Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Kanisa \ Kanisa Ulimwenguni

Chama cha Signis kitafanya Kongamano mjini Seoul mwaka 2021!

Viongozi wa chama cha Signis wamechagua Kongamano la Kimataifa kwa mwaka 2021 kufanyika njini Seoul nchini Korea ya Kusini - RV

12/05/2018 13:30

Chama katoliki duniani kwa ajili ya mawasiliano  Signis kitafanya kongamano lake  huko Seoul nchini Korea ya Kisini mwaka 2021. Uamuzi huo ulitolewa  katika mkutano wa mwaka ulifanyika mjini Bruselles hivi karibuni na wa Baraza kuu  la  Chama hicho.  Kila baada ya miaka 4 Signis uandaa tukio la kimataifa, ili wanachama wake na marafiki waweze kukutana, kujadiliana na kubadilishana mawazo juu ya maendeleo  uendelevu ya vyombo ya habari na mawasiliano. Hata hivyo  ipo mikutano kama hiyo iliytanguliwa kufanyika maka vile wa Roma (2001 na 2014), Lione 2005, Chiang Mai 2009 na Québec City 2017. 

Katika kung’amua maeneo ya kijiongrafia kati ya nchi ya China na Japan ni kutaka kuonesha umuhimu wa Uinjilishaji wa kanda hiyo kwa maana katika eneo liliochaguliwa  kufanyika tukio hili kubwa la kimataifa , historia ya   Kanisa Katoliki hilo haikuwahi kupata mwanzo wa wageni wa kimisionaria kama ilivyo katika maeneo mengi ya nchi duniania, kinyume chache ni kwa njia ya waamini walei mahalia ambao walijifunza taratibu kumjua Yesu wakati wa kufanya  ziara yao ya kila mwaka katika mji wa Peking! Kwa mujibu wa Signis anathibitisha kuwa, nchi ya Korea ya Kusini kwa dhati wapo waamini wengi katoliki wanao wakilisha  asilimia 11% ya watu wote ambao ni (karibia milioni 5,8 ya waamnini) na Kanisa Katoliki la Korea, kwa dhati liko mwendao kazi wa uinjilishaji kwa Bara la Asia ya Kaskazini. Mkutano wa Signis mwaka 2021 pia unakwenda sanjari na kumbukumbu ya miaka 200 tangu kuzaliwa kwa Mtakatifu Andrea Kim , padre wa kwanza mkatoliki nchini Korea , anayewakilisha kifodini cha wakorea wengi na ambaye anajulikana na kupendwa sana na waamini wakatoliki nchini Korea.

Atakaye karibisha mgeni wa Kongamano la kimataifa la Signs atakuwa ni Chuo Kikuu Katoliki cha Seoul cha Korea ya Kusini , kinachoendeshwa na Jimbo Kuu la Seoul;  kati ya shughuli za kiutamaduni ambazo zitafanyika wakati wa tukio hilo litakuwa lile la kutembelea sehemu inayolindwa na wanajeshi mpakani unaoigawa nchi ya Korea ya Kusini na ile ya Kaskazini.  Halikadhalika katika  kuadhimisha  siku ya 52 ya Upashanaji Habari ikiongozwa na kauli mbiu “Ukweli utawaweka huru: Habari za kughushi na uandishi wa habari wa amani” Signis na Sekratarieti ya mawasiliano imetoa kampeni ya shindano kimataifa kwa kauli mbiu “#giveTRUTHvisibility” “ toa ukweli unao onekana”.

Shindano hilo linajikita katika uengenezaji wa    picha kubwa na video inayowalenga watoa habari. Michoro hiyo na utengenezaji wa video  dunia nzima  unajikita juu ya mada ya siku ya 52 ya Upashanaji Habari, 2018 yenye kauli mbiu “Ukweli utawaweka huru: Habari za kughushi na uandishi wa habari wa amani”. Chama katoliki duniani kwa ajili ya mawasiliano Signs na Sekretarieti ya Mawasiliano Vatican wametoa shindano hilo “#giveTRUTHvisibility”, kwa kutaka kukusanya kutoa chachu hai katika suala la nyeti na changamoto za kisasa kuhsu mawasiliano. 

Signis ikielezea juu ya  shindano hilo, ni kwamba wale wote wanaotaka kuingia katika shindano, wanaweza kutuma video yao, au picha iliyochorwa lakini ikihisiana  na mada ya ujumbe wa wawasiliano 2018. Na kwa washindi wa kampeni hiyo wataweza kupata zawadi ya fedha. Kwa mujibu wa Bi Helen Osman Mwenyekiti wa Signis anathibitisha kwamba  hii ni kutaka kuhamasisha na kutia moyo talanta nyingi zilizopo katika dunia hii, ili kukabiliana  na mada hiyo msingi kwa utambuzi wa kazi binafsi kwa njia ya mitandao katoliki duniani.

Naye Nataša Govekar, mkurugenzi wa kitengo cha kitaalimungu -kichugaji cha Sekretarieti ya Mawasiliano Vatican, na mwakilishi rasmi katika chama cha  Signis amesisitiza zaidi juu ya  lengo jipya la kuanzisha tukio hilo na kwamba ni kutia  moyo katika mazungumzo ya kimataifa juu ya mada hasa ya Habari za kughushi. Na ni mategemeo yake, shindano hili linaweza kutoa msukumo na sababu zaidi kwa vijana kutoa mchango wao  kwa namna ya ubunifu wa mada ya “Habari za kughushi” kuelekea katika “uandishi wa habari wa amani”.

Mwisho wa  kushiriki shindano lazima kujiandikisha na kutuma kabla ya tarehe 30 Septemba 2018.  Picha na video zitaweza kusambazwa duniani kote kwa njia ya wanachama wa Signis ambao wako katika nchi 90 duniani;na maelezi kamili ya kijiandikisha katika shindano hilo yanarudiwa mara kwa mara katika uwanja mpana wa Facebook, na wote mnaalikwa kushiriki shindano hilo. Katika  maelezo mengi zaidi  na kutambua Chama cha Signs unaweza kuingia katika tovuti: http://http://www.signis.net

Sr Angela Rwezaula 

Vatican News  

 

12/05/2018 13:30