruma, haki na amani. Kwa njia ya Mkurugunzi mtendaji wa Caritas Eugene Kabilika amesisitiza kwamba,  ni kwa njia ya mazungumzo ya kweli, yenye lengo la mapatano yanaweza kute suluhisho la kudumu. Hata hivyo mwaliko pia ni kwa ajili ya wazalendo wote wa Zambia , kwamba wawe na  matashi mema ya kushiriki katika matendo hai ya  na kuchangia mchakato huo ili wote waweze kufikisha nchi yao katika njia ya kweli.
Njia ambayo haki za binadmu zinaheshimiwa kwa dhati, uwazi na uwajibikaji unatiliwa mkazo na kusifiwa, maskini kwa namna ya pekee wakulima wanalindwa dhidi ya kuhamishwa kutoka mashamba yao kwa nguvu, pia kuwa na ushirikishwaji wa rasilimali za nchi kwa usawa. 

Na sr Angela Rwezaula 
Vatican News

31/05/2018 08:59