Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Kanisa Barani Afrika \ Amani

Kanisa Katoliki A.Kusini washutumu tendo la kuchoma Msikiti wa Durban !

Maombolezo kwa kifo cha Imam katika msikiti wa Durban Afrika ya Kusini aliyeuwawa na wengine wawili kujeruhiwa - AP

12/05/2018 15:20

Tumepokea kwa mshutuko pia maskitiko makubwa ya mashambulizi ya msikiti wa Imam Hussein huko Verulam, Durban  na janga kubwa la kuwawa kwa imaman wa msikiti huo na wengine wawili kujeruhiwa. Ndiyo maneno yaliyomo katika ujumbe uliotiwa saini na Askofu Stephen Brislin, Askofu Mkuu wa Cape Town na Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Afrika ya Kusini (SACBC, wakishutumu vikali shambulizi la kigaidi katika msikiti wa kiislam mapema wiki hii katika mji huo.

Askofu Mkuu Brislin kwa niaba ya Kanisa Katoliki Afrika ya Kusini, anatoa salam za rambi rambi kwa wanafamilia na marafiki wa Imam aliye uwawa pia kuwatakia heri na baraka ili wapene  kwa haraka wale wote waliojeruhiwa. Katika ujumbe huo unaonesha kuunganika na kusononeka na wanajumuiya wa msikiti wa Imam Hussein,ambao pia  umeaharibi  vibaya kwa moto na  wakati huo kubaki katika sala ya kuwaombea.

Halikadhalika ujumbe unashitumu vikali umwagaji dumu  na mashambulizi yasiyo na maana, wakiomba nguvu za vyombo vya serikali kufanya kazi yake  kwa haraka ili kuhakikisha wanapatikana wahusika hao na kutendewa haki kwa kile walichotenda kwa mujibu wa sheria. Askofu Brislin anahitimisha, akisema kuwa, uvumilivu wa dini umekuwa ni wa muda mrefu na wenye tabia ya jamii ya Afrika ya Kusini  ambao haukuwahi kumdhuru mwingine na kwa maana hiy wataendelea kusali kwa ajili ya amani katika nchi yao na dunia nzima, amani inayojikita juu ya kuheshimu hadhi na haki za kila binadamu.
Kwa mujbu wa shirika la habari za kimisionari Fides, mnamo mnamo 10 Mei baada ya sala ya saa sita , watu watatu wenye silaha na visu waliingia ndani ya miskiti na baada ya kuwachoma visu watu watatu , waliwasha moto msikiti huo, Imani alikufa pale pale, wakati watu wawili walibaki wamejeruhiwa.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News

12/05/2018 15:20