2018-05-07 10:09:00

Nia ya Papa Francisko kwa mwezi Mei ni kwa walei ndani ya Kanisa


Kama kawaida ya nia za maombi ya kila mwezi kupitia mtandao wa kijamii, Baba Mtakatifu Francisko  kwa  mwezi wa Tano, maombi yake yamewaendea waamini walei  wote ambao wako  mstari wa mbele kujikita katika maisha ya Kanisa. Baba Mtakatifu Francisko anasema, Kanisa linahitaji ushuhuda wao kuonesha  ukweli wa Injili na mifano yao  hai ili  kuelezea imani kwa njia ya matendo hai na mshikamano! Anawashukuru waamini walei wote ambao kwa moyo wote wako tayari kujihatarisha na hawaogopi, kutoa maisha yao kwa maskini, walio baguliwa na kuwekwa pembezoni ili waweze kuwa na matumaini zaidi ya maisha yao.

Aidha anakazia zaidi  wito wa kusali  mwezi huu, ili waamini walei waweze kutimiza utume wao maalumu, walio upokea katika ubatizo na kujiweka tayari katika ubunifu wa  huduma ndani ya changamoto za ulimwengu wa sasa!

Sr Angela Rwezaula
Vatican News!

 








All the contents on this site are copyrighted ©.