Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baba Mtakatifu Francisko \ Hotuba

Tanzia: Professa Mario Agnes amefariki dunia!

Papa Francisko anamkumbuka kwa moyo wa unyenyekevu na shukrani Prof. Mario Agnes aliyefariki dunia hivi karubuni na kuzikwa tarehe 12 Mei 2018.

12/05/2018 18:08

Baba Mtakatifu Francisko amepokea kwa majonzi mazito taarifa za kifo cha Professa Mario Agnes, aliyewahi kuwa Rais wa Chama cha Vijana wa Italia kitaifa na Mkurugenzi mkuu wa Gazeti la L’Osservatore Romano linalomilikiwa na kuendeshwa na Vatican. Baba Mtakatifu anakumbuka kwa unyenyekevu na moyo wa shukrani dhamana na utume uliotekelezwa na Professa Mario Agnes enzi ya uhai wake katika maisha na utume wa Kanisa.

Huyu alikuwa ni mwamini mlei, aliyejisadaka bila ya kujibakiza kwa ajili ya huduma kwa gazeti la L’Osservatore Romano. Baba Mtakatifu anaiombea roho ya marehemu Professa Mario Agnes, iweze kupokelewa miongoni kwenye utukufu wa Ufalme wa Mungu. Anapenda kuwafariji na kuwaombea wale wote walioguswa na kutikiswa na msiba huu mzito!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Vatican News!

12/05/2018 18:08