2018-05-11 15:43:00

Nchi Takatifu inaandaa hatua za kiroho kwa wanafamilia ya Mungu!


Mwishoni mwa mwezi wa nne, katika miji ya Yeriko na Nazareti ilifanyika kozi kwa  vingozi wanaosaidia wanandoa na vijana,ili kuweza kuwasaidia na kuongoza hatua za kiroho ndani ya falilia. Hii ni sehemu ya  mpango wa kichungaji kwa miaka miwili 2018-2019 katika maparokia ya Israeli na Palestina. Kozi hii imeandaliwa na Baraza la Kichungaji kwa ajili ya Familia mjini Yerusalemu, mahali ambapo washiriki 100  viongzo wameudhuria kozi hiyo, katika Mpango huo wa  kipatriaki mjini Yerusalem  ambao kwa dhati ni wa kweli na wa ubunifu!

Lengo la kuwafundisha kikundi hicho ni kutaka waweze kusikiliza  kwa makini mahitaji ya familia, hata  katika maparokia mahalia, kwa namna ya kutaka kupyaisha ndani ya familia yale mahusiano na watoto; mahusiano na wengine, kama vile, jinsi gani ya kukabiliana na kipeo cha nchi  na utume wa Familia katika Kanisa na jamii,kuanzia katika maparokia binafsi ya upatriaki wa Yerusalemu.

Akifafanua zaidi juu ya kozi hiyo kwa wahudumu hao,  Padre Rafiq Khoury, Katibu Mkuu wa Baraza la Kichungaji , amesema hiyo ni kuanzia katika hali halisi na ukawaida wa shughuli zao za kila siku na ili  kwamba, waweze kufikia hatua ya kusoma na kutafakari  kwa kina na kushirikishana maandiko matakatifu ya kale, kwa mtindo kweli wa kawaida wa kushirikishana. Aidha kwa yule anaye alikwa kuwa kiongozi wa mchakato wa kusindikiza familia, anaalikwa kutafakari kwa kina na kutambua lengo kuu la mchakato mzima wa kusindikiza wana familia , uliotengenezwa na kutolewa na Baraza la Kichungaji ka Upatriaki wa Yerusalemu.

Hata hivyo pia shughuli hiyo imeanza tangu mwanzo wa mwaka huu na ambayo amethibitisha kuwa, inatia moyo, maana hiyo, matokeo ya hatua hiyo yataonekana katika tafakari zaidi mwaka kesho; lakini kwa Kwa sasa wazo kuu ni kuwasindikiza familia zote katoliki  na vijana katika maisha yao na mwaka kesho mafunzo  kama hayo yatafanyika katika mji wa Betlehemu tarehe 25 -26 Mei!

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.