Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Kanisa Barani Afrika \ Elimu

Tanzania: Andaeni makatekista watakaotetea na kulinda watoto!

Mpango wa utetezi na ulinzi wa watoto wadofo nchini Tanzania uliotolewa na Baraza la Maaskofu unatakiwa kuwekwa kwenye matendo na siyo kinadharia - RV

11/05/2018 16:04

Makatekista wote wa nchi wanapaswa kujifunza vema juu ya siasa  ya utetezi na ulinzi wa watoto  iliyokubaliwa na maaskofu mnamo mwaka 2017. Habari zilitozotolewa na Shirika la habari za kimisionari fides wanathibitisha kuwa  Padre Jovin  Riziki Mkurugenzi wa ofisi ya huduma za kijamii wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC amethibitisha kuwa katika kazi nzuri iliyofanywa na Kanisa, hasa katika utangulizi kwa mantiki ya dini kati ya watoto, maaskofu wanaonesha   wajibu wa kila mtu kuendeleza uwezo na kujifunza vema juu ya siasa ambayo inalinda na kutetea kwa namna ya kufikia watu wengi katika utoaji wa nyenzo msingi za kusimamia na kuwalinda watoto.  Padre Riziki amethibitisha hayo wakati wa hotuba yake katika semina ya  siku tatu uliyoandaliwa na Sekretarieti ya jimbo kuu kwa ajili ya makatekista na semina hiyo imemalizika  hivi karibuni, kurasini jijini Dar Es Salaam Tanzania.

Wakati wa hotuba hiyo, Padre Riziki pia ameongeza kusema kwamba hata  Waziri wa Afya ameagiza kuwakilisha mpango mzima juu ya utetezi na ulinzi wa watoto, uliokubaliwa mwaka jana na maaskofu wa nchi katika ofisi yake, mpango ambao unapaswa kujikita katika matendo ya dhati hasa  kwa wale wanao fanyakazi ndani ya Kanisa Katoliki na wale ambao wanajikita na shughuli ya ufundishaji shuleni na vituo vya kulea na kutunza yatima. Kwa maana hiyo ni lazima kuwasaidia wengine mafunzo kama hayo katika majimbo juu ya kuanzishwa kwa shughuli hii ya maaskofu katoliki nchini Tanzania.
  
Katika semina hiyo pia hawakukosa kujita kwa kina kuhusiana na  mada nyeti sana  inayohusu vitendo viovu na vihalifu dhidi ya watoto, na jinsi  gani watoto wengi wanaathirika kisaikolojia, kihisia, hata kijinsia, suala nyeti ambali linazidi kuongezeka ndani ya jamii. Siasa hiyo ni wazi, kwa maana kila anayejiingiza katika ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto, lazima ahukumiwe.Kati ya lengo madhubiti na  msingi la  maaskofu katoliki  Tanzania, ni lile la ulazima wa kuanzisha  ofisi kwa ngazi ya kitaifa na kijimbo, kwa maana  ya kwamba, masuala yote yanayohusu manyanyaso ya wadogo yaweze kukabiliwa kwa kina. Zaidi Padre Riziki amehitimisha akisema, shule zote zinapaswa kuwa na mwakilishi na mwakili wa kulinda na kutetea watoto, ili kuweza kung’amua wale ambao wana athiri wadogo na habari hizo ziweze kufika  Parokiani au katika ofisi ya mkurugenzi wa jimbo anayehusika na utetezi wao kwa ufanisi wa kukabiliana na tatizo.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News

11/05/2018 16:04