2018-05-22 13:18:00

Kard.Baldisseri: Madhabahu ni mahali pa mang'amuzi ya miito kwa vijana!


Katika maadhimisho ya Sikukuu ya Pentekoste Makanisa yote ulimwenguni wameadhimisha kwa shangwe kuu, ambapo wachungaji wa Mungu wamepata fursa kubwa ya kuweza kutazama kwa karibu wito wa Kanisa kwa mantiki ya Yesu ambaye kabla ya kupaa mbinguni alikuwa ametoa ahadi ya kuwatumia Roho Mtakatifu na  ambaye angewakumbusha yote ambayo alikuwa amewafundisha wakati wa kutangaza Injili hadi miisho ya dunia. Tarehe 20 Mei 2018 iliadhimishwa misa  kwenye Madhabahu mpya ya Mtakatifu Francisko wa Assisi ya kuvua nguo, ambapo ilikuwa ni misa ya aina yake na yenye maana kuu ya kujikita kutazama utume kwa mantiki ya sasa. Katika historia, Madhabahu hiyo inafungamana na kumbukumbu ya Mtakatifu Francisko ambaye alipenda  umaskini wa dhati hadi kuvua nguo zake mbele ya umati na kumrudishia Baba yake Petro Bernardone ili aweze kujikabidhi na kupokelewa  mikononi mwa  Askofu Guido wa Assisi kwa wakati ule. 

Misa iliongozwa na Kardinali Lorenzo Baldissseri Katibu Mkuu wa Sinodi  ya Maaskofu. Na wakati wa mahubiri yake, ametoa wito wa kurudia mambo msingi hasa kwa Mungu ambaye kwa njia ya Yesu Kristo ameonesha   upendo wake mkuu na kwa mfano wa Mtakatifu Francisko wa Assisi. Katika kutazama kwa kina historia ya kuvua nguo ya Mtakatifu Francisko wa Assisi ndipo Kardinali Baldisseri ametumia fursa hiyo kutazama kwa kina maeneo hayo muhimu hasa kwa kuzingatia suala la vijana, mahali ambapo, amesema kuwa,  Papa Francisko amependelea kufanya Sinodi ya Maaskofu inayo wahusu ambayo inayotarajiwa kuanza tarehe 3 hadi 28 Oktoba Vatican. Kardinali amesisitiza umuhimu madhabahu hiyo hasa kwa ajili ya vijana na zaidi  wale ambao wanakwenda Asisi katika hija ili kutafuta maana ya maisha yao wakiwa wamejazwa ndani yao uchungu, na wakati mwingine utupu kutokana na mambo mengi ndani ya jamii ambayo inaleta ugumu na uzito wa mambo mengi na ili waweze kupata maana halisi ya maisha yao.

Hata hivyo Kardinali Baldisseri amekumbuka barua ya Baba Mtakatifu Francisko aliyo waandikia maaskofu wa Assisi akiwakabidhi Madhabahu hiyo ya utume wa kujikita na ambao leo hii ni muhimu sana, utume kwa ajili ya vijana, mahali pa kufanyia mang’amuzi ya miito. Na hatua za Sinodi inatarajiwa kujikita ndani ya tendo jipya lenye mtindo  wa mantiki ya kiutamaduni katika miito na matokeo ambayo yanaunganisha na kuonekana zaidi katika mfumo kati ya uchungaji wa vijana na uchungaji wa miito. Baba Mtakatifu anakazia umuhimu wa mahitaji ya kupokelewa kwa vijana, kuthaminishwa na kusindikizwa. Kwa maana hiyo Madhabahu hiyo inajinyakulia thamani kubwa msingi, mahali ambapo vijana wanaweza kusaidiwa kufanya mang’amuzi ya miito yao. 

Na mwisho Kardinali Baldisseri amekumbusha pia mahitaji ya huduma ya mang’amuzi makini kwa wale ambao wanapewa majukumu ya kuwasindikiza vijana kwa namna ya kwamba kizazi kupya kiweza kutambua kung’amua sauti ya Mungu kwa ajili ya maisha yao: “Ili vijana waweze kung’amua vema wito wa Mungu katika maisha yao wanahitaji wahudumu ambao ni makini na walio jifunda vema ili kuweza kuwasindikiza vijana wajikite katika hatua zao msingi”( Evangelii gaudium).  Utambuzi huo unakuja kutoka ndani kwa njia ya  Neno la Mungu ambalo ni taa katika hatua zetu na kutafsiri ya kwamba, Bwana anazidi kutuma njia ya Roho Mtakatifu ili waweze kuachagua njia kwa ujasiri, uhuru na uwajibikaji. 

Na Sr Angela Rwezaula 
Vatican News

 








All the contents on this site are copyrighted ©.