2018-05-25 17:31:00

Askofu mkuu Santo Rocco Gangemi ateuliwa kuwa Balozi wa El Salvador


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Santo Rocco Gangemi, kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini El Salvador. Kabla ya uteuzi huu, alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Guinea na Mali. Itakumbukwa kwamba, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto wa kumi na sita, tarehe 27 Januari 2012 alimteua Monsinyo Santo Gangemi, kuwa Balozi mpya wa Vatican kwenye Visiwa vya Solomoni pamoja na kumpandisha hadhi kuwa Askofu mkuu na kuwekwa wakfu kama Askofu mkuu hapo tarehe 17 Machi 2012.

Tarehe 6 Novemba 2013 akateuliwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Guinea na tarehe 5 Februari 2014 akateuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Balozi wa Vatican nchini Mali. Askofu mkuu Santo Rocco Gangemi alizaliwa tarehe 16 Agosti 1961 huko Messina, Kusini mwa Italia. Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi, akapadrishwa tarehe 28 Juni 1986. Kuanzia tarehe Mosi, Julai, 1991 alianza kutekeleza utume wake katika medani za kidiplomasia ndani ya Kanisa huko: Morocco, Italia, Romania, Cuba, Chile, Ufaransa, Hispania na Misri.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Vatican News

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.