Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baba Mtakatifu Francisko \ Sala ya Malaika wa Bwana

Papa awaombea waathirika wa shambulio la kigaidi nchini Indonesia!

Waamini nchini Indonesia wakiombea ndugu zao walio athirika katika shambulio la kigaidi - AP

14/05/2018 16:14

Niko karibu na watu wapendwa wa Indonesia kwa namna ya pekee jumuiya ya kikristo ya mji wa Surabaya , waliopata shambulio baya na  kubwa dhidi ya maeneo ya ibada. Ninatoa sala zangu kwa ajili ya waathirika wote na ndugu zao wote. Kwa pamoja tuombe Mungu wa amani ili aweze kusitisha matendo ya nguvu na vurugu pia ili ndani ya mioyo yote isiwepo nafasi za hisia ya chuki na vurugu, badala yake iwe nafazi ya mapatano kindugu. Ni ujumbe wa maskitioko yake Baba Mtakatifu aliyo utoa mara baada ya sala ya Malkia wa mbingu katika viwanja vya Mtakatifu Petro mjini vatican,tarehe 13 Mei 2018 ikiwa ni Sikukuu ya  Domenika ya Kupaa wa Bwana. 

Baba Mtakatifu Francisko, akindelea na maneno yake kwa mahujaji na waamini pia amekumbusha juu ya Tukio la siku ya 52 ya Maadhimisho ya upashanaji habari  duniani, ambayo imeongozwa na kauli mbiu 2018 “Fake news”, kwa maana ya habari za kughushi na uandishi wa amani”. Baba Mtakatifu ametumia fursa hii kuwasalimia wahudumu wote wa vyombo vya habari, kwa namna ya pekee waandishi ambao wanajikita kutafuta ukweli wa habari na  kuchangia katika jamii ya haki na amani.

Baada ya kuwataja na kuwasalimia makundi kadhaa walio udhuria sala ya Malkia wa mbingu, wazo lake pia limewaendeea  kikundi cha wahanga wa  kujitolea, wapanda milima, ambao wameunganika mjini Trento nchini Italia katika Mkutano wao wa kitaifa. Amewatia moyo ili wawe mashuhuda wa upendo na wahudumu wa amani kwa mfano wa Teresio Olivelli, mtu wa kujitolea na mtetezi wa wadhaifu, ambaye hivi karibuni ametangazwa kuwa mwenyeheri. 

Kadhalika akikumbuka siku ya akina mama inayoadhimishwa kila wiki ya pili ya mwezi Mei nchi nyingi za dunia, ameomba kuwapigia makofu mama wote, amesalimu na kuwashukuru kwa ajili ya kutunza familia. Aidha amekumbuka mama wa Mbinguni ambaye katika tarehe 13 Mei ya  ila mwaka inakumbusha Mama Yetu wa Fatima aliye watoke watoto watatu wa Fatima mnamo mwaka 1917. Baba Mtakatufu amesema Mama Maria atusaidie kuendelea katika safari yetu ya kiroho. Amewatakia matashi  mema siku ya Domenika na kuomba sala kwa ajili yake kama kawaida na mwisho kuwaaga!

Tukirudi katika tukio la shambulio nchini Indonesia, vyombo vya habari na utawala  mahalia, vinathibitisha kuwa idadi ya watu walio uwawa katika shambulio la kigaidi nchini Indonesia, imepanda kutoka watu wawili na kufikia watu 9. Watu wengine 13 wamejeruhiwa, katika mashambulio ya kigaidi yaliyolenga makanisa kadhaa katika mji wa pili kwa ukubwa nchini humo wa Surabaya.  Idara ya polisi kupitia kwa msemaji wake Frans Barung Mangera, imesema kuwa mashambulio matatu tofauti yalitokea kwenye makanisa- Kusini mwa Java, aidha  Idara ya usalama imeongeza kusema kuwa, milipuko yote mitatu ilitokea dakika kumi baada ya nyingine na mashambulio hayo yanaminika kutekelezwa na Kundi la serikali ya kiislam linalojiita Jemaah Ansharut Daulah na miongoni mwa waliouwawa ni pamoja na mhanga wa kujitoa kufa.

Sr Angela Rwezaula
Vatican News!

14/05/2018 16:14