2018-05-14 15:43:00

Semina juu ya kuelimisha vijana katika mwanga wa Amoris Laetitia!


Tarehe 4-5 mei 2018 imefanyika semina ya pili  kimataifa ya mtandao wa wataalam ambao wanajifunza na kufanya tafiti za elimu kwa mantiki ya kihisia na kijinsia, semina iliyo andaliwa na Baraza la Kipapa la Walei Familia na maisha kwa kuongozwa na mada ya “Kuelimisha vijana katika mwananga wa Amoris Laetitia”, yaani  kutoka katika wosia wa Baba Mtakatifu Francisko  juu ya furaha ya upendo  ndani ya Familia.

Waataalam kutoka katika vitengo vya taalimungu, falsafa ,uchungaji, elimu na mawasiliano kutoka sehemu mbalimbali za dunia wameunganika na wahusika wakuu wa Baraza hilo, kwa lengo kutaka kutoa uhai katika  mfumo wa kiditali katika huduma  kwa ajili ya wazazi na vingozi, walimu ambao kwa dhati wanajuhusha kwa kipindi kirefu katika utambuzi wa mipango ya elimu kwa mantiki ya kihisia na kijinsia  mantiki ambazo tayari zipo katika hali halisi ya nchi tofauti duniani kote. Vilevile semina hiyo ilikuwa ni kutaka kukabiliana na kukutana kati yao wataalam  kwa ajili ya maendeleo zaidi ya kuanzisha hata mambo mengine mapya yanayo kusudiwa na kushuhudiwa na  Kanisa mahalia, kwa kutoa mapendekezo na kutafuta ukweli wa uhai wa maisha ya dhati katika jumuiya mbalimbali mahalia.

Aliyefungua semina hiyo ni Kardinali Kevin Farrelli rais wa Baraza la Kipapa la Walei, Maisha na familia ,kwa hotuba yake, ambaye pia iliweza kuweka chachu na hotuba ya  Padre Alexendre Awi Mello Katibu wake na msidizi pia kwa upande wa Maisha Bi Gabriella Gambini. Matoke ya kwanza ya mpango katika jumuiy mbalimbali , itawakilishwa mwezi agosti wakati wa fursa ya Mkano wa Familia duniani mjini Bublin Ireland wakati huo semina ya kazi kama hiyo inatarajiwa kufanyika mwezi novemba mwaka huu!

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.