Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baba Mtakatifu Francisko \ Mahubiri

Siku ya Kupaa Bwana yakumbusha kuelekeza mioyo juu na mwanzo wa utume!

Kupaa kwa Bwana ni siku ya kutukumbusha kuelekeza mioyo na macho yetu mbinguni na pia mwanzo wa utume wa Kanisa - AFP

14/05/2018 15:59

Leo hi inchini Italia na kama ilivyo katika nchi nyingine wanaadhimisha Siku Kuu ya Kupaa kwa Bwana. Sikukuu hii inafunga mambo mawili, kwa upande mmoja inaalika kuelekeza mtazamo wetu mbinguni, mahali ambapo Yesu mtukufu anakaa kulia kwa Mungu (taz Mk 16,19). Kwa upanda mwingine, ni kutukumbusha mwanzo wa utume wa Kanisa. Je ni kwanini?  Kwa sababu Bwana mfufuka na aliyepaa mbinguni anawatuma mitume wake kutangaza Injili duniani kote. Na zaidi kupaa kwa Bwana ni kutuhimiza kuelekeza mioyo na  mtazamo wetu juu mbingu, ili baadaye kuendelea kutazama hata ardhini kwa kujikita kwenye matendo ya dhati ambayo Bwana Mfufuka ametukabidhi!

Ni mwanzo wa tafakari ya Baba Mtakatifu Francisko  Domenika ya tarehe 13 Mei 2018, wakati Mama Kanisa anaadhimisha Sikukuu ya Kupaa Bwana Mbinguni , mara baada ya siku arobaini ya kufufuka kwake Yesu Kristo. Baba Mtakatifu Francisko ametoa tafakari hiyo kwa mahujaji na waamini wengi kutoka pande zote za dunia wakati wa sala ya malkia wa Mbingu mjini katika uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican. Akiendelea na tafakari hii, anaonesha mwaliko, unatolewa na Injili ya siku ambayo inajikita katika tukio lenyewe la  Kupaa kwa Bwana Mbinguni,  lakini mara baada ya kuwakabidhi mitume wake shughuli ya kufanya. 

Hii ni shughuli ambayo haina kikomo anathibitisha Baba Mtakatifu,kwa maana haina mwisho na ambayo inashinda nguvu za kinadamu. Yesu kwa dhati anawatuma mitume wake: “ Enendeni duniani kote, kulitangaza Injili kwa kila kiumbe (tazMk 16,15). Hii ni jambo la kushangaza hasa ukifikiria kwamba,  anawakabidhi kundi dogo la  mitume ambao walikuwa ni watu rahisi, wasio na uwezo mkubwa kitaaluma! Lakini pamoja na  na kutokuwa na taaluma ndicho  kinakwenda kukabiliana na wakuu wa dunia na kuwaalika wapeleke ujumbe wa upendo na huruma ya Yesu kwa kila pembe ya dunia!

Baba Mtakatifu anafafanua kuwa, mpango wa Mungu unawezakana tu kwa nguvu za Mungu mwenyewe ambaye anawakabidhi mitume wake. Kwa maana hiyo Yesu anawahakikishia kwamba,  utume huo utaongozwa na Roho Mtakatifu. Bwana Yesu anasema: Mtakapopokea   nguvu ya Roho, atawashukieni  ninyi, mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, katika nchi yote ya Yudea na Samaria na hata miisho ya dunia (Mdo 1,8). Na utume huo uliweza kukamilishwa, kwa maana mitume walianza kazi hii ambayo inaendelezwa na wengine walio fuata. Utume alio ukabidhi Mitume wake  kwa karne nyingi bado hata leo hii unaendelea, japokuwa unahitaji  ushirikiano wa dhati, na kuongeza: Kila mmoja kwa nguvu ya Ubatizo alio upokea utume huo anao uwezo kushiriki upande wake na kutangaza Injili. Ni ubatizo unaotupatia uwezo, hata kutoa msukumo wa kuwa mmisionari na kutangaza Injili.

Kupaa kwa Bwana mbingunu ni mwaliko mpya wa kuona uwepo wa Yesu kati yetu na unatualika kuwa na macho na moyovilivyo wazi ili kuwa naye na kuweza kumhudumia  na kumshuhudia kwa wengine. Ni waamini wote, wawe wake  au waume wa kupaa , maana yake watafutao Kristo katika njia zake katika nyakati zetu na kuchuka neno la wokovu hadi miisho ya dunia. Katika hatua hizo tunakutana na Yesu mwenyewe kwa ndugu na  zaidi wale maskini, wanaoteseka katika miili yao na majaribu ya  uzoefu wa uzee, hata katika umaskini mpya kijamii. Kama ilivyo kuwa mwanzo  wa Kristo mfufuka kwa  kuwatuma mitume wake kwa nguvu ya Roho Mtakatifu, leo hii Yeye pia anawatuma wote, yaani sisi kwa nguvu zile zile ili kupeleka ishara za dhati, zinazo onekana za matumaini. Yesu anatupatia matumaini kwa sababu yeye amekwenda mbinguni na amefungua milango ya mbingu akiwa na matumaini ya kwamba hata sisi tutafika huko!

Bikira Maria ambaye ni Mama wa Bwana wetu aliyekutafa na kufufuka  na kushiriki kwa imani katika jumuiya ya kwanza ya mitume , atusaidia ili tuendelee kuelekeza mioyo yetu juu kama anavyoshauri kufanya katika Liturujia. Na wakati huo huo atusaidie kukanyaha  miguu yetu ardhini na kupanda kwa ujasiri Injili katika hali halisi za kila maisha na katika historia.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!

14/05/2018 15:59