Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Vatican \ Hotuba

Ziara ya Kard. Sandri nchini Lebanon kuwatia moyo waamini wa nchi hiyo!

Siku ya mwisho ya ziara ya Kardinali Sandri nchini Lebanon alifanya maadhimisho katika kanisa la Mama Yetu wa Harissa

14/05/2018 16:30

Domenika tarehe 13 Mei 2018 , Kardinali Leonardi Sandri, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la mazungumzo ya kidini amefanya  ziara yake iliyo andaliwa na Ubalozi wa Lebanom na kukutana kwanza na na vijana wanne walioudhuria Mkutano wa maandalizi ya Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya vijana 19-23 Machi 2018. Vijana wawakilishi kutoka nchi ya mashariki walikuwa wanatoka katika Kanisa la Kigiriki –Melkiti, Siro Katoliki na mwislam mmoja ambaye hakuweza kukutana naKardinali kutokana na kuwa nje ya chi.

Ha hivyo vinana watatu mbele ya  Kardinali Sandri  wametoa shukrani zao binafsi na kumweleza kwa furaha kutokana na  fursa waliyoipata ya uzoefu wa kusikiliza Baba Mtakatifu na Kanisa kwa ujumla kwa njia ya vijana wawakilishi kutoka pande zote za dunia  wao binafsi wana matumaini ya kuwa mtindo huo, unaweza kutambuliwa na kufanyika katika Makanisa yote mahalia, kuanzia hata katika nchi za Mashariki wanakozaliwa. Wasemaji  wakuu wa vijana wengine katika sinodi ya maandalizi, wamemkabidhi pia Barua Kardinali Sandri ili amfikishie Papa.  Pamoja  hayo pia wameonesha shauku kubwa ya kumkaribisha nchini Lebanon kwa niaba ya sauti za wanzao wa nchi za Mashariki kama ilivyo katika dunia, hasa  katika maswali yaliyo tolewa katika mkutano wao. Aidha wameweza kumwonesha hali halisi ya mateso wanayo ishi kutokana na miaka ya mwisho ya vita na vurugu na matukio mengi sana ambayo yanatoa msukumo wa kuwa na wasi wasi  wa maisha endelevu katika nchi zao mahalia, kwa upande mwingine kuonesha hata  imani ya wali yao kama msingi wa zawadi ya kugeuza kurasa za giza ili kuishi ndani ya familia na jamii pamoja na hali halisi ya matukio yanayo ikumba dunia uliyo mezwa na malimwengu kuanzia katika nchi yao na nchi nyingine ambazo zina ustawi wa maendeleo japokuwa kuroho ni maskini!

Haidha vijana hao wametoa sifa kubwa ya uzoefu ambao wameufanya mjini Roma na wengine , ulio wawezesha kubaliana na mantiki nyingi japokuwa umewawezesha kugundua jinsi gani Asia ni bara kubwa ambao limejaa tamaduni nyingi na pia hata kugundua jinsi  gani ilivyo ngumu kutambua hata heshima ya wengine kwa mantiki ambazo kwa mfano kijana wa Vietnam au Ufilippin anaweza kutafsiri uzoefu wa mwenzake anayeishi karibu na nchi za Mashariki au nchi nyingine.

Hata hivyo baada ya mazungumzo na vijana hao Kardinari amefuatilia hata shughuli za Balozi wa kitume nchini huo  Monsinyo Santus na kumshukuru kwa fursa ya mkutano huo na kwamba ni kama mojawapo ya mageuzi ambayo lakini yanapawa kuanzisa katika mioyo ya kila mmoja na zaidi  kwa vijana ambao wanatakiwa wawe mashahidi na waaminifu ndani ya jamii yao, si tu kupinga badhi ya mambo mabaya kama rushwa ufisadi au namna ya ulimbikizaji mali, badala yake ni kujikita hawali ya yote wao kuwa mstari wa mbele ili kuweza kutoa jua angavu la nchi yao na Kanisa.

Baada ya mazungumzo na picha za Pamoja, Kardinali alikwenda katika Madhabahu ya Mama yetu wa Harissa, mahali ambapo aliadhimisha misa akiwa na Patriaki wa Kimaroniti na baadhi ya maaskofu , kwa liturujia Takatifu ya  kizamani ya kiantiokia, ya Misa baada ya Kupaa kwa Bwana, pia  fursa ya kubariki sanamu ya Maria wa Lujan, Msimamizi wa nchi ya Argentina. Mwanzo wa maadhimisho walisoma ujumbe wa kubariki sanamu hiyo ulio anindikwa na  msimamizi mkuu wa Madhabahu ya Lujan na ule wa waziri wa Mambo ya nchi za nje wa Argentina na Mke wa Rais wa nchi ya Argentina mwenye asili ya nchi ya nchi ya Lebanon.

 Mahubiri yaliyotolewa kwa lugha ya kiarabu na kifaransa na Kardnali Rai, wakati Kardinali Sandri alitoa salam, mara baada ya liturujia kwa lugha ya kiitalino, ambapo alitoa pia  salam kutoka kwa Baba Mtakatifu Francisko na kuwaomba waendelee kusali kwa nia ya mambi ya mwezi Mei kwa ajili ya amani na zaidi kujiandaa mioyo yao kwa ajili ya mkutano unaotarajiwa kufanyika na Mapatriaki wakatoliki na wakiothodox wa nchi za mashariki huko Bari ambao Baba Mtakatifu ataudhuria tarehe 7 Julai 2018 

Baada ya misa walianza maandamano na mama sanama ya Bikira Maria wa Lujan kupitia katika barabara ya Madhabahu ya Harissa mahali ambapo waliweka sanamu hiyo na Kardinali Sandiri alisimama katikati ya umati wa waamini akisalimia mahujaji wengi, wakionesha namna wazi ya ukatoliki yaani umoja wa Kanisa ambapo hata katika nchini ya Lebanon unajielezea chini ya ulinzi wa Maria. Sala na baraka kwa wote, watoto, wagonjwa vajana na familia katoliki na zisizo katoliki, haya wakiwemo wanawake kutoka Sri-Lanka, waethipia wakiwa wamevalia mavazi yao ya rangi mbalimbali za kitamaduni kwa ajili ya Mama Maria wa Harissa. Kwa hakika Bwana ni mwenye taifa kubwa la watu walio unganika kwa moyo wote na kusadiki kwa imani  ambao  kweli wanakabiliana na safari na majaribu na mateso, lakini zaidi ya yote ni mashahidi wa uso mwangavu wa Kristo mfufuka katika hali halisi ya lugha, kabila utamaduni na uhakika wa kuwa wote ni wana wa Baba Mmoja aliyeko mbinguni. Baada ya chakula cha Mchana Kardinali Sandri  ameanza safari ya kurudi mjini Roma.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!

14/05/2018 16:30