Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Vatican \ Hotuba

Papa apewa zawadi ya Picha inayohusu Wito wa Mwinjili Mathayo

Baba Mtakatifu amepokea picha inayohusu Wito wa Mtakatifu Matayo, kutokana na fursa ya filam ya Caravaggio, roho na damu iliyotengenezwa na ushirikiano wa Sky na Vyombo vya habari Vatican

31/05/2018 16:27

Baba Mtakatifu Francisko, amepewa zawadi ya picha inayohusu Wito wa Mtume Mathayo.Pia picha  hiyo imetengenezwa na wasanii kutoka huko Tifernate  huko Perugia nchini Italia. Zawadi hiyo ni kutokana na fursa  ya utengenezaji wa Filam moja inayoitwa “Caravaggio, roho na damu” ambayo inahusiana na maisha ya  wito wa Mtakatifu Matayo. Baba Mtakatifu amewatia moyo ili waendelee na mpango wa shughuli waliyo ianzisha, na kwamba  ni mipango inayopeleka utamaduni wa uzuri katika dunia na kuifanya sanaa iweze kuonekana katika maisha ya binadamu na kwa kila aina kijamii!

Tukio hilo, limefanyika tarehe Jumatano tarehe 30 Mei 2018 asubuhi kabla ya kuanza katekesi yake  Baba Mtakatifu ambapo, picha hiyo ilimeletwa na wawakilishi wakuu wa vyombo vya habari,  Sky na Vatan, pia hata mwanzilishi wa sanaa  Stefano Lazzari ambao kwa pamoja wameshirikiana kutengeneza Filam yenye jina la “Caravaggio, Roho na damu”.

Mhusika wa na mkurugenzi wa Filam ya kisaanii kutoka Shirika la Habari Sky, ameelezea juu ya furaha ya kukutana na Papa Francisko ambaye ameweza kwa ufupi kuelezea  juu ya Mtakatifu Matayo wakati akiwa kijana, kwamba alikuwa amebobea katika mambo ya fedha na kuhesabu, lakini akaangazwa na mwanga wa Mungu. Pamoja na hayo Pia mhusika huyo amethibitisha kuwa Filam hiyo imetengenezwa kiufundi kiasi cha kuweza  kutoa tafsiri ya picha hiyo ya “Caravaggio, roho na damu” kama alivyo weza kufafanua hata Baba MtakatifuNi shughuli ambayo imetendeka kiufundi kwa ushirikiana wa Sky na  Vyombo vya habari Vatican.

Vile vile amekumbusha kuwamba huo ni mkakati ulioanzishwa na vyombo vya Habari  na Vatican na Sky tangu 2013, kwa kutoa filam ya kwanza ya kisanii ya  Makumbusho Vatican, kwa kushirikiana na uongozi wa Jumba la Makumbusho Vatican; ya  pili ilikuwa ni Mtakatifu Petro na Makanisa Makuu ya Papa, Roma, iliyotolewa manmo mwaka 2016 kwa ushirikiano wa vyombo vya habari Vatican, wakati wa kuandaa Jubileo ya Huruma. Na mwaka 2017 wakiwa na uongozi wa Majumba ya makumbusho Vatican, waliweza kutoa filam iitwayo  “Taffaello – Mwanzo wa Sanaa”;  na nyingine  iko katika mchakato wa kutengenezwa ambayo itatolewa mwezi Oktoba yenye jina la Michalengelo- asiye na mwisho”.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News

31/05/2018 16:27