Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baba Mtakatifu Francisko \ Hotuba

Askofu mkuu Gabriel Charles Palmer-Buckle ahamishiwa Cape Coast

Askofu mkuu Gabriel Charles Palmer Buckle ateuliwa kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Cape Coast nchini Ghana.

11/05/2018 15:29

Baba Mtakatifu Francisko ameridhia ombi lililowasilishwa kwake na Askofu mkuu Matthias Kobena Nketsiah wa Jimbo kuu la Cape Coast, nchini Ghana la kutaka kung’atuka kutoka madarakani. Wakati huo huo, Baba Mtakatifu amemtuea Askofu mkuu Charles Palmer Buckle, kuwa Askofu mkuu wa Jimbo Kuu la Cape Coast. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Gabriel Charles Palmer Buckle alikuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Accra, Ghana.

Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Gabriel Charles Palmer Buckle alizaliwa kunako tarehe 15 Juni 1950. Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi, akapewa Daraja Takatifu ya Upadre tarehe 12 Desemba 1976. Mtakatifu Yohane Paulo II akamteua kuwa Askofu wa kwanza wa Jimbo Katoliki la Koforidua, nchini Ghana na kuwekwa wakfu hapo tarehe 6 Januari 1993. Tarehe 28 Mei 2005 akateuliwa kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Accra, nchini Gana. Tarehe 11 Mei 2018 Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Cape Coast, nchini Ghana.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Vatican News!

11/05/2018 15:29