2018-05-20 11:35:00

Roho Mtakatifu anatoa msukumo wa kwenda hadi miisho ya Dunia!


Kuja kwa Roho Mtakatifu siku ya Pentekoste katika Somo la kwanza, inafananishwa na upepo wa nguvu (Mdo 2,2). Sura hii inaeleza nini? Upepo wa nguvu unafanya ufikirie nguvu kubwa, lakini isiyo ishia hapo. Ni nguvu inayo badili hali halisi, kwa maana  upepo huleta mabadiliko, kama vile mkondo wa  baridi kukiwa na joto na mkondo wa joto kukiwa na baridi, mvua kukiwa na ukame (…. ) Hata Roho Mtakatifu kutoka ngazi ya juu inafanya kazi hiyo, maana ni nguvu ya Mungu inayobadili dunia. Utenzi wa Roho Mtakatifu umekumbusha kuwa  “Roho katika  kazi ni pumziko, katika machozi ni  burudiko”. Vile vile tunaomba: “Osha machafuko yetu, panyeshee pakavu petu na kuponya majeraha”. Yeye anaingia katika hali halisi na kubadili mioyo na matukio; kwa maana tunaomba “alegeze ukaidi, awashe moto wa uadili na kunyoosha  upotevu wote”.

Ni utungulizi wa Mahubiri ya Baba Takatifu Francisko wakati Mama Kanisa anaadhimisha Siku Kuu ya kuja kwa Roho Mtakatifu( Pentekoste), katika Misa Takatifu iliyo fanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Mjini Vatican tarehe 20 Mei 2018. Baba Matakatifu anaendelea na ufafanuzi  wa mabadailiko ya moyo kwamba: Yesu alikuwa amewambia mitume wake“ Mtapokea nguvu ya Roho Mtakatifu(….) na mtakuwa mashahidi ( Mdo 1,8). Na ilitokea hivyo kwa sabababu ya kuwaona  mitume wale, waliokuwa na hofu kwanza, wakifunga milango baada ya ufufuko wa Mwalimu, wanabadilishwa na Roho kama alivyokuwa amesema Yesu katika Injili ya siku na wanatoa ushuhuda ( Yh 15,27).Baba Mtakatifu anathibitisha, kutoka kwenye woga, wanakuwa wajasiri na wanaanza safari ya kutoka Yerusalemu hadi miisho ya dunia. Walikuwa na hofu wakiwa na Yesu kati yao na sasa ni watangazaji bila Yeye, kwasababu Roho amewabadili mioyo yao!

Roho amefungua mioyo yao iliyo kuwa imetiwa mhuri wa hofu na  anashinda ugumu, huo kwa yule anayefurahishwa na vipimo vya matinki za zawadi tu. Roho inapanua mioyo finyu, Roho inasukuma kwenda kutoa  huduma na hata yule anayependa  kukaa katika hali nzuri anaondoka kwenda kuhudumia. Aidha Roho inamfanya atembee yule anayejiamini amefika, Roho inamfanya  aote ndoto yule mwenye kujazwa na ubaridi. Hayo ndiyo mabadiliko ya mioyo Baba Mtakatifu anathibitisha!  Ni watu wengi wanatoa ahadi katika kipindi cha mabadiliko,katika  mwanzo mpya na upyaisho,  lakini uzoefu unafundisha kuwa, hakuna juhudi binafsi katika ardhi  hii zinaweza kubadili mambo na kutosheka kikamilifu katika moyo wa binadamu. Hiyo ni kwasababu mabadiliko ya Roho ni tofauti, kwa maana siyo ya mapinduzi ya maisha yanayo tuzunguka, badala yake  yanabadili mioyo yetu kwa ndani ; pamoja na hayo, Roho haituondolei mara moja matatizo yetu tuliyo nayo,bali inatoa uhuru wa ndani ya  moyo, ili kukubaliana na matatizo hayo; na hatupewi yote kwa haraka, bali inatufanya tutembee kwa matumaini, bila kuchoka kamwe katika maisha!

Roho inatunza moyo ili kuendelea kuwa kijana. Baba Mtakatifu anafafanua kwamba, pamoja na jitihada za kutaka kuongeza maisha, yote hayo ni bure kwani yatakuwa na mwisho, badala yake Roho ndiye anakuja na kupyaisha mioyo ya ndani! Je anafanyaje? Anapyaisha mioyo na  kubadili kutoka katika maisha ya dhambi na kuwa na msamaha. Hayo ndiyo mabadiliko makubwa, yaani  kutoka katika dhambi na kuwa wenye haki na kubadilika kabisa kwa kuondokana na utumwa wa dhambi na kuwa huru; kutoka katika wana wa utumwa, kuwa wana wenye thamani; kutokata tamaa, kwa kuwa na matumaini. Hiyo ndiyo Roho Mtakatifu anafanya kazi ya kuzaa furaha na kuchanua amani ya moyo.

Leo hii tujifunze kitu ni gani cha kufanya tutakapo kuwa tunahitaji kubadilika kweli. Ni nani hasiye kuwa na dhambi? Baba Mtakatifu Francisko ameuliza; Zaidi tukiwa katika ardhi hii, mahali ambapo kuna shida nyingi za kuelemewa na uzito wa maisha, katika udhaifu unao tusumbua; tunaona ugumu wa kwenda mbele, hata kupenda kwa dhati inakuwa ngumu! Kwa maana hiyo, Baba Mtakatifu anasema, tunahitaji kula dawa za virutubisho kwa upya vyenye nguvu. Lakini nguvu hiyo ni Mungu tu. Ni Yeye tunaye kiri imani ya Nasadiki na anatoa maisha!  Baba Mtakatifu ameongeza: Ni jinsi gani ingekuwa vizuri kupata viritubisho vya nguvu hiyo kila siku ya maisha, yaani kutamka  kila unapoamka “Njoo Roho Mtakatifu, njoo katika moyo wangu, njoo katika siku yangu”!

Baada ya kubadili mioyo hubadili hata matukio: Baba Mtakatifu amesema, kama upepo uvumao na kupuliza kila mahali, ndivyo Yeye anafika hata katika hali iliyo nzito. Katika kitabu cha Matendo ya Mitume,kitabu ambacho Baba Mtakatifu anasema ni kitabu cha kugundua zaidi, mahali ambapo Roho yuko mstari wa mbele, kinaonesha mwendo kasi unao endelea lakini wenye utajiri na mshangao kwani,wakati mitume walikuwa wanasubiri, Roho aliwatuma kwenda kwa wapagani. Anafungua njia mpya kama inavyo onesha  katika tukio la shemasi Filipo. Roho inamsukuma aende katika njia ya jangwa, kutoka Yerusalemu hadi Gaza, katika eneo linalosikia linalia machozi ya uchungu! Roho Mtakatifu anabadili mioyo na matukio na kupeleka amani katika nchi Takatifu. Katika njia ile ambayo Filipo alihubiri kwa mfanyakazi wa Ethiopia na kumbatiza; Roho anampeleka  huko Azoto na Kaisari: daima katika hali mpya ili kuweza kutangaza  habari mpya ya Mungu. Vilevile yupo Paolo ambaye alilazimishwa na Roho ( Mdo 20,22) na kwenda hadi miisho ya dunia akipeleka Injili kwa watu ambao walikuwa bado hawajuhi. Iwapo kuna Roho daima kuna matokeo  ya jambo fulani mapya, Yeye anapopuliza hatulii kamwe!

Wakati maisha yetu katika Jumuiya yanapitia  kipindi kigumu, mahali ambao kuna tokea ukimya wa ndani dhidi ya upya wa Mungu ni ishara mbaya! Ina maana ya kutafuta mahali pa kujiegemeza badala ya upepo wa Roho. Unapoishi kwa kujitosheleza na  huwezi kwenda kuwafikia walio mbali, ni ishara mbaya! Baba Mtakatifu anasisistiza, ni Roho anapuliza, lakini sisi tunapenda kuegemea Tanga, japokuwa, wakati mwingine tumefanya uzoefu wa kuona mambo makuu ya Mungu. Hasa katika kipindi kigumu cha giza, Roho huyo huingilia  kati na kutoa utakatifu angavu!  Yeye ni moyo wa Kanisa na daima uongeza chachu hai ya matumaini, hutoa furaha na matunda mapya, hutoa vichipukizi vya maisha. Kama vile katika familia anazaliwa mtoto, Baba Mtakatifu anathibitisha kuwa, mtoto huyo hubadili utaratibu wa muda, unapoteza usingizi, lakini ukiwa na furaha ambayo inapyaisha maisha na kutoa msukumo wa  kuendelea mbele, kwa kupanua upendo huo. Ndiyo kazi ya Roho inayotoa radha ya utoto katika Kanisa. kwa maana shughuli uendelea kuzaliwa kwa upya .

Roho inaimarisha upendo tangu mwanzo. Roho Mtakatifu anakumbusha Kanisa ya kuwa katika  karne za kihistoria, kijana wa maka 20, yupo mchumba ambaye Bwana alimpenda upeo. Kwa maana anahimiza kutochoka kabisa kukaribisha  Roho katika mazingira yetu na kuomba daima kabla ya kuanza shughuli za siku kwamba  “ Uje Roho Mtakatifu”!  Yeye anatoa nguvu za mabadiliko, nguvu moja ambayo ni kusema, ndiyo kiini na kitovu. Ni kitovu kwasababu kinasukuma katikati,na kufanya kazi kuanzia ndani ya kina cha moyo! Roho  inaleta umoja katika migawanyiko, amani katika mivutano na  nguvu katika vishawishi! Mtakatifu Paulo anakumbusha katika Somo la Pili kwamba matunda ya Roho Mtakatifu ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole na kiasi (Gal 5,22).

Roho anatoa upendo Mkuu na Mungu, nguvu ya kina ili kuweza  kwenda mbele, wakati huo huo ni nguvu ya kiini inayo toa msukumo kutoka ndani kwenda nje. Yule anayepeleka ndani ya moyo, ndiye yule  anaye wasukuma kwenda pembezoni, katika kila kona ya maisha ya binadamu; Yule anaye tuonesha Mungu anatusukuma kuelekea kwa ndugu, anatuma na kufanya mashahidi na kwa njia hiyo , Mtakatifu Paulo anasisitiza juu ya matunda ya Roho Mtakatifu kuwa ni upendo, utu wema, ukarimu na upole na Roho Mtakatifu ni mfariji anayetia moyo kuwaelekea kwa wengine. Anayeishi kwa Roho katika tasaufi hii anajikuta kuwa na msukumo wa kwenda na wengine kwa Mungu na katika dunia!

Baba Mtakatifu amehitimisha akiomba ili wote tuweze kuwa namna hiyo.  Roho Mtakatifu, upepo wa nguvu wa Mungu,unao puliza juu yetu, upulize katika mioyo yetu na kutufanya tupumue huruma ya Baba. Upulize juu ya Kanisa na kutusukuma kwenda  hadi miisho ya dunia, kwasababu ni wewe unaye peleka na huwezi kupeleka kitu tofauti na wewe! Upulize juu ya dunia upepo mwanana wa amani na ubaridi mwanana  wa kutuliza na matumaini. Njoo Roho Mtakatifu  na utubadili ndani, na kupyaisha dunia!  Amen 

Ba Sr Angela Rwezaula 
Vatican News








All the contents on this site are copyrighted ©.