2018-05-10 15:56:00

Mazungumzo ya kidini kati ya wakristo na waislam huko Amman Jordan!


Kila mtu au kikundi kinacho jikuta katika hali ya mahitaji kutokana na kuathirika na mateso, anapaswa kupewa msaada, kwani huyo/ hao ni ndugu kaka na dada kibinadamu, pia ni suala ya haki kwa kila binadamu!  Amethibitisha  hayo Kardinali Jean-Louis Tauran katika ujumbe aliowatumia washiriki wa mazunguzmo ya pamoja kati ya Baraza la Kipapa la Majadiliano ya kidini na Taasisi ya mafunzo ya Imani za kidini, mkutano uliofunguliwa tarehe 9 na  kufungwa 10 Mei 2018 katika mji Mkuu wa Amman nchini Jordan.

Ujumbe wa Kardinali, umesomwa wakati wa uzinduzi wa mkutano wa mazungumzo hayo na Askofu Miguel Angel Ayuso Guixot, katibu mkuu wa Baraza la Kipapa la Mazungumzo ya kidini, akiongoza wajumbe Katoliki na kati yao akiwepo Monsinyo Khaled Akasheh, mkuu wa ofisi ya Kiislam; wakati huo huo wawakilishi wa kiislam aliongoza Mfalme El Hassan bin Talal, rais wa Baraza tawala la Taasisis inayo wakaribisha. Mada kuu ya mazungumzo ya kidini hadi tarehe 10 Mei 2018, ni dini na hadhi ya maisha  na mazunguzmo ya kidini katu ya dini mbalimbali kwa namna ya pekee ya kiislam na kikristo kwa kuchanganua kwa kina  mtazamo wa kikristo wa  kiislam!

Askofu akiendelea na kusoma ujumbe huo, amekumbusha matukio ya kutisha ya kigaidi kwa kile kijulikancho  Serikali ya kiislam katika nchi za Mashariki ya kwamba, hayawezi kamwe kusahaulika kwa sababu waliofanya matendo hayo maovu wametumia jina la dini na kusababisha uhalifu mkubwa zaidi dhidi ya binadamu. Pamoja na hayo ni sifa kwa utambuzi wa hakika kwa upande wa viongozi wa dini ya kiislam na waislam wengine wengi kuweza  kukataa kabisa juu ya uthibitisho wa  uhalifu unaofanyika kwa kutumia jina la dini. Na siyo hiyo tu Askofu anasema  kwa maana haya kundi  dogo la kiislam hadi sasa limekuwa waathiri wa mateso na matokeo yake kulazimishwa kukimbia makumi elfu ya watu katika maendeo yao na wengi wao kuwawa na magaidi hao.

Ziara ya Baba Mtakatifu Francisko, mwezi Mei 2014 katika nchi hiyo, ilikuwa na maana ya kutaka kutoa msaada kwa ndugu na kaka waislam, kwa maana hiyo ni  kuonesha kuwa undugu ni suala muhimu katika maisha ya mwanadamu. Na kwa maana hiyo ni kuthibitisha kuwa suala la mshikamano kwa wale wanaoteseka ni wajibu wa kufanywa na madhehebu yote dini na imani kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Mazungumzo ya kidini katika ujumbe wake. Aidha  anasisitiza suala la ukaribu zaidi , kwani ndiyo msingi na uaminifu wa kila dini na waamini wake kuonesha kwa matendo ya dhati.

Mwisho Kardinali Tauran katika ujumbe wake, amezungumzia kwa kirefu juu ya dini ambazo zimekuwa  chanzo cha vurugu na ugaidi na kwa hakika anathibitisha kuwa, misimamo mikali kama hiyo ndiyo imekuwa sababu ya  jamii nyingi kukumbwa na umaskini, ukosefu wa haki, uhalifu na ukosefu wa matazamio endelevu, kwa njia hiyo Kardinali Tauran katika ujumbe huo unasisitiza kuwa,  sababu nyinginezo kwa sasa, haziwezi kabisa kudharauliwa au kuwekwa pembezoni na  bila kutazamwa kwa kina!

Na kutokana na  mazungumzo ya kidini, vitabu vya shule, mitandao na kwa namna ya pekee vyombo vya habari kijamii vinaweza kuchukua nafasi muhimu kwa maana ya kwamba, wakati mwingine inaweza kuwa hasi au chanya kwa ajili ya amani katika jamii na duniani. Na ndipo ameonesha umuhimu wa matendo ya dhati katika mang’amuzi, kwani, uchaguzi mbaya unaweza kusababisha itikadi mbaya, mivutano, mapigano na wengine, katika kesi za vurugu na ugaidi kwa jina la dini; na wakati kinyume chake, njia ya ukaribu wa dini inaweza kuwa kisima cha amani binafsi na kijamii na ambayo taratibu ikaweza kusambazwa amani duniani kote!

Sr Angela Rwezaula
Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.