2018-05-16 15:40:00

Papa amekutana mjini Vatican na wawakilishi wa Wabudha kutoka Thailand


Baba Mtakatifu Francisko, Jumatano 16 Mei 2018, amekutana na wawakilishi wa Wabudha kutoka Thailand, mjini Vatican ambapo wakati wa hotuba yake ameshukuru zawadi ya Kitabu chao Kitakatifu katika Lugha ya kisasa ya wamonaki wa Ekalu la Wat Pho. Baba Mtakatifu anasema, hiyo ni ishala njema ya ukarimu wao na urafiki ambao unawaunganisha kwa miaka mingi katika hatua ndogo ndogo za safari yao. 

Anakumbuka kwa namna ya pekee mkutano mmoja mjini Vatican kati ya Mwenye heri Papa Paulo VI na hayati Somdej Phra Wanaratana, ambapo kwa heshima, ipo sanamu yake katika  mlango wa makaribisho wa Baraza la Kipapa la Mazungumzo ya Kidini, mahali ambapo wao kwa siku hizi za mkutano wamepata fursa ya kutembelea Baraza hilo.

Baba Mtakatifu anarudia kwa upya kuwataka wabudha na wakatoliki waendeleze uhusiano wao kwa kina  na kujiendeleza katika ufahamu wa pamoja hasa katika kutakiana mema na heshima katika tamaduni za tasaufi; Katika ulimwengu wawe  mashahidi wa thamani ya haki, amani na utetezi wa hadhi ya binadamu. Na mwisho wamewashukuru na kusifu mkutano huo na kumalizia kwa baraka ya Mungu kwa furaha na utulivu.  

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!          








All the contents on this site are copyrighted ©.