Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baba Mtakatifu Francisko \ Mahubiri

Paulo anashuhudia utii kwa njia ya Roho na upendo kwa zizi lake!

Tuwaombee kwa Mungu maaskofu wapate neema ya kuaga vema inapofikia wakati wao kwa mfano wa Mtakatifu paulo mtume

15/05/2018 16:04

Neno la Mungu kutoka katika Kitabu cha  Matendo ya mitume , limeongoza mahubiri ya Baba Mtakatifu siku ya Jumanne 15 Mei 2018 wakati wa ibada ya Misa Takatifu kwenye Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican. Mtume Paulo anashuhudia utii kwa Roho Mtakatifu na Upendo kwa zizi lake wakati wa kuaga wazee wa Kanisa tayari kueleke huko Yerusalemukwa mujibu wa wito wa Roho Mtakatifu. Kutokana na hilo Baba Mtakatifu amewaomba waamini wote kusali kwa ajili ya maaskofu wote ili kwa mfano wa Mtakatifu Paulo wanaweza kujifunza kuaga zizi lao kwa njia hiyo!

Akiendelea na mahubiri anasema, hiyo ni sehemu yenye wito wa nguvu ambao kweli unafikia  hatua ya kutafakari kwa  kina ndani ya moyo japokuwa ni wazi kwamba  ni hatua inayotufanya wote kutazama kila hatua ya askofu yoyote  yule wakati wa kuaga. Somo la siku, kutoka katika kutabu cha Matendo ya mitume linasimulia jinsi gani  toka Mileto Mtakatifu Paulo aliwaita wazee wa Kanisa lakini, wakati wa hotuba yake alianza kuwaonesha kila hatua aliyopitia katika jumuiya yao wakati wa utume huo na kwa  kwa upande mwingine,  Baba Mtakatifu Francisko anabainisha kuwa, unaweza kufikiri Paulo anajisifu, lakini ndiyo mantiki msingi inayo mfana kuanzia hapo  hadi kufikia lengo kamili la kuwaaga! 

Paulo pamoja na sifa hiyo, anajisifia katika mambo mawili: kwanza ya dhambi zake;  pili juu ya  msalaba wa Kristo ambao ulimwokoa. Akelezea juu ya hisia ya kwenda Yerusalemu Paulo anataka kuwa ni kwa njia ya Roho. Papa anafafanua kuwa huo ndiyo  uzoefu wa kiaskofu, kwa maana askofu anajua kung’amua Roho, anatambua kung’amua Roho wa Mungu anapoongea na anatambua namna ya kujizuia dhidi ya roho wa dunia. Paulo kwa namna nyingine anaelekea katika mateso yaani kuelekea katika msalaba, maana anasema mwenyewe kuwa hajuhi anakuoelekea isipokuwa Roho Mtakatifu mji kwa mji humshuhudia akisema, ya kwamba vifungo na dhiki vyamngoja!

Je ni kwa maana ya kukumbusha jinsi gani Yesu aliingia Yerusalemu? Baba Mtakatifu anajibu Hapana! Kwa maana Yesu aliingia kwa ajili ya  ateswe, lakini Paulo anaelekea katika mateso. Mtume Paulo anajitoa kwa Bwana na kutii, ndiyo utashi wa Roho. Askofu anayekwenda mbele daima kwa mujibu wa Roho Mtakatifu ndiye Paulo Baba Mtakatifu anathibitisha!

Mwisho Mtume anawaaga kati ya huzuni waliokuwapo na kuwachia ushauri ambao siyo wosia wa malimwengu yaani mambo yasiyo kuwa na idadi kwa maana ya wosia wa kidunia; badala yake wosia wake ni ule upendo mkuu ambao ni Yesu Kristo. Na wosia wa pili ni ule wa zizi.  Hasa wa kuwa wangalizi wa zizi lote na wao wenyewe. Wakeshe juu ya zizi ; wao ni maaskofu kwa ajili ya zizi ili kulinda zizi na siyo kwa ajili ya kupanda juu yake kama vile ni kazi ya kuajiliwa hapana 

Paulo anamkabidhi Mungu makuhani kwa uhakika kuwa atawalinda na kuwasaidia, wakati huo huo akiendelea:  Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe.
Baba Mtakatifu anaongeza Paulo hakuwa na kitu japkuwa neema yaMungu tu na ujasiri wa kitumea ambao ulionesha na Yesu Kriato na mwokozi ambaya alimjalia. Kwa maana wao wenyewe wanajua ya kuwa mikono yake  hiyo imetumika kwa mahitaji yake na ya wale waliokuwa pamoja naye .

Paulo anasewathibitishia ya kuwa” Najua mimi ya kuwa baada ya kuondoka kwangu mbwa-mwitu wakali wataingia kwenu, wasilihurumie kundi;  tena katika ninyi wenyewe watainuka watu wakisema mapotovu, wawavute hao wanafunzi wawaandamie wao”. Kwa hiyo kesheni, mkikumbuka ya kwamba miaka mitatu, usiku na mchana, sikuacha kumwonya kila mtu kwa machozi Aidha Mtakatifu Paulo anaendelea kusema kuwa, hakutamani fedha wala dhahabu, wala mavazi ya mtu. Na katika mambo yote nimewaonyesha ya kuwa, kwa kushika kazi hivi imewapasa kuwasaidia wanyonge, na kuyakumbuka maneno ya Bwana Yesu, jinsi alivyosema mwenyewe, Ni heri kutoa kuliko kupokea. Alipokwisha kunena haya akapiga magoti, akaomba pamoja nao wote. …
Baba Mtakatifu Francisko ameongeza kusema kuwa anaposoma sehemu hiyo anajiuliza ni askofu na anapaswa kuaga, hivyo anamwomba Bwana neema ya kuweza kuaga namna hiyo siku ikiwadia. Je nitaweza kuwa mshindi kama Paulo? Lakini kwakuwa Bwana ni mwema na mwingi wa huruma atawezesha hilo  na ndiyo hivyo hata  anapofikiria maaskofuu wengine, ili Bwana aweze kuwapa neema ya kuweza kuaga na roho kama hiyo, nguvu kama hyo na upendo wa Yesu katika matumaini ya  Roho Mtakatifu!

Sr Angela Rwezaula 

Vatican News!

 

15/05/2018 16:04