2018-05-16 16:16:00

Ujumbe wa Kard. Tauran kwa wawakilishi wa mkutano wa dini za kidharma!


Baraza la Kipapa la Mazungumzo ya kidini kwa ushirikiano na ofisi ya kitaifa ya Uekumene na mazungumzo ya kidini ya Baraza la Maaskofu Italia, Umoja wa wabudha Italia, umoja wa wahindu Italia, Chama cha Sikh Sewa na Taasisi ya Jainology, wameandaa Mkutano wanye mada kuu DHARMA na LOGOs. Mazungumzo na ushirikiano katika nyakati ngumu. Mkutano ulio fanyika katika ukumbi wa Mikutano wa  Baraza la Maaskofu Italia, ambapo  wabudha, wakristo , Wahindu, Wajainist  na Sikh wameudhuria mkutano huo wenye mada msingi  na hai katika nyakati zetu.

“Kuanzishwa kwa mazungumo kati ya wabubudha , wahindu, jainist na sikh ni kutaka kushinda zile hukumu na kujifungua binafsi ambayo mchakato na sehemu ya utamaduni wa ugonvi, ili kuelekea katika hatua za utamaduni wa makutano”.  Ndiyo maombi ya Kardinali Jean-Louis Tauran Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la mazungumzo ya Kidini katika ujumbe wake kwa washiriki wa mkutano huo. Ujumbe wa Kardinali ulio somwa wakati wa ufunguzi tarehe 15 Mei 2018 na katibu   mkuu wa Baraza hilo Askofu Miguel Ángel Ayuso Guixot.

Katika mkatano huo, wamewaalika hasa maprofesa wenye walio na asili ya kimonaki katika tamaduni mbalimbali, hasa asili ya India na wote wanao jikita katika mazungumzo binafsi na wataalam katika ulimwangu wa kikristo na katoliki. Kardinali Tauran katika ujumbe wake, akisifu uthabiti na mshikamano wa kidini, ametoa wito wa kuwa na tabia ya kujifungua wazi na upendo kwa namna ya kuweza kushinda vingiti vya kuhukumiana na kuwa wazi, kujifunza na kuwa na uwelewa zaidi ambao ni utajiri wa urithi kila binadamu, na kufanya kazi kwa ajili ya umoja wa familia ya binadamu.

Aidha Kardinali  Tauran anaonesha kwa namna ya pekee umuhimu wa kuendeleza kuhamasisha  utamaduni wa makutano kati ya wanafunzi, kwa mujibu wa ushauri na wito wa Papa Francisko kuhusu suala hili nyeti. Katika utambuzi ya kuwa yapo mabadiliko makubwa kati ya enzi za zamani na sasa katika shule kwa maana ametoa mifano iliyokuwa ya kizamani ya kujifungia ndani ya chuo kikuu na kwamba haiku ana matatizo, lakini kwa sasa ni kinyme kwani ni suala ambalo linahitaji mabadiliko ya kweli. Ni changamoto, hivyo wanao uwajibu mkubwa wa kuhamasisha kwa  wanafunzi wao bila kutafuta hukumu za kila imani ya dhehebu au matendo ya kiutamaduni, badala badala yake ni kukuza heshima ya kila mmoja, kwa maana hiyo ni kusema kutazama zaidi ya kile kinachounganisha kuliko kile kinachotengenisha. Kukuza heshima na amani ndiyo  thamani kubwa katika  kuelekea kwa wale ambao wako  tofauti au ni wageni na ambao mara nyingi wamefikiriwa tofauti na kuwa vizingiti matokeo yakwa ni kubaguliwa.

Zaidi Kardinali Tauran katika ujumbe wake anasisitiza juu ya dunia hii, ambayo vurugu na vita vinakatisha ndani yake, wakati huo huo watu wangi wanasubiri waone  wahusika wa dini zote ndiyo wanakuwa  mstari wa mbele na thabiti katika mazungumzo na kuchukua nafasi ya kuwa mawakili hai , katika kujikita kutafuta amani na umoja kwa kila mtu  ili aweze kuhisi kukumbatiwa kama binadamu, kwa namna ya pekee wale maskini na waathirika. Mwisho anahitimisha akiwaomba wafanye uzoefu hai  katika kukuza dhamiri ya uwelewa kati ya watu ili wajenge jamii iliyo bora ya kibinadamu , haki na bila ubaguzi.

Sr Angela Rwezaula
Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.