Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Habari \ Habari za Kimataifa

WHO na Bank ya Dunia waunda bodi ya kudhibiti magonjwa ya mlipuko!

Who na Bank ya Dunia wameunda bodi ya kudhibiti magonjwa ya mlipuko kama vile Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa wakati huu - REUTERS

25/05/2018 12:57

Shirika la Afya ulimwenguni WHO na Benki ya dunia wameunganisha jitihada zao na kuunda bodi itakayosaidia kuimarisha usalama wa afya duniani. Bodi hiyo itakayoongozwa kwa pamoja na aliyewahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Gro Harlem Brundtland na Katibu Mkuu wa shirikisho la vyama vya msalaba mwekundu duniani, ICRC, Elhadj As Sy, itakuwa na jukumu la kufuatilia mara kwa mara mwelekeo wa magonjwa kama njia ya kuepusha kuzuka kwa magonjwa ya mlipuko na ya dharura.

Uzinduzi huo umefanyika  mapema wiki hii huko Geneva, Uswiss na kushuhudiwa na wabunifu wa mpango huo ambao Bw. Tedros Ghebreyesus,  Mkurugenzi Mkuu wa WHO,  na Rais wa Benki ya Dunia Bw. Jim Yong Kim ikiwa ni kandoni mwa mkutano wa 71 wa Baraza Kuu la WHO! Na wakati wa mazungumoz yao, Bw.Ghebreyesus  amezungmza juu ya  umuhimu wa kuwa na bodi hiyo akitoa mfano wa magonjwa ya mlipuko kama Ebola nchini Jamhuri ya kidemokasia ya Congo, DRC, ambako WHO  na washirika wamekuwa wakisaidia kukabiliana nao. 

Katika kusisitizia zaidi, Bw.Ghebreyesus ameongeza kusema kuwa, mfumo waliokubaliana utafanya kazi ya kuratibu na pia  kujiandaa mapema kwa kuhakikisha wahusika wako tayari kukabiliana na milipuko hiyo na hivyo kuokoa maisha ya wengi. Naye Daktari Kim amesema kwa muda mrefu wamekuwa wakichukua hatua za dharura kushughulikia milipuko lakini wakati huo wakikamilisha hatua hiyo wanasahau kufuatialia. Hivyo amesema, mfumo walioanzisha utasaidia ufuatiliaji na pia kuandaa mazingira ya tahadhari ya mapema ili kuepusha kuzuka tena kwa magonjwa ya milipuko siku za mbeleni.

Na wakati huo huo hata haki za binadamu na  mizozo kote duniani zinaibua vitisho na machungu kwa mamilioni ya raia wakiwemo wanawake, wasichana, wanaume, wavulana na watoto. Hiyo ni kwa mujbu wa Ni kauli ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres wakati akihutubia kikao cha Baraza la Usalama kilichokutana 24 Mei 2018 mjini  New York, Marekani kujadili ulinzi wa raia kwenye mizozo ya kivita. Bwana Guterres amesema, zaidi ya watu milioni 128 kote ulimwengni wanahitaji msaada wa haraka wa kibinadamu na idadi hii kubwa inatokana na mizozo. Mwaka jana Umoja wa Mataifa ulirekodi vifo na majeruhi zaidi ya 26,000 miongoni mwa raia katika nchi sita tu zilizoathiriwa na mizozo duniani, na ambapo, Katibu Mkuu amezitaja nchi hizo kuwa ni Afghanistan, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Iraq, Somalia na Yemen.

Pamoja na hayo Katibu Mkuu anaonesha pia madhara mengine kwamba, raia hao hao kwenye maeneo ya mizozo wanakumbwa na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu ikiwemo kubakwa na aina nyingine za ukatili wa kingono. Ametolea mfano Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kusema, Umoja wa Mataifa ulirekodi zaidi ya visa 800 vya ukatili wa kingono unaohusiana na kuwepo kwa mzozo, ambapo ni ongezeko kwa asilimia 56 ikilinganishwa na mwaka uliotangulia. Kandokando ya ukatili wa kingono, vifo na majeruhi, mizozo imeendelea kuwaong’oa watu kutoka kwenye makazi yao na kusalia bila kufahamu hatma yao. Bwana Guterres kwa namna hiyo ametumia fursa hiyo kupazia sauti kali vitendo vya pande kinzani kwenye mizozo katika kuangusha au kufyatua makombora yao kwenye makazi ya watu kinyume na sheria za haki za kimataifa za kibinadamu.

Mashambulizi hayo kwenye miji na majiji amesema kwamba, yanaua na kujeruhiwa makumi ya maelfu ya raia kila mwaka na kusambaratisha makazi na miundombinu muhimu ikiwemo ile ya maji na nishati. Kwa mantiki hiyo Katibu Mkuu ametoa mapendekezo matatu, kwanza, serikali zitunge sera za kitaifa za kulinda raia kwenye mizozo, pili nchi wanachama ziunge mkono Umoja wa Mataifa na wadau wengine katika kushirikiana na vikundi visivyo vya kiserikali kutunga sera, mifumo na mipango ya kulinda raia.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!

25/05/2018 12:57