Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Kanisa Barani Afrika \ Maendeleo

Maaskofu wa Burundi kuwataka wanachi umakini wa kura ya maoni ya Katiba!

Wasiwasi wa Maaskofu nchini Burundi kuhusiana na kura ya maoni juu ya mabadiliko ya Katiba ya nchi kuhusu kubadili ibara ya 299

10/05/2018 14:23

Hivi karibuni, umetolewa ujumbe wa Baraza la Maakofu Katoliki Burundi kuhusu upigaji wa kura ya maoni ya kubadili Katiba itakayofanyika tarehe 17 Mei 2018. Katika ujumbe huo, Kanisa Katoliki la Burundi, linashutuma vikali juu ya pendekezo la maoni ya kutaka kubadli Katiba inayotarajiwa hivi karibuni, ambapo kwa maoni hayo ni kama kutaka kumwezesha rais Pierre Nkurunziza kubaki katika madaraka hadi mwaka 2034. Maaskofu wanaawalika watu wenye mapenzi mema kufanya tafakari makini katika mageuzi hayo, katika ujumbe huo  Baraza la maaskofu, wanaonesha wazi kutokubalina na tendo la rais kutaka kuondoa misingi ya katiba ya kuongoza miaka 5 na si zaidi ya hawamu tatu mfululizo.
 
Pamojana na hayo katika nchi ya Burundi, maoni ya mageuzi yanaendelea kuleta wasiwasi na mivutano mikali kati ya wapinzani wanao muunga mkono andelee tena miaka 15 zaidi wengine ambao hawakubalini na mabadiliko ya katiba. Maskofu wa Burundi wanafikiria kuwa, jambo muhimu kabla ya kubadilisha kwa kina maandiko ya Katinba hiyo, hawali ya yote lazima wakabiliana na kipeo kipeo cha nchi kwa upande wa kisiasa na kijamii kinacho ikumba tangu miaka mitatu iliyopita kwa kunyanyasa watu na kubaki na kuwatia hofu. Mpango wa kutazama kwa upya Katiba kwa mujibu wa Maaskofu hautilii maanani  ibara ya 299 ya sasa ya katiba kwa sababu mpaka  sasa haikufikiria kuwaunganisaha watu wa Burundi.

Ibara ya katiba hiyo kwa mujibu wa maaskofu wanasisitiza haina haja ya mchakato wa mabadiliko na ambayo yanaweza kutokea iwapo hadi sasa inahatarisha umoja wa taifa kati ya watu wa Burundi au mapatano. Maaskofu wanathibitisha kuwa,  wanachokiona hadi sasa nchini humo, badala ya kuunganisha watu wa burundi, utafikiri wamekula nyongo za  mahusiano kati ya watu wa jamii hiyo. Na kwa maana hiyo wanathibitisha kuwa, sasa siyo kipindi  mwafaka cha kufanya  mchakato wa mabadiliko ya Katiba! 

Lakini pamoja na hayo wanasema, kutokana na mfumo wa demokrasia ya Burundi, kura za maoni ndiyo zenye neno la mwisho, na hivyo ni mategemeo yao kwamba, kura za maoni ndizo zinaweza kuleta amani na uhuru kwa watu wa Burundi kwa kupiga kura ya ndiyo au hapana. Kwa maana hiyo, wanaalika wananchi na waamnini wenye mapenzi mema kujikita kwa kina kuona jambo jema kwa manufaa ya nchi. Hata hivyo wana wanakumbuka juu ya mkutano na makubaliano ya amani uliofanyika mjini Arusha nchini Tanzania, ambapo mkataba ulikuwa unaonesha juu ya kusitisha vita vya wenyewe kwa wenyewe,lakini pamoja na hayo tangu 2015 demokrasia imeendelea kuwa kipeo kikali cha nchi.

Mwaka huu kwa hakika rais Nkurunziza ameonesha upendeleo wa  katika uchaguzi ili kutaka aweze kuendelea katika hawamu ya tatu, lakini kwa kufanya hivyo ni kukiuka Katiba ya nchi na hata makubaliano ya Mkataba wa Arusha, tendo ambali hadi sasa limesababisha kipeo kikubwa cha kisiasa, katiba, kijamii na kiuchumi, na mamilioni ya watu wa Burundi kulazimika kukimbilia nchi zilizo karibu yake. Ujumbe wa maaskofu kupitia chombo cha habari za kimisionari Fides unahitishwa kwa kuwaalika na kuwashauri watu wote wenye mapenzi mema wasichanganyikiwe kwa sababu wanathibitisha kwamba, uchaguzi unapita lakini maisha yanaendelea mbele.

Maaskofu anasema, katika kila tokeo la uchaguzi wa maoni ya kura,yaani "ndiyo au hapa", ikishinda maoni ya ndiyo wataongozwa na Katiba Mpya, na iwapo itashinda kura ya maoni ya hapana, ina maana watendelea kuongozwa na katiba ambayo inaongoza hadi sasa.
Kutokana na hilo ndipo mwakiko wa nguvu kwa wote unatolewa kwamba, kitakacho hesabiwa sana kwa wanaburundi wote ni ile hali ya kubaki na umoja na kushughulikia kwa moyo wote ulinzi wa amani ya wana Burundi na ili mwishowe kuweza kufurahia demokrasia ya kweli.

Sr Angela Rwezaula
Vatican News!

10/05/2018 14:23