2018-05-08 16:08:00

Kazi ya Maendeleo ya Binadamu Afrika ipo tangu mwanzo wa umisionari


“Wazo wa maendeleo endelevu ya binadamu linaweza kufikiriwa tu kuwa labda ni jipya , lakini si jipya bali limekuwapo tangu hawali, hasa kwa mtazamo wa Afrika, kwa maana tulipo pokea ujumbe wa ukristo kutoka kwa wamisionari, watu wetu wali upokea, si tu kama ujumbe wa kiroho lakini pia kwa sababu ni ujumbe mwema wa maendeleo ya binadamu”.

Hayo yamethibitishwa na Kardinali John Olorunfemi Onaiyekan, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Abuja nchini Nigeria akizungumzia juu ya maendeleo  endelevu ya binadamu  na ukuaji wa Kanisa la Nigeria kwa ajili ya ustawi wa jamii. Amezungumza hayo akiwa katika hija ya kitume hivi karibuni mjini Vatican na maaskofu wenzake wote ambapo walikutana na  Baba Mtakatifu,pia kupata nafasi ya kutembelea Mabaraza ya Kipapa,mojawapo,kutembelea hata Baraza la Kipapa kwa ajili ya maendeleo endelevu ya Binadamu.

 Kardinali Onaiyekan akiendelea na tafakari hilo anaseme, ni tangu mwanzo wa shughuli za kimisionari, shughuli za maendeleo ya binadamu na ile ya kichungaji, imekuwapo  bila kufikiria mmoja ni bora ya mwingine, na hivyo anapongeza mpango wa Vatican kuanzisha  Baraza la Kipapa linalojikita moja kwa moja na masuala hayo na ili kwa pamoja kuna uwezekano wa kufupisha umbali katika makanisa yao mahalia.

Na hivyo anasema, mfano Baraza la Maaskofu wa Nigeria, wanafikiria kwa namna ya umoja na ushirikishwaji wa kila kitu kinachotolewa kutoka katika Baraza hilo. Dunia hii inafuata mantiki ya ulimwengu lakini kwa sasa  hakuna  muda wa kubaki imegawanyika vipande bali upamoja. Kwa maana Kardinali anasisitiza, mapema iwezekanavyo ni lazima kujikita katika kukua kwa pamoja, wote kusaidiana katika maendeleo ya kiroho, ukweli na katika hadhi ya binadamu na hiyo ndiyo mambo msingi na kweli katika mchakato wa ukristo!

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News








All the contents on this site are copyrighted ©.