2018-05-30 15:30:00

Papa Francisko ameendelea kufafanua maana ya Sakramenti ya Kipaimara


Kwa kuendelea juu ya mada kuhusu Sakramenti ya Kipaimara, ninapendelea leo hii kuweka mwanga wa kina cha muungano wa sakramenti hii kama mchakato mzima wa mwanzo wa ukristo. Ndiyo utangulizi maneno ya katekesi ya Baba Mtakatifu Francisko,Jumatano 30 Mei 2018 katika Uwanja wa Mtakatifu Petro Vatican kwa waamini na mahujaji wote waliofika kuudhuria katekesi yake, ikiwa ni sehemu ya pili ya ufafanuzi wa Sakramenti ya kipaimara aliyoanza tarehe 23 Mei 2018.

Baba Mtakatifu akiendelea na ufafanuazi amesema:kabla ya kupakwa mafuta ya kiroho ambayo utoa uthibitisho na nguvu za neema ya Ubatizo,anayepokea kipaimara anaalikwa kujipyaisha kwa ahadi ambazo zilifanywa na wazazi na wasimamizi wake akiwa mdogo. Kwa sasa yeye wenyewe  anakiri imani ya Kanisa na kuwa tayari kujibu “nasadiki” kwa maswali yanayoulizwa na  askofu. Hao wako tayari kwa namna ya pekee kuamini katika Roho Mtakatifu ambaye ni Bwana mleta uzima, ambaye leo hii kwa njia ya Sakramenti ya Kipaimara anapewa  nguvu hiyo kwa namna ya kipekee, kama walivyo pewa Mitume siku ile ya Pentekoste. Ujio wa Roho Mtakatifu unatokea  katika mioyo ya wale  wanaodumu kwa moyo mmoja katika kusali ( Mdo  1,14),  hivyo  baada ya sala ya ukimya kwa jumuiya, Askofu wakiwa ameweka mikono yake juu ya wanaopokea Kipaimara akiomb  Mungu aweze kuwapa Roho Mtakatifu Mfariji. Roho ndiye  yule mmoja  (taz 1 Kor 12,4), lakini anafika kwetu akiwa na  utajiri wa zawadi ya   hekima, akili,  shauri, nguvu,  elimu, ibada na  uchaji wa Roho, kama ilivyosikika sehemu ya Biblia inayohusu zawadi ziletwazo na Roho Mtakatifu. 

Kwa mujibu wa Nabii Isaya (11,2), zawadi saba ni karama za Roho ambazo alipewa Masiha kwa ajili ya kutimiza utume wake. Hata Mtakatifu Paulo anaandika wingi wa matunda ya Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole na kiasi;. (Gal 5,22). Ni Roho mmoja anayegawa kwa wingi zawadi ambazo zinatajirisha Kanisa moja. Roho pamoja na utajiri uliopo wa tofauti  lakini wakati huo huo kwa namna moja hufanya umoja, yaani umoja katika utajiri wa kiroho ambao upo ndani ya wakristo, Baba Mtakatifu amethibitisha! Katika utumaduni ulioneshwa na Mitume, Roho ambaye anakamilisha neema ya Ubatizo anajidhihirisha vizuri zaidi  kwa njia ya kuwekea mikono juu yao ili waweze kupokea Roho Mtakatifu. (taz Mdo  8,15-17; 19,5-6; Eb 6,2).  Ishara hiyo ya kibiblia kwa dhati, inajieleza kwa wale wote wanaopokea Roho Mtakatifu kwa kufuata ishara ya kupakwa mafuta yenye manukato anayoitwa Krisma ambayo hutumika katika   katika nchi ya Mashariki na Magharibi hata siku zetu. (KKK 1289).

Mafuta ya Krisma ni aina ya dawa, pia mafuta ya kupaka ambayo yakipakwa au kuwekwa katika kiungo cha mwili yanatibu majeraha na viungo kutoa harufu nzuri. Kwa  thamani hiyo, ilichukuliwa kama ishara ya kibiblia na kiliturujia ili kuelezea matendo hai ya Roho anayetolewa wakfu na kuthibitisha ubatizo kwa  kuwapamba kwa karama nyingi. Sakramenti ya kipaimara inatokea kwa njia ya kupakwa mafuta ya Krisma katika paji la uso, kwa njia ya Askofu anaye wawekea mikono wakati huo akitamka: Pokea mhuri wa paji ya Roho Mtakatifu, anayekupatia zawadi hizo. Baba Mtakatifu anaongeza kusema: Roho Mtakatifu ni zawadi isiyo onekana  na mafuta ya krisma nichapa ya  mhuri unaoonekan!  Kwa kupokea katika Paji ishala ya msalaba kwa mafuta yanayonukia, mwenye kupokea kipaimara kwa namna hiyo anapokea chapa ya kiroho yenye kuwa na maaana ya kufananishwa kabisa na Kristo na kupatana neema ya inayaosambaratika kati ya waamini kwa manukato mema,“kwa maana sisi tu manukato ya Kristo, mbele za Mungu, katika wao wanaookolewa, na katika wao wanaopotea ( 2 Kor 2,15).  

Baba Mtakatifu amehitimisha akiwahimiza kwa ufupi kusikiliza mwaliko wa Mtakatifu Ambrosi wakati wa mahibiri yake kwa walio pokea kipaimara:“kumbuka umepokea mhuri wa kiroho… na utunze kile ulichokipokea. Mungu Baba amekupatia chapa, na kuthibitishia kwa Yesu Kristro, amekuwekea ndani ya moyo wako dhamana ya Roho (De mysteriis 7,42: CSEL 73,106; cfr KKK, 1303).  Ni zawadi ya aina yake ya Roho ambayo ni muhimu kupokea kwa shukrani kubwa na kuipa nafasi yake ya ubunifu. Ni zawadi ya kutunzwa kwa ungalifu na kuifuatia kwa upole, kuacha iweze kupenya kwa kina kama vile vile nta ikiwa inawaka upendo, kwa ajili ya kutafakari Yesu Kristo katika ulimwengu wa sasa (taz Gaudete et exsultate, 23).

Na Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!

 








All the contents on this site are copyrighted ©.