2018-05-23 13:03:00

Ili kutambua mapenzi ya Mungu ni vema kuwa na kiongozi wa kiroho!


Askofu Marcello Semeraro wa Jimbo la Albano nchini Italia na Katibu wa  Sinodi ya Maaskofu, ametoa hotuba yake hivi karibuni  katika Semina inayohusu maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtumishi wa Mungu Askofu Tonino Bello apate daraja la Upadre. Semina hiyo imeongozwa na  mada: “ ushuhuda na  Kirene wa Furaha” ambapo amesema kuwa, sehemu yenye  nguvu na ambayo ni  kazi ya kuelimisha ili kuweza kukutana na Mungu moja kwa moja, ni elimu ya mshangao, ambayo inahitaji makutano ya mimi na wewe ili kuweza kuhisi ule umoja na Mungu na kuhisi kusindikizwa kweli na uwepo wake, lakini kazi hiyo ya kutambua mapenzi ya Mungu ni vema kuwa na kiongozi wa kiroho, anaye sindikiza hatua za mchakato wa mang'amuzi kamili ya miito.

Kadhalika katika hotuba hiyo, Askofu Semeraro ametafakari kwa kina juu ya wale ambao wanapewa majukumu ya kusindikiza kazi ya miito na  ambapo anasisitiza ya kuwa leo hii ni jambo nyeti na msingi, wakati Kanisa Katoliki likijiandaa na Sinodi ya Maakofu kwa ajili ya vijana mwezi Oktoba mwaka huu. Anafafanua kuwa maandalizi ya kwanza yamefanyika ili kuweza kutimiza kwa hakika jinsi gani ya kuweza kung’amua tasaufi za kiutamaduni na ambayo pamoja na umuhimu wake, lakini pia ulazima wa usindikizwaji wa mtu hadi anafikia ukomavu kamili wa mang'amuzi hayo.

Kwa maana hiyo amethibitisha kuwa, inahitaji maendeleo halisi katika kutambua dhamiri ya mapenzi ya Mungu ili kuweza kufikia kwa dhati ule  mchakato kamili wa makutano ya moja kwa moja na Kristo. Lakini kazi hiyo kwa dhati haiwezekani iwapo hakuna mtu wa kusindikiza kiroho ili kufikia kweli mang’amuzi kamili na binafsi.

Akitazama kwa kina sura ya msindikizaji wa miito kwa mujibu wa maandishi ya Askofu Tonino Bello aliyoandika mwaka 1990 kuhusiana na  wito, katika mada :“nitakupenda hadi juu ya mwamba”,  Askofu Semeraro anathibitisha kwamba aliandikia akiwa na malengo mawili: “wito” na “ahadi”. Malengo hayo anafafanua kuwa yanatoa mwaliko wa kutazama kazi ya ubunifu ya Mungu na kila mmoja mbele yake ambaye ni mtu wa aina ya pekee, asili na asiyerudiwa tena !  Kwa maana hiyo anasititiza Askofu Semeraro, juu ya kazi kubwa binafsi inayo hitajika kufanya ili kwa matumaini pawepo kweli utambuzi yakini ambao umesikimikwa ndani ya moyo wa kila mtu tangu kuubwa kwake.

Na Sr Angela Rwezaula

Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.