2018-05-09 15:19:00

Tarehe 8 Mei ni Siku ya Chama cha Msalaba Mwekundu Duniani


Ni zaidi ya miaka 150, inaadhimishwa Siku ya Dunia ya Chama cha Msalaba Mwekundu  na Nusu Mwezi mwekundu kila ifikapo tarehe 8 Mei sanjari na  kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwa mwanzilishi wake Henry Dunant. Ni siku ya aina yake, kwa ajili ya kuwakumbuka watu wa kujitolea milioni 17 duniani ambapo Chama cha Msalaba mwekundu kinashirikisha misingi ya kibinadamu, bila ubaguzi au kusimamia upande wowote wa chama, kwa kushirikiana na kile cha Nusu Mwezi Nwekundu,vikunganisha  vyama vya kitaifa 190 na kuunda mtandao mmoja wa kimataifa ambao ni muhimu kuandaa mipango kwa ngazi ya ulimwengu katika kutoa msaada, kukuza uwelewa , urafiki na ushirikiano na amani ya kudumu kati ya watu.

Ili  kuadhimish siku hiyo, kwa kawaida  huanzishwa mambo mengi ya kitaifa, lakini hata ya  kiutamaduni na mafunzo. Kwa namna ya pekee nchini Italia wametoa nafasi kubwa ya mafunzo, kuhusu mada  ya hutoaji msaada wa kwanza kwa namna ya pekee, jinsi gani ya kuokoa maisha kwa njia ya matendo rahisi. Lengo ni kuhamasisha watu juu ya mambo msingi ya kwanza hasa, kuingilia kati iwapo inatokea dharura kwa upende wa watoto.

Katika siku hiyo watu wa kujitolea duniani kote pia wanafanya kumbukumbu ya maneno ya Papa Francisko  aliyowambia wakati wa hotuba yake mnamo tarehe 27 Januari 2018 alipokutana na watu wa kujitolea wa Chama cha Msalaba Mwekundu katika Ukumbi wa Mwenyeheri Paulo VI. Katika hotuba yake, anaonesha kuwa, utume wa mtu wa kujitolea unajikita katika kuinama kwa kila mtu anayehitaji msaada kwa haraka kwa namna ya upendo upeo. Ili kueleza hiyo aliongozwa Injili ya Msamaria mwema, ambaye mara baada ya kumwona mtu aliyejeruhiwa na maharamia, hakupitia mbali na mtu  huyo. Alikuwa ni mgonjwa na hakumkumu, wala kijiuliza maswali ya kimadili au kidini, kwa urahisi alianza haraka kumfariji majeraha yake.

Baba Mtakatifu pia alisisitiza juu ya Kanuni msingi ambayo Katiba inahimiza kwa chama hicho,  hasa ya kwanza ikiwa ni ubinadamu, kwamba wao wanajikita kwa namna ya kuzuia na kutoa faraja kwa kila mateso ya kibinadamu. Na kutokana na mateso hayo yalimfanya Baba Mtakatifu akumbuke na kuonesha hali halisi ya mateso yaliyopo katika uso wa dunia yetu, kuanzia kwa watoto, wazee na watu wengi wasiojulikana na ambao  alisema, sura zao hazijulikani, zimejificha chini ya kivuli cha sintofahamu. Aidha hali halisi kama ile ya majanga ya asili, tetemeko la ardhi mafuriko na uokaji wa wahamiaji baharini.

Akiendela kutoa maana ya utume wa watu wa kujitolea alisema kuwa ujezi wa umoja na uelewa kati ya mt una watu, kuanzisha amani ya kudumu yenye msingi wa kibinadamu na kijamii,na hisia za urafiki.  Kutokana na hiyo Baba Mtakatifu alihimiza  kutazama wengine kwa miwani inayoona karibu zaidi ya mbali ambayo inatazama urafiki uanao shinda vizingiti vya kuona mtu kama mgogoro, badala yake wanachama wasaidie kuwa wajenzi wa dunia inayo onekana na iliyo jaa ubinadamu. Msingi mwingine wa kanuni ya Chama cha Msalaba Mwekundu  unahimiza uadilifu, ambao Baba Mtakatifu alisema kuwa hausimamii upande wowote, iwe katika migogoro binafsi  au  katika migogoro ya kisiasa, rangi au ya kidini. Kigezo hiki cha utekelezaji kinatofautiana sana na mwenendo ambao leo kwa bahati mbaya umeenea alisema na kuongeza kwa amasikitiko, wa kutofautisha nani anayestahili hukudumiwa au kusaidiwa  kutoka kwa wale, ambao kinyume chake wanaitwa wasiyo stahili.

Na kwa maana hiyo katika kukumbuka siku ya Msalaba mwekundu Duniani tarehe 8 Mei, inataka kurudisha kukumbusha maana ya utume wa ujenzi wa uelewa wa pamoja katika huduma ya jirani; katika  kudumisha shauku ya kimantiki ya kibindamu na jamii;  juu ya hisia za kirafiki na ili dunia iweze kweli kuwa bustani nzuri ya ubinadamu, kwa maana hata katika maneno yake ya mwisho, Baba Mtakatifu aliwakumbuka hata mashihidi wengi wa kujitolea walio kufa wakitoa maisha yao kwa ajili ya wengine. Hiyo ni kutaka kuthibitisha usema wa Yesu kuwa “Hakuna upendo zaidi kuliko mtu autoaye uhai wake kwa ajili ya rafiki zake na  ninyi ni marafiki zangu mkifanya ninayo wahamuru”( Yh 15,13-14)

Sr Angela Rwezaula
Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.