2018-05-07 13:51:00

Sinodi ya Maaskofu 2019 lazima ipate ufumbuzi wa Uinjilishaji Amazonia


Kwa mujibu wa Askofu Jose Lisboa de Oliveira msimamizi wa kitume wa Itacoatiara, huko Amazon ya Brazil aliyefika kwa mara ya kwanza Julai 2017 akihojiwa juu ya utume wake anasema, yuko anajaribu kuanza kuijua hali halisi ya Amazon. Amethibitisha hayo katika Gazeti la Habari za kimisionari Fides  wakati akuchambua juu ya umuhimu wa  Sinodi ya Maaskofu kuhusu Amazon itakayofanyika Oktoba 2019  hivyo anasisitiza kuwa, wako katika eneo ambalo daima limewakilisha changamoto katika uinjilishaji. Kwa mujibu wa Askofu ambaye hivi karibuni pia ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya kichungaji ya Mazingira, nchini humo anasema ni fursa kwa ajili yao, hata kwa Kanisa duniani, kuweza kuitambua hali halisi ya Kanisa la Amazzon ili kwamba wanaweza kujitka kwa matendo ya dhati ya unjilishji mahalia, vilevile wanaweza kutoa huduma yao kikamilifu katika watu hawa.

Zaidi Askofu Lisboa de Oliveira anasema kuwa, Sinodi tarajiwa hawali ya yote hiyo inaanzia katika hali halisi waliyo nayo na watakuwa na uwezo wa kusaidia kutafuta mbinu nyingine mbadala kwa namna ya kuwezesha mchakato wa  uinjilishaji unakuwa wa dhati,moja kwa moja kwa moja, wa ukaribu na watu ambao daima wameishi katika maeneo hayo na zaidi ambao sasa wanahitaji msaada wa uwepo wao wa mshikamano na ushirikiano ili kuendeleza  kuheshimu watu wa asili na utamaduni wao!

Hata hivyo Pia Askofu  amesimulia katika Gazeti la Habari za kimisionari Fides, juu ya matatizo ya maadhimisho ya Ekaristi Takatifu katika jumuiya nyingi za Amazzon ambayo ndiyo yalimsukuma Baba Mtakatifu Francisko kumtuma hata Askofu Mstaafu wa Jimbo la Xingu Aprili 2014, na ambaye baada ya zaiara yake alisema kuwa, Ekaristi katika jumuiya hizo ni jambo la kipekee,kwa maana misa  inaadhimisha mara moja au mbili kwa  mwaka. Kwa kufuata mawazo ya Askofu Krautler, ambaye ni mjumbe  wa Baraza la Maandalizi ya Sinodi,anathibitisha kuwa, kama Kanisa, ni lazima kutafakari ili kuwezesha  jumuiya zote zina fanikiwa kuwa  maadhimisho ya ekaristi kama ilivyo na  uwezekano wa kuadhimisha Neno la Mungu leo hii. Lakini Swali linakuja, ni jinsi gani  ya kupata wahudumu wa kuwawezesha kuadhimisha ekaristi katika jumuiya hizo? Na kwa hakika katika jumuiya hio wapo wachungaji, lakini wanakwenda kuadhimisha  mara chache sana. Kwa maana hiyo, jumuiya nyingi hazina mfuasi wa moja kwa moja anayewasaidia, na ndiyo maana ni rahisi kuingiza aina nyingi za mawazo ambayo daima siyo ya kidini.

Askofu anathibitisha kuwa Amazon ni jumuiya ambayo haina kiongozi wa kuwaongoza. Lakini pamoja na hayo matatizo hayo  hayajioneshi tu katika Amazon, lakini pia hata katika kanda nyingi nchini Brazil na duniani.Vilevile Askofu anaeleza, tatizo jingine ni lile ambalo linapaswa kukabiliana ni ulinzi wa msitu wa Amazon. Kama ilivyo kesi ya Brazil, Askofu pia anatoa wito wa serikali ya sasa kutafuta kila njia ili kuwezesha Ammazon na utajiri wake, kama ilivyo hata mipango inayohusu uuzaji wa misitu, utajiri wa madini au kuchukua ardhi ambayo ni mali ya watu wa asili. Katika mwanga huo Askofu hana wasawasi juu ya nafasi ya Kanisa aliyo chukua katika utetezi na ulinzi wa Amazon, ikiwa ni misitu, maji, watu wa asili, ambao kwa hakika ndiy mada kuu msingi zitakazo wekwa mbele ya mababa wa Sinodi, ili kuweza kutoa mwelekeo wa hakika kwa namna ya ambayo wote, kama ilivyo Kanisa zima, hata Amazon linaweza kuwa na majimbo, ubalozi, maparokia na jumuiya.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News








All the contents on this site are copyrighted ©.