Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Kanisa \ Kanisa Ulimwenguni

Bikira Maria wa La-Vang nchini Vietnam anaheshimiwa sana na waamini wake!

Bikira Maria wa La- Vang nchini Vietnam akiwa na mtoto mikononi mwake, anaheshimiwa sana na waamini wengi nchini humo

09/05/2018 15:31

Tangu asili yake nchini Vietman  katika karne ya XVI wakati  walipofika wamisionari wa kwanza wakiwa wadomenikani, wafranciskani, kufutia  wajesuit, historia ya Kanisa la Vietnam ilikuwa inaendelea kuteseka na kuwa na wafiadini wengi. Kati ya mwaka 1625-1886 ufalme wa nchi hiyo ulitunga sheria 53 dhidi ya wakristo. Waathirika wa mateso hayo wanakadiriwa kuwa laki 130. Na Sehemu kubwa ya mashahidi waliotangazwa na Mtakatifu Yohane Pauli II walikatwa vichwa vyao, wengine kunyongwa, kuwekwa katika vinywa vya wanyama, au wengine kufa wakiwa katika gereza kufuatia na  mateso makali mwilini mwao.
 
Anayejuliana sana katika mateso hayo ni Padre Andrea Dũng Lạc, wa Vietnam aliyekatwa kichwa chake mnamo 21 Desemba 1839. Padre Lac alizaliwa mnamo mwaka 1785 katika familia moja maskini ya kivietnam. Akiwa bado mdogo aliuzwa na wazazi wake kwa katekista mmoja mkatoliki, ambaye kwa bahati nzuri alimlea vizuri na akakua kiakili katika akimwelekeza njia ya Kanisa hadi kufikia daraja takatifu la upadre mnamo  tarehe 15 Machi 1823. Baada ya kuwa paroko, alipata matatizo makubwa kutoka kwa viongozi watawala mahalia kutokana na ushuhuda wake kwa waamini, hivyo waliamua kumweka mahabusu. Hakutolewa humo hadi waamini kuingilia kati kwa njia ya kulipa fidia. Alihamishwa mara nyingi lakini hali hiyo iliendelea hivyo, kwa sababu ya utume wake wa kufundisha Neno na imani ya Kristo kwa wakatoliki, ndipo waliamua akatwe kichwa chake mara baada ya kulazimishwa kukana imani,  akiwa na Padre aliyekuwa amemkaribisha katika parokia yake, Padre  Pietro Trương Văn Thi, ch.

Kanisa la Vietnam pamoja na sifa ya uwepowa watakatifu wafiadini wengi lakini pia wanafanya ibada kuu ya Mama Maria, hasa katika madhabahu ya La -Vang  kwa sababu ya historia msingi mnamo mwaka 1798, Mama Maria aliwatokea kikundi cha wakristo wanaoteseka akiwa juu ya mti na kuwaeleza kuwa yeye ni kama mkuu wa mahakama  na “Msaada wa Wakristo”.

Mtakatifu Yohane Paulo II mnamo tarehe 19 Juni 1988 baada ya kuwatangaza watakatifu Mashahidi 117 wa Vietman, wakati wa sala ya Malaika wa Bwana alisema kuwa, kutokea kwa Mama Maria wa La-Vang na imani ya mahujaji katika  Madhabahu hiyo, hija ya mawazo yao iwapele moja kwa moja kati ya madhabahu za Mama Maria duniani ili kuweza kutua katika nchi ya Vietnam, nchi yenye rutuba ya damu ya wafia dini 117 ambao wametangazwa”.

Historia Madhanahu ya La Lang: Madhabahu ya La- Vang iko katika Jimbo Kuu la Hue nchini Vietnam katikati. Jina la La –Vang linatokana na msitu, mahali ambapo enzi za zamani jumuiya ndogo ya  kikristo ilizoea kwenda kuchanja kuni. Kuanzishwa kwa kituo cha Mama Maria huko kinatokana lakini na mateso makubwa ya wanajumuiya  hao , kwasababu mwaka 1789 wakristo walikuwa wamekimbia mateso ya Mfalme Canh-Thinh, bila kuogopa hatari yoyote ya wanyama wakali, njaa na magonjwa. Walikuwa wamekusanyika katika mti mkubwa sana, wakisali rosari ili kuomba msaada wa mateso hayo. Kwa njia hiyo Bikira Maria aliwatokea mara nyingi akiwa amemshika mikono mwake mtoto Yesu na kuwatia moyo ili wawe na  uvumilivu kwa maana atawalinda!

Vilivile historia ni kwamba,  mara ya amani kidogo katika  eneo hilo, mara moja walijenga kikanisa kidogo cha miti na ndiyo ukawa mwanzo wa hija ya waamini wengi. Na kutokana na mateso makali ambayo yaliendelea kuwasonga wakristo wa Vietnam kwa karne hizo waliendelea kujikabidhi kwa mama Maria. Na  ibada kuu ya Mama Maria ilibaki  kuwa ndiyo msingi wa imani ya mashahidi  hao ambao mara kwa mara hata walipokuwa wanakwenda kukabiliana na mauti, walikuwa wamevaa rosari shingoni mwao. Mwaka 1886 baada ya utulivu kidogo, Kanisa dogo la miti la Mama Maria wa La- Vang lilichomwa moto, lakini baadaye mwaka 1901, wakalijenga kwa upya Kanisa na kubarikiwa na  Padre Morineau,  mmisionari kutoka Ufaransa akiwa na waamnini wengi.
Kikanisa kiliweza kupanuliwa mwaka 1924 na Askofu Eugenio Allys, wa jimbo la Hue alikibariki, lakini kutokana na kuendelea na mateso ya Kanisa, kilichomwa kwa mara nyingine tena, lakini mahujaji waliendelea kwenda kusali rosari. Kulijengwa tena kikanisa cha muda japokuwa kabla ya  madhabahu hiyo kuharibiwa, Baraza la Maaskofu Katoliki wa Vietnam walikuwa tayari wameitangaza kuwa Madhabahu ya Mama Maria Kitaifa kwa Barua ya kichungaji mnamo 1961na mwaka huo huo pia hata Vatican iliweza  kuipatia  mahali hapo  utambulisho kwa cheo cha  Kanisa Kuu dogo.

Katika barua ya Vatican ilikuwa inasema; “Tunaweza kufikiria kuwa matendo haya yenye maana ya viongozi wa Kanisa ni matashi mema kwa ajili ya ujenzi wa madhabahu , ambayo ni matarajio yetu kufanyika mapema iwezekanavyo, katika  uhuru na amani na sifa na shukrani kwa  yule ambaye kizazi kinamwita mbarikiwa” (taz Lc 1,48). Kwa namna hiyo Madhabahu kwa njia ya maombezi ya Malkia wa mashihidi, inaweza kuendelezea fadhila zake na kiroho kwa ajili ya kuwasaidia si wakatoliki tu wa Vietnam, bali kwa umoja wa taifa, na zaidi katika maendeleo ya raia na kimaadili ya nchi”. Madhabahu hiyo ilijengwa kwa upya na kutabarukiwa mwaka 1998, na kurudia kuwa kituo kikubwa cha ibada ya Bikira Maria kwa wakatoliki na  watu wote wenye mapenzi mema !

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News

09/05/2018 15:31