2018-05-16 15:16:00

Katika Katekesi Papa amehitimisha Liturujia ya Sakramenti ya Ubatizo!


“Ndugu wapendwa habari za asubuhi. Leo hii tunamalizia mzunguko wa Katekesi ya Ubatatizo. Matokeo ya kiroho katika sakramenti hii inayo onekana kwa macho, lakini kwa kufanya  kazi ndani ya moyo wa yule ambaye amekuwa kiumbe mpya inatokana na tendo lile la kupokea nguo nyeupe na mshumaa unaowaka”. Ni utangulizi wa tafakari ya Katekesi ya Papa Francisko, Jumatano 16 Mei 2018, katika viwanja vya Mtakatifu Petro kwa mahujaji na waumini wote waliofika kusikiliza katekesi hii. Akiendelea kufafanua juu ya hatua ya mwisho wa liturujia ya sakaramenti ya Ubatizo, Baba Mtakatifu anathibitisha kwamba, baada ya kuvalishwa utu mpya ambao umeumbwa kwa mfano wa Mungu na ambao hujionesha katika maisha ya kweli ya uadilifu na utakatifu  (taz Ef 4,24).

Imejitokeza asili ambayo ilikuwa tangu hawali ya  wabatizwa wapya kuvaa nguo mpya, inayong’aa na kufanana na mwangaza wa maisha aliyo fanya Kristo na katika Roho Mtakatifu. Pamoja na nguo nyeupe kuwa ishala ya kuangaza kile kilichotokea katika sakaramenti, pia inatangza hali halisi ya kubadilishwa katika utukufu wa Mungu. Je ina maana gani kuvaa Kristo? Ili kutambua hili ni mtakatifu Mtakatifu Paulo anatukumbusha fadhila zipi ambazokila  mbatizwa anapaswa kuzipalilia akisema  “Basi, kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu, mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi. Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu. (wakol 3,12-14).

Hata kukabidhiwa mwanga wa mshumaa wa Pasaka, unaonesha matokeo hayo ya ubatizo  ambapo Padre anasema, “ Pokeeni mwanga wa Kristo”.  Maneno hayo yanakumbusha kuwa sisi  siyo mwanga bali ni Yesu Kristo aliye mwanga,( Yh 1,9;12,46), ambaye alikufufuka katika wafu na kushinda giza la ubaya. Sisi tunaalikuwa kupokea mwanga wake!  Kama mwanga wa mshumaa wa Pasaka utoavyo mwanga katika mishumaa yote midogo, ndivyo  upendo wa Bwana mfufuka unawasha mioyo ya wabatizwa wote  na kuwajalia mwanga na nguvu. Tangu zamani, Baba Mtakatifu anathibitisha, sakramenti ya Ubatizo ilikuwa inajulikana kama mwangaza, na wabitizwa wapya walikuwa waliitwa waangazwa. Hiyo kwa dhati ndiyo wito wa kikristo kutembea daima kama watoto wa nuru na kuyashika yote katika imani.  “Maadamu mnayo nuru, iamini nuru hiyo, ili mpate kuwa wana wa nuru. Gv 12,36).
 
Katika shughuli ya ubatizo ikiwa ni watoto, kazi kubwa ni ya wazazi pamoja na wasimamizi, ili waweze kuendeleza mwanga wa neema ya ubatizo kwa ajili ya watoto na kuwasaidia kushikilia imani hiyoMafundisho ya kiristo ni haki ya watoto; kwa maana yana ongoza hatua kwa hatua kujua ishala za Mungu katika Kristo;  kwa maana hiyo yanachimba mzizi kwa kina katika imani waliyoipokea katika ubatizo. Uwepo hai wa Kristo unatoa ulinzi, unatetea na kujipanua ndani mwetu; ni mshumaa ambao unaangaza hatua zetu, mwanga unao elekeza mang’amuzi yetu na kuwasha mioyo ili kwenda kukutana na Bwana na kutufanya tuwe na uwezo wa kusadia wale ambao wako njia moja na sisi, hadi kufikia  muungano usio tengenishwa na Yeye. Siku ile, katika kitabu cha ufunuo kinasema: “Wala hapatakuwa na usiku tena; wala hawana haja ya taa wala ya nuru ya jua; kwa kuwa Bwana Mungu huwatia nuru, nao watatawala hata milele na milele” (taz 22,5).

Katika kuadhimisha sakramenti ya Ubatizo inahitimishwa na sala ya Baba Yetu, ambayo ni sala ya jumuiya nzima ya wana wa Mungu. Kwa hakika wana waliozaliwa katika ubatizo wanapokea kwa ukamifu zawadi ya Roho Mtakatofu katika kipamara na kushiriki Ekaristi, wakijifunza nini maana ya kumwelekea Mungu na kumwita Baba katika Kanisa Takatifu. Baba Mtakatifu amehitimisha akisema kuwa, katika hitimisho la Katekesi juu ya luiturujia ya sakaramenti ya Ubatizo , anarudia kutoa mwaliko  kwa kila mmoja kusoma na kutafakari vema wosia wake wa kitume wa hivi karibuni, Gaudete et exultate (n. 15).  Furahini na shanglieni kwa maana  neema ya ubatizo ipate kutoa matunda katika hatua za utakatifu. Mwachie kila kit una kumufulia Mungu hadi mwisho na mchague Yeye, hurudi kwa  upya kuchagua Mungu! Usikate tamaa kwa sababu nguvu ya Roho Mtakatifu iweze kufanya kazi na utakatifu,  kwa maana tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,  upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria ( taz Gal 5,22-23) .

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.