Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Kanisa Barani Afrika \ Amani

Maaskofu wa Cameroon wametoa wito ili kusitisha vurugu na ghasia nchini!

Nchini Cameroon kumekuwapo na mandamano ya kile cha kudai haki dhidi ya ubaguzi wa kati yao wa lugha mbili ya kingereza na kifaransa - REUTERS

23/05/2018 13:25

“Sitisheni kila aina za vurugu na hacheni kutuua:sisi ni ndugu wote kaka na dada, tuanze safari ya mazungumzo na mapatano, haki na amani”. Ndiyo wito wa wa nguvu ulio tolewa hivi karibuni na Baraza la Maaskofu nchini Cameroon kufuatia  hali mbaya inayo kumba kipeo cha siasa ya  kijamii, kwa miezi kadhaa kuzidi kuongezeka kasi zake hasa katika Kanda inayozungumza lugha ya kingereza nchini humo.  Maaskofu wa Cameroon kwa barua iliyotiwa saini na Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Cameroon, Askofu Mkuu Samuel Kleda wa Jimbo Kuu la Duala wanasema kwamba, katika maeneo hayo vurugu ni nyingi na zisizo za kibindamu na ukatili wa kiajabu zenye mizizi ya wapinzani ambayo inazidi kuwa tishio kwa wote.

Kanda ya lugha ya kingereza huko Kusini mashariki na kaskazini Mashariki, wanahisi kwa miaka mingi ubaguzi wa Serikali ya kati, hasa kutokana na ukosefu wa kutokuweza kutumia lugha ya kingereza katika mahakama na  mashule mahalia katika nchi ambayo sehemu kubwa inaongozwa kwa lugha ya kifaransa. Tangu mwaka 2016 kanda hizo mbili ya Kingereza zimekuwa na mivutanano kiasi za kujitangazia uhuru wake kutoka katika Serikali ya Kati ya Rais Paul Biya.

Tangu wakati huo, kipeo hicho kikaanza mfululizo wa  mapigano makali kati ya nguvu za serikali na vyama vya kudai huru, ambapo hadi sasa vimesababisha waathirika karibia 150 , kati yao 64 ni raia, 150,000 wamerundikana mahali pamoja ndani ya nchi na karibia wakameruni26,000 ni wakimbizi nchini Nigeria. Pamoja na  taarifa hiyo lakini idadi inawezekana ikawa kubwa zaidi kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa kwamba wakimbizi walioko Nigeria wanaweza kufikia 40,000, sehemu kubwa ikiwa ni wanawake na watoto. Na pia wanathibitisha kuwa, wakimbizi 5 kati ya 100 wanawezekana kuwa na mahali pa usalama,wanaobaki wanalala katika majengo yaliyo achwa wazi, au kulala nje bila nyumba.

Kutokana na hali mbaya, maaskofu wa Cameroon wanaomba hasa suala hili kuingilia kati kwa haraka iwezekanavyo ili kuweza kuhepuka kipeo ambacho kinaweza kuleta vita vya wenyewe kwa wenyewe ndani ya nchi na visivyo kuwa na maana wala msingi.  Pamojana na hali halisi ya wakaimbizi, hata maaskofu wa Nigeria wanahimiza hasa kuomba msaada kutokana na wakimbzi katika mikoa ya Taraba, Benue, Akwa-Ibom na Cross River, na kwamba hali mbaya ya umaskini unazidi kuwakumba hasa jumuiya mahalia. Hawana chakula, maji ya kunywa na mahali pa kulala. Watu wengi ni wagonjwa na wanakufa bila kuwa na matibabu, kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Vijiji Nigeria katika Shirika la habari za kimisionari Fides. 

Aidha taarifa inasema kuwa, hakuna hata ruhusa ya mwandishi yoyote wa habari kuweza kuingia katika maeneo yenye kipeo, lakini kwa bahati nzuri wapo mashahudua wa kuona moja kwa moja,ambao wamelazimika kukimbia nyumba zao  na wanathibitisha majanga haya kwamba wengi wako mbaroni bila hatia, mauaji na mateso kutoka katika makundi ya wadai uhuru, vilevile vurugu za nguvu kwa watoto na unyanyasaji kijinsia.

Kwa sasa ni Caritas ya Cameroon kama shirika ka kibinadamu lililopo katika kanda hizo zenye  matukio ya vurugu na ghasia kipofu. Caritas wanajaribu kutoa chakula, maji na vifaa vya afya, nyezno za kuweza kuwapatia mahali pa kulala hakuna kwa maana hiyo wanatoa wito wa kuomba msaada wa dharura ili kuweza kuwasaidia wakimbizi 5000 wa Cameroon walioko na ambao watafika  nchini Nigeria. Kwa hakika hali ni ya kutisha sana kwa maana watu badala ya kulima katika mashamba yao ya kilimo, wanalazimika kukumbia kujificha katika misitu kutokana na kuogopa kuwawa, kwa miezi hii nyumba nyingi zimechomwa moto na watu wengi kutekwa nyara au kuwawa! Hakuna usalama hata kidogo, watu wanaishi kwa hofu na kukimbia kila siku!

Na Sr Angela Rwezaula 
Vatican News

23/05/2018 13:25