2018-05-22 13:50:00

Barua ya Maaskofu Italia:Mabadiliko ya kina katika tukio nchini mwetu!


Barua ya Baraza la Maskofu wa Italia kwa Jumuiya kikristo katika maadhimisho ya miaka 25 ya Waraka uliokuwa na jina “ Nilikuwa mgeni na mkanikaribisha “( 1993-2018), ambapo wameandika Barua mpya ambayo  imepewa jina “ mabadiliko ya kina” katika tukio nchini mwetu". Nia na msukumo wa kuandika kwa upya ni kutokana na mwendelezo wa ishara za matukio ya wahamiaji  katika nchi ya Italia. Na katika utangulizi wa barua hiyo,  Tume ya Baraza la Maaskofu wa Italia katika kitengo cha wahamiaji, wanatoa mwaliko kwa Jumuiya nzima ya kikristo nchini Italia kuwa wakarimu na kuondokana na hofu, pia kuweza kujibu swali la Mungu aliye uliza Kaino yuko wapi ndugu yako? ( Yh 4,9). Suala ambalo hata Baba Mtakatifu Francisko alirudia kutafakari wakati alipotembelea huko Kisiwani Lampedusa mnamo tarehe 8Julai 2013.

Mwaka 1993 wahamiaji walikuwa ni tukio jipya na dharura ambapo ilikuwa ni vigumu bado kupoka ukuu, hata  matarajio ya uhamiaji huo. Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Ndani  ya nchi ya Italia, wahamiaji nchini walikuwa 987,405, sehemu kubwa ikiwa ni kutoka katika Umoja wa nchi za Ulaya  hata Ulaya ya Mashariki. Lakini leo hii wahamiaji katika nchi ya Italia imekuwa tukio la kushangaza hasa ongezeko lake, hadi kufikia miaka ya mwisho kuona wahamiaji wenyewe ni waitaliani kuelekea sehemu nchi nyingine. Kwa mujibu wa takwimu pia zinaonesha kuwa, mwanzoni mwa  mwaka 2016 wahamiaji wameongezeka milioni 5 ya wakazi wote sawa na asilimia 8,3%. Na miaka mitatu ya mwisho idadi ya wahamiaji imebaki sawa na kuongezeka wahamiaji wanao omba makazi, wakati mwaka wa mwisho waitaliani 124,000 wamehamia katika nchi nyingine. 

Barua mpya ya  Maaskofu inaelezea kuwa, katika Ujumbe wa Siku ya wahamiaji na wakimbizi duniani mwaka 2018, Baba Mtakatifu Francisko katika mwendelezo wa utume wa Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI na Mtakatifu Yohane paulo II amesisitiza kuwa waamini wote na watu wenye mapenzi mema wanaalikwa kujibu changamoto  za nyakati  za uhamiaji  kwa ukarimu, upendo, busara, uvumilivu, kila mmoja kwa katika wajibu.

Maaskofu wa Italia katika maelekezo yaa kichungaji 2010-2020 wanakumbusha kuwa matukio ya wahamiaji bila shaka ni moja ya changamoto kubwa ya kuelimisha. Wanao utambuzi ya kuwa hata wakristo mbele ya tukio la ulimwengu la wahamiaji katika fursa na matatizo yake, siyo rahisi kuzuia na kutengeneza kiwanda cha majibu, lakini wote wanaweza kukukabiliana kwa hali halisi na akili, ubunifu, shauku na wakati huo huo kuwa na busara, ili kuzuia kutoa majibu suluhisho la urahisi tu. Aidha wanatambua jinsi gani vipo  vizingiti vya makaribisho. Lakini zaidi ya ule ubinafsi, na kwa yule anayejifungia katika utajiri wake, uchumi, sera za kisiasa ambazo hazitambui binadamu katika ukamilifu wake, kuna vizngiti ambavyo vipo vya kutoweza kutoa uwezekano wa hali halisi ya mahali pa kukaa , kazi na maisha ya hadhi.

Aidha Maaskofu wanabaisha kuwa wanao utambuzi wa kipeo amabcho kinaelendela kuimbumba nchi ya Italia na ambayo inasababisha pia ugumu wa kupokea kwasababu jirani anaonekana kama mshindani na siyo kama fursa ya upyaisho wa jamii na kiroho na katika kutoa nafasi ya ukuaji wa pamoja kwa manufaa ya nchi ya Italia. Kutokana na vigezo hivyo Maaskofu wa Italiwa wanasema shughuli  kubwa inayohitajika kwa sasa ini ile ya kuelimisha ambayo inatakiwa kuzingatia hali halisi na kisaidia kushinda hofu, hukumu, kutoaminiana, kwa  kuhamasisha pia kuwa na  dhimiri kamili, mazungumzo na ushirikiano!

Vilevile wakitazama watoto wageni, wanasisitiza juu ya kuwa na  umakini hasa kwa ongezeko la watoto ambao wanazaliwa  nchini Italia, na wale ambao wamefika na wazazi wao nchini Italia. Kutokana na dhana hii, ndipo maaskofu wanahamasisha maparokia yote hasa katika vituo vya mkusanyiko na malezi ya kiroho , ili kutumia nafasi hiyo kuelimisha dhamiri ya utambuzi wa dhamiri na hadhi ya wahamiaji kwa sababu ya kufikiria jinsi gani wageni hao wanalazimia kuacha ardhi yao na kujikuta wako nje ya mazingira yao, wengine bila kupenda , lakini kutokana na matatizo. Ni dharua katika jamii na hasa jumuiya ya kikristo kuwasaidia wahamiaji ili waweza kupokelewa na kusaidiwa  kiuchumi na  kijamii katika nyakati hizi!

Na Sr Angela Rwezaula 
Vaticsn News!








All the contents on this site are copyrighted ©.