Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Kanisa Barani Afrika \ Amani

Nchini Nigeria wamefanya maandamano ya mshikamano na wakristo!

22 Mei nchini Nigeria wamefanya maandamani ya amani na mshikamano na Wakristo - AP

23/05/2018 13:42

Katika  nchini Nigeria hali halisi ya nchi siyo nzuri  kabisa kutokana na matukio mabaya dhidhi ya binadamu. Kwanza ni lile tishio la Boko Haram ambalo kwa kipindi kirefu limekuwa janga kubwa kwa binadamu wengi nchini huko, ikiwemo matukio ya utekeji nyara wa watoto wa shule na watu mbalimbali katika nchi hiyo; pili kundi la wachungaji wa mifugo wa Kifulani kwa ukatili wa kupindukia kuwaua watu wasio na hatia wakiwemo hata wachungaji wa Kanisa.

Kutokana na matukio hayo tarehe 22 Mei 2018, yamefanyika maandamano ya amani  na mshikamano ili kupinga  kila aina za vurugu dhidi ya wakristo ambao kwa siku nyingi wamekuwa waathirika na kuteswa na kundi la wachungaji wa mifugo wa kifulani nchini humo. Maandamano hayo yamefanyika siku ambayo pia ilikuwa ni mazishi ya mapadre wawili walio uwawa na kundi la wafulani mnamo tarehe 24 Aprili 2018.

Mandamano hayo yameandaliwa na Baraza la Maaskofu wa Nigeria ili kuhamasisha taasisi za usalama kitaifa, kuwa na ulinzi na usalama wa raia wake. Taarifa zinaonesha kwamba, tangu mwanzo wa mwaka huu, watu 100 wamepoteza maisha yao kutokana na mashambulizi ya wachungaji wa kifulani katika kanda ya kiislam. Na moja ya tukio la mauaji kama hayo ni  lile la tarehe 24 Aprili2018 katika Parokia ya Mbalom, mahali ambapo pamoja na muaji  yaliyo fanyika watu 20 walijeruhiwa!

Watu wengi wameitikia wito wa Baraza la Maaskofu nchini Nigeria kuandamana kwa amani na mshikamano katika hatua hizo za kupinga vitendo viovu dhidi ya maisha ya binadamu wasio kuwa na hatia. Maaskofu, mapadre, watawa , waseminari kila kona ya taifa imeungana kwa pamoja tamko hilo la maaskofu wakiomba nguvu za serikali kuingilia katikwa haraka  ili kulinda usalama wa raia wa nchi ambaye anazidi kuteswa na kuuawa bila kujali thamani ya maisha ya binadamu amnaye ni mfano na sura ya Mungu, mwenye haki na hadhi yake kama binadamu anayetakiwa kuishi hadi siku yake ya mwisho wa maisha yake, hali kadhalika kulindwa heshima yake na utu wake na  misingi ya haki kwa kila mtu anayeishi katika taifa hilo na mahali popote.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News

23/05/2018 13:42