2018-05-23 12:44:00

22 Mei ya kila mwaka ni kumbukumbu ya Mtakatifu Rita mama wa upendo!


Katika kumbukumbu ya Liturujia ya Mtakatifu Rita ambayo hufanyika kila ifikapo tarehe 22 Mei, hata kwa mwaka huu kama utamaduni, maadhimisho ya Misa kuu yameudhuriwa na mamia ya mahujaji na waumini mahalia huko Cascia nchini Italia, mahali ambapo baada ya misa, wamebariki mawaridi, kama ishara ya utakatifu na kesi mbalimbali zisizowezekana. Sababu ya kubariki maua hayo,ni kufanya kukumbuka ya  tendo la miujiza wa kuchanua mawaridi wakati wa kipindi cha baridi enzi za Mtakatifu Rita, akiwa mtawa wa ndani wa Shirika la Mtakatifu Agostino; vilevile ni ishara ya mwanamke mwenye  kuchanua imani yake na kutoa arufu nzuri ya Kristo japokuwa amezungukwa na miiba katika safari ya maisha! 

Aliye ongoza Misa Takatifu ya Sikukuu ya Mtakatifu Rita kwenye uwanja wa Madhabahu ya Mtakatifu Rita, alikuwa ni Kardinali Amato Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la kuwatangaza watakatifu. Wakati wa mahubiri yake, amekumbuka, Mtakatifu Rita kwa kina hasa katika kuchambua maisha yake  ya ujasiri mkuu na kusema kuwa  Yeye anatoa ujumbe rahisi kwa maana kama mama, anawaalika wanandoa kuwa waaminifu na mafunzo ya kikristo kwa watoto wao. Kwa wazazi pia Mtakatifu Rita anawawaalika kuwa na busara katika imani na ushuhuda wa kikristo; kwa vijana anawashauri wawe na matumaini ya wakati ujao na kuwa wakarimu katika kusamehe, wakati huo huo kushinda mantiki za chuki na vurugu; kwa wagonjwa anawasihi kuwa Injili iwe ndiyo nguvu na utulivu wa kubeba msalaba kila siku; kwa watawa anasisitiza juu ya uaminifu wa wito wao walio upokea na furaha ya umoja; na kwa wote anawakumbusha utakatifu wa kweli. 

Mamia ya mahujaji waliofika katika maadhimisho katika mji wa Cascia  ulio haribiwa na tetemko la ardhi manamo mwaka 2016, wamefika kwa moyo wote kusali  katika madhabahu ya  Mtakatifu Rita ambaye anapendwa na watu wengi duniani! Pamoja na waamini na mahujaji walioshiriki Misa Takatifu iliyo ongozwa na  Kardinali Angelo Amato pia walishiriki maadhimisho hayo Askofu Mkuu Renato Boccardo wa Jimbo la Spoleto-Norcia, Padre Alejandro Moral Anton Mkuu wa Shirika la Mtakatifu Agostino na Padre De Michieli  wa Shirika la wagostino wa Kanda ya Italia.

Na Sr Angela Rwezaula 
Vatican News








All the contents on this site are copyrighted ©.