Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baba Mtakatifu Francisko \ Hotuba

Papa amekutana na wawakilishi wa dini za Kidharma na wakristo!

Papa amekutana na wawakilishi wa dini ya Dharma yaani:Wahindu, wabudha,jainists na Sikh pia na Wakristo - RV

16/05/2018 15:53

Tarehe 16 Mei 2018, Baba Mtakatifu Francisko amekutana na wawakilishi wa mkutano kutoka katika madhehubu ya wakristo, Wahindu, wabudha, jainists na Sikh. Wakati wa hotuba yake ameonesha furaha yake ya kukutana nao wakiwa katika fursa ya mkutano  wa mada ya “Dharma na Neno. mazungumzo na ushirikiano katika enzi ngumu”. Mkutano huo umefanyika mjini Roma 15 Mei 2017. Pamoja na hayo shukrani kwa wote ambao wameweza kuanzisha jambo hili linalo waunganisha madhehebu ya dini ya wakristo, Wahindu, wabudha, jainists na Sikh. 

Akendelea na hotuba yake amaesema, mazungumzo na ushirikiano ni ufunguo wa maneno katika nyakati zetu ambazo ni ngumu katika mantiki, kwa maana enzi hizi zinaona mivutano na migogoro, pamoja na vurugu , ziwe ndogo au kubwa katika ngazi iliyo ndefu na kubwa. Zaidi ndiyo sababu ya kumshukuru Mungu iwapo viongozi wa dini wanajikita  mstari wa mbele katika shughuli ya kujikita katika kuhamasisha utamaduni wa makutano na kutoa mfano wa mazungumzo na ushirikiano uli wazi ambao ni huduma ya maisha, hadhi ya binadamu na utunzaji wa mazingira.

Amerudia kuwashukuru kwa yote wanayo tenda  na kwa pamoja kushirikiana kwa mujibu wa utamaduni wa dini ili kuweza kuhamasisha wema katika dunia hii. Amewabariki wote na familia zao.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!

16/05/2018 15:53