2018-05-19 18:00:00

Siku ya Kimisionari Duniani:Pamoja na vijana tupeleke Injili kwa wote!


Katika ujumbe wake, Baba Mtakatifu Francisko wa Siku ya Umisionari Duniani mwaka 2018 kwa namna ya pekee  anasisitizia juu ya umuhimu wa utume wa Kristo alio waachia mitume wake kwa maana ya waamini wote, kwa namna ya pekee kabisa amewatazama vijana kwa karibu ambapo anawakumbusha kwamba, wao ni matumaini ya utume wa Kanisa na kwamba, Mashirika ya Kipapa ya Kazi za Kimisionari  yamesaidia mchakato wa uinjilishaji hadi miisho ya dunia. Hayo yote yamesisitizwa katika vipengele:pamoja na vijana tupeleke Injili kwa wote; Maisha ni utume; tunawatangazia Yesu Kristo; tutangaze habari hadi miisho ya dunia na kushuhudia upendo.

Pamoja na vijana, tupeleke Injili kwa wote 
Akifafanua juu ya pamoja na vijana kupeleka Injili kwa wote; Baba Mtakatifu ametaka kufanya tafakari juu ya utume wa kimisionari ulio kabidhiwa na Yesu. Kwa kuwalenga vijana,lakini  piani kwa wakaristo wote ambao wanaishi katika Kanisa wakijikita ndani ya maisha yao kutunza wana wa Mungu. Kile ambacho kinatoa msukumo wa kuongea kwa wote, na kuzumza na vijana ni uhakika imani ya kikristo ambao unabaki daima kuwa kijana na kufungua utume wa Kristo anao ukabidhi, kama vile maneno ya Mtakatifu Yohane Paulo II aliyekuwa anapenda sana vijana na ambaye alijionesha kwa matendo ya dhati kwa ajili yao. Katika Waraka wa kitume  (Redemptoris missio, 2), anasema, “utume unaimarisha imani. Fursa ya Sinodi itakayo adhimishwa Roma mwezi Oktoba, mwezi wa kimisonari, inatoa fursa ya kutambua vema kwa mwanga wa imani ya kwamba Bwana Yesu anataka kusema na vijana kwa njia yao  na katika jumuiya ya kikristo.

Maisha ni utume:
Baba Mtakatifu katika kipengele cha maisha ni utume anajikita kufafanua kuwa, kila mme na  mwanamke ni utume na ndiyo sababu ya kujikuta wanaishi katika ardhi. Tendo la kupendezwa ili kuweza kutumwa  ni hatua mbili za mwendo zilizomo ndani ya moyo na zaidi hasa ukiwa kijana mdogo unahisi nguvu za upendo wa kina ambazo zinatoa ahadi ya wakati ujao na kukusukuma uende mbele katika maisha. Hakuna hata kijan mmoja anayehisi kukatisha maisha au kutopendezewa. Baba Mtakatifu anaongeza, kuishi kwa furaha na uwajibikaji binafsi kwa ajili ya dunia ni changamoto kubwa! Kadhalika anathibitisha, kuwa anao utambuzi wa mwanga na kivuli cha kuwa vijana, hasa anapofikiria ujana wake na familia yake. Anakumbuka vema matumaini ya kina kwa ajili ya wakati endelevu. Aidha amesisitiza, tenedo la kujikuta katika dunia hii siyo kwa maamuzi yetu, kinyume chake ni kutambua kuwa yupo aliye anza na ambaye yuko mbele  yetu na anatufanya tuishi. Kila mmoja anaalikwa kutafakari juu ya hali halisi hii yanni  Mimi ni mtume katika ardhi hii na ndiyo maana anajikuta katika dunia,(Taz Wosia, Evangelii gaudium, 273).

Tunawatangazia Yesu Kristo:

Kwa kufafanua kipengele, “Tunawatangazia Yesu Kristo, Baba Mtakatifu anasema, Kanisa linatangaza bure kile ambacho kimepokea bure (taz Mt 10,8; At 3,6), Kanisa linaweza kushirikishana na vijana wote ile njia na ukweli ambayo inaleta maana ya kuishi katika ardhi hii. Yesu Kristo, aliyekufa na kukufuka kwa ajili yetu, anatoa uhuru wetu, ambao unakutafakarisha na ili ujikite katika  kutafuta, kugundua na kutangaza maana ya kweli na utimilifu huo.
Kutokana na kutafuta huko, Baba Mtakatifu anasisitiza kwa vijana wasiwe na hofu ya Kristo na katika Kanisa lake! Ndani yake ndimo ipo tunu inayojaza furaha ya maisha. Anathibitisha hayo kutokana na kutokana na uzoefu wake ya kwamba, kwa neema ya imani ameweza kupata msingi wa ndoto zake na kwa nguvu ya kuweza kuzitimiliza. 

Ameona sura za mateso mengi na umaskini unaobadilisha sura nyingi za ndugu kaka na dada. Lakini pamoja na hayo yote, yule anayekaa na Yesu, ubaya ndiyo chachu ya kumfanya apende zaidi na zaidi. Watu wengi wanaume na wanawake, vijana wengi wameonesha kutoa maisha yao kwa ukarimu, hata kufikia kifodini kwa ajili ya upendo wa Injili katika huduma ya ndugu. Katika msalaba, Baba Mtakatifu anaongeza kusema, tunajifunza mantiki ya Mungu ya kujitoa kwake kwa ajili yetu sisi (taz Kor 1,17-25) kama isemavyo Injili kwa ni kwa ajili ya maisha ya dunia (taz Yh3,16). Kuwashwa upendo wa Kristo na kutekeketezwa kwa yule anayewaka ili  akue , ang’ae kumwangaza yule anayependa (ta 2 Kor 5,14). Katika shule ya watakatifu inatufungua katika upendo mkubwa wa Mungu, na kwa njia hiyo Baba Mtakatifu amewaalika wajiuliza kila wakati: je Kristo angefanya nini katika nafasi yangu?

Kueneza imani hadi miisho ya dunia:
Baba Mtakatifu anasema, hata vijana kwa njia ya Ubatizo wamekuwa washiriki hai wa Kanisa na kwa pamoja kuna utume wa kupeleka Injili kwa wote. Wao ni vichipukizi vya maisha. Kukua katika neema ya ya imani ambayo imetokana na Sakramenti ya Kanisa ambavyo inajikita katika kizazi ili kushuhudia, mahali ambapo kuna hekima uzoefu unageuka kuwa ushuhuda na kuwatia moyo wale ambao wanafungua wakati endelevu. Mambo kama hayo ya vijana hugeuka kwa mara nyingine tena kuwa msaada na matumaini kwa wale ambao wamefikia ukaribu wa kuhitimisha hatua zao za mwisho. Baba Mtakatifu halikadhalika amesifi tofauti za karama mbalimbali za maisha  kwa maana anaongeza kuwa, utume wa Kanisa unajenga daraja kati ya kizazi, ambapo imani katika Mungu na upendo kwa ajili ya jirani uundwa na dhana za umoja wa kina.

Kueneza imani kwa namna hii moyo wa utume wa Kanisa ni  kwa njia ya kuambukiza upendo, mahali ambapo kuna furaha na mwamko wa kuelezea upatikanaji wa maana kamili ya  maisha. Ili kuweza kusambaza imani na kuvutia inahitaji mioyo uliyo wazi, na upana katika upendo. Siyo rahisi kuweka kizingiti katika upendo kwa maana “Pendo lina nguvu kama kifo” (taz Wim 8,6). Na upando huo unazaa makutano, ushuhuda, kutangaza; unazaa kushirikishana katika upendo kwa wote ambao wako mbali na imani, wanaojionesha tofauti na wakati mwingine wako kinyume na wagomvi. Katika mazingira ya binadamu m utumaduni na dini bado kunahitajika Injili ya Yesu, uwepo wa Sakramenti ya Kanisa inyowakilishwa katika sehemu za pembezoni, katika “miisho yote ya dunia”. Ni tangu wakati wa Pasaka ya Yesu mitume wamisionari walitumwa  kwa hakika ya kuwa na Bwana daima   (taz Mt 28,20; Mdo 1,8). Baba Mtakatifu anabainsha kwamba tendo hilo ndilo liitwalo Missio ad gentes.

Pembezoni zaidi ambayo imeachwa na binadamu anaye hitaji Kristo ni katika utofauti wa kukosa imani au hadi  kufikia hatua ya kuwa na chuki dhidi  ya ujazo wa maisha ya Mungu. Kwa maana hiyo Baba Mtakatifu anathibitisha, kila umaskini wa mwili  na kiroho, kila uhalifu wa ndugu na kaka, daima ni matokeo ya kukataa Mungu na upendo wake. Miisho ya dunia Baba Mtakatifu anasema leo hii kwa ajili yao vijana ni mahusiano, ambayo daima ni rahsi kuingiliwa. Katika kufafanua anasema, ni katika dunia ya kidigitali, mitandao ya kijamii ambayo imesambaratika na kukatisha kila kona, wakati huo huo inazidi kufuta mipaka na umbali na kupunguza utofauti.  Hatua hiyo utafikiri kila kitu kimo mikononi, kila kitu ni kazi na kwa haraka. Pamoja na hayo Baba Mtakatifu anathibitisha, bila kuwa na zawadi inayojikita ndani ya maisha yetu, inawezakana kabiasa ukawa na mamilioni ya watu wa kuwasiliana nao, wakati huo huo huna hata mmoja uliyeungana naye katika maisha. Kwa njia hiyo, utume wa kufikia miisho ya dunia unahitaji zawadi binafsi katika wito tuliyo pewa na Yule aliyetutangulia katika ardhi hii. ( Lc 9,23-25). Baba Mtakatifu amesema, kuwa vijana wanataka kumfuata Kristo, lakini cha muhimu ni kumtafuta na kukubali wito wao binafsi.

Kushuhudia upendo
Hatimaye katika kipengele cha mwisho kuhusu kushuhudia Kristo, Baba Mtakatifu Francisko anawashuru hali halisi zote za Kanisa ambazo zinawezesha kukutana na Kristo binafsi aliye hai katika Kanisa lake, akiwa na maana katika mazingiri ya Parokia, vyama vya kitume, mashirika ya kitume, jumuiya za kidini na sehemu mbalimbali za huduma ya kimisionari. Vijana wengi wanakutana katika kujitolea kimisionari, katika mitindo ya kuhudumia walio wadogo. ( taz Mt 25,40) kuhamasisha hadhi ya binadamu,na kushuhudia furaha ya kupenda na kuwa mkristo. Katika uzoefu huo wa Kanisa unafanya kila mmoja kujifunza na siyo tu katika maandalizi ya kufanikiwa kitaaluma, bali katika mandeleo na kutunza zawadi ya Bwana ili iwe bora katika kuhudumia wengine. Mitindo hii Baba Mtakatifu amesema ni ya kupongeza ya huduma ya kimisionari ya sasa ambayo ni mwanzo wa matunda na mang’mauzi ya miito ambayo inaweza kuwasaidia kutoa uamuzi wa zawadi ya kujitoa binafsi kama wamisionari.

Katika mioyo ya vijana ndipo yalizaliwa Mashirika ya Kipapa ya Kazi za Kimisionari  ambayo yamesaidia mchakato wa uinjilishaji hadi miisho ya dunia kwa kuchangia ukuaji wa binadamu na utamaduni wa watu wengi wenye kiu ya Ukweli.  Maombi na msaada wa zana ambazo kwa ukarimu zinatolewa na kugawanywa kwa njia Shirika la  POM, linasaidia Vatican  kuwaelekea wale ambao wanajikuta kwenye  matatizo, na wameweza kwa namna moja kuwa na uwezo wa kushuhudia katika mazingira yao. Hakuna yoyote aliye maskini wa kuweza kukosa chochote cha kutoa kwa maana hawali ya yote yeye mwenyewe ni zawadi. Baba Mtakatifu amerudia kuhimiza juu ya Wosia wake alioutoa kwa vijana nchini Cile ya kwamba: wasifikiri kamwe kuwa hawana chochote cha kuweza kutoa, na kwamba   huna haja ya mtu yoyote kwa maana ni watu wengi wanakuhitaji wewe, hivyo lazima kutafakari jambo hilo. Kila kijana afikirie katika moyo binafsi ya kuwa “wapo watu wengi wananihitaji”! (Mkutano wa vijana katika madhabahu ya Maipu 17 Januari 2018.

Baba Mtakatifu amehitimisha akiwakumbusha mwezi Oktoba wa kimisonari ujazo , mahali ambapo Sinodi itafanyika na inayowahusu, anathibitisha kwamba, itakuwa ni fursa kubwa kwa ajili ya kutufanya  tuwe mitume wa kimisionari wenye  shauku kwa ajili ya Yesu na utume wake, hadi miisho ya dunia. Maria Malkia wa Mitume, watakatifu Francisko wa Xavier  na Mtakatifu Teresa wa Mtoto Yesu, Mwenye heri Paulo Manna watuombee na kutusindikiza daima.
Sr Angela Rwezaula 
Vatican News

 








All the contents on this site are copyrighted ©.