2018-05-10 16:31:00

Makombora ya Isreali yauwa watu 23 nchini Siria na wengine kujeruhiwa!


Makombora ya Israeli yenye lengo la kulipiza kisasi dhidi ya Iran katika ardhi ya Siria yamesababisha vifo vya watu 23 na wengine kadhaa wamejeruhiwa. Jeshi la Israeli limesema limeyashambulia maeneo kadhaa ya kijeshi ya Iran katika maeneo tofauti ya Siria, katika kile kinachoelezwa kuwa ni moja kati ya opereshani zake kubwa za kijeshi katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni. Waziri wa Ulinzi wa Israeli Avigdor Lieberman anaelezea zaidi kuwa Iran ndiyo iliyaonza kuliingilia taifa la Israeli, ikijaribu kufanya makabiliano dhidi yao,na hawaruhusu Iran iifanye Siria kuwa eneo la mashambulizi dhidi ya Israeli. Na kuongeza kusema kuwa hiyo ni sera iliyo wzi sana na wanachotekeleza sasa kinazingatia sera hiyo.

Israeli ilifanya operesheni hiyo baada ya kusema kuwa wameshambuliwa na maroketi takribani 20 katika eneo wanalolikalia la milima ya Golan, ambapo mashambulizi hayo yalitokea upande wa Siria. Kwa mujibu wa shirika la uangalizi wa haki za binaadamu la Siria lenye makazi yake London, Uingereza operesheni hiyo imesabisha vifo vya wapiganaji 23 wakiwemo wanajeshi watano wa jeshi la Siria na wengine 18 kutoka makundi washirika. Tukio hilo limetokea baada ya wiki kadhaa za wasiwasi na kufuatia hatua ya rais wa Marekani, Donald Trump kujiondoa katika makubaliano muhimu ya mpango wa nyuklia wa Iran wa mwaka 2015! 

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News








All the contents on this site are copyrighted ©.