2018-05-08 15:46:00

Mbio za waseminari wa Marekani kwa ajili ya msaada wa Iraq na Siria !


Mbio za kubalishana kijiti kwa  kilometa 250 kupitia nchini Italia kwa ajili ya ukusanyaji wa fedha ya kuwasaidia wakaristo wanao teseka katika nchi za Mashariki zinafanyika kwa mara nyingine tena mwaka huu. Ni mbio zilizo anzishwa na waseminari walioko  masomoni mjini Roma katika Taasisi ya Kipapa ya Amerika ya kusini, ambao hadi sasa wamweza kukusanya  Euro 1,200 ambazo zitaweza kusaidia chama cha Mfuko wa Kanisa hitaji (Acs) ili kuwezesha msaada katika nchi ya Siria na Iraq.

Mmoja wa waseminari kutoka nchi ya Louisiana Marekani ya Kusini Joseph Caraway, ambaye pia anafanya mbio hizo akihojiana na wawakilishi wa Chama cha Mfuko wa Kanisa Hitaji (Acs) amesema, inawezekana haziweze kukutana na mtu yoyote anayemfanyia mbio hizo, lakini hilo haliwezi kuzuia kupenda na kusaidia kwa njia ya matendo hai aliyo nayo. Vilevile anasema,wengine wanaweza kufikiria mbio ni jambo dogo sana la upendo, lakini yeye amejifunza kuwa, upendo kwa jirani unapitia hata katika ishara zilizo ndogo kabisa. Mshikamano unatoa nafasi kubwa, kwa mfano wa Kanisa katika ulimwengu, kwa maana kila mmoja anaweza kushiriki katika  kufanya uzoefu wa Kristo kwa namna na mtindo wake wa upendo. 
 
Kuhusiana na kampeni hiyo, mwaka huu ni  wa nne tangu kikundi cha wana mbio Mjini Roma waanze kujikita katika kampeni kwa ajili ya msaada. Wengi wao wanafanya mazoeiz kila wakati na wanakutana katika sehemu fulani ambap kabla ya kuanza mbio kwanza ni kusali pamoja, kwa maana hiyo ni zawadi wanayotaka kuitoa. 

Mseminari anasisitiza kuwa, haitoshi tu kutambua na kujua kuwa kunwa wakristo wanoteseka, kutokana na kukiri imani yao, badala yake ni kuonesha matendo ya dhati hata kama ni madogo. Lakini hata hivyo amesisitiza ulazima wa kusali kwa ajili ya ndugu hao wanaoteseka na kuwasaidia kwa matendo ya dhati. Miaka miwili mfululizo, waseminari hawa wametaka kwa mara nyingine tena ukusanyaji wa fedha hizi uwandeee  nchi ya Iraq na Siria kupitia chama cha Mfuko wa Kanisa hitaji, kwa maana ni rasolimali muhimu ya kusaidia ndugu katika matatizo yao, na hivyo  ni muhimu  kwa wote kuweza  kufanya mambo makubwa!

Sr Angela Rwezaula
Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.