2018-05-07 13:06:00

Akofu Mkuu Jurkovic katika Kamati ya maandalizi ya mkutano 2020!


Katika mkutano wa Umoja wa Mataifa na mashirika mengine mjini Geneva wa maandalizi mkutano wa kutazama kwa upya mkataba  ya Kimataifa dhidi ya silaha za kinyukilia 2020,uliofanyika hivi karibuni, Askofu Mkuu Ivan Jurkovic  Mwakilishi wa kudumu Vatican katika ofisi za umoja wa Mataifa zilizoko Geneva ametoa hotuba yake. Na katika hotuba hiyo anonesha jinsi gani Vatican inawatia moyo wote walio anzisha hatua ya mchakato huo kwa ajili ya wema endelevu katika roho ya makutano na urafiki kati ya watu.

Na kutokana Kutokana na hiyo  Baba Mtakatifu anapongeza Mkutano wa wakuu wa nchi za Korea Kaskazini na Kusini, uliofanyika mnamo tarehe 27 Aprili 2018, ambapo pia alipta fursa ya kutoa wito kwa wahusika hao  wa sera za kisiasa kuwa na ujasiri wa matumaini ili waweze kuwa mafundi stadi wa amani na kuwatia moyo waendelee  na njia hiyo wakiwa na imani na kuwa wazi katika hatua mchakato wa mazungumzo kuelekea katika Pensula ya Korea iliyo uhuru, na bila silaha za kinyuklia.

Silaha za maangamizi, kwa namna ya pekee ya kinyuklia, zinaunda uwongo wa usalama, anathibisha na kusema kuwa, misingi ya uongo huo wa amani, husababisha hofu kubwa, na wakati huo watu kwa hakika wanatamani amani ya kweli, usalama na msimamo, ambao ni kinyume na hofu. Upendeleo wa kutengeneza nguvu za kinyuklia ni kinyume na mapenzi ya watu katika ukweli wa amani na ushirikishwaji wa maendeleo ya kibinadamu.

Vatican inaamini kwamba, kuanzishwa kwa mchakato wa mapatano katika   Peninsula ya Korea unaweza kuwa ushuhuda na ambao unaweza kuleta maendeleo halisi ya kusitisha silaha zote ikiwemo hata zile za maangamizi. Kwa utambuzi kwamba, mchakato wa mapatano ndiyo umeanza,Vatican ina matumaini ya kuwa kuanzishwa kwake utakwenda sambamaba na msimamo wa dhati katika kupata matokeo ya vipimo na hasa kuruhusu International Atomic Energy Agency (IAEA) yaani Chombo muhimu katika kitovu cha dunia cha ushirikiano katika kambi za nyuklia ili  kuhamasisha ulinzi, usalama na amani ya matumaini ya teknolojia ya nyuklia. Kinafanya kazi kwa ngazi ya juu  Zaidi hasa kuhusiana na meeneo ambayo yanatengeneza nguvu, afya, chakula, kilimo na ulinzi wa maendeleo!

Kwa njia hiyo, Askofu Mkuu Jurkovic anasema, inawezekana chombo hiki kuwa huru kuchukua majukumu muhimu ya  kuhakiki, kwa maana ni muhimu katika ujenzi wa matumaini na kuongeza nguvu ya amani na usalama, wakati huo huo, wanaweza kuonesha ukweli wa amani  inayo  jengwa juu ya haki, maendeleo ya uchumi kijamii halikadahalika uhuru, heshima misingi ya haki za binadamu, ushiriki wa ustawi wa umma na ujenzi wa matumaini kati ya watu.

Askofu Mkuu Jurkovic amesisitia kuwa, wakati wanaendelea na maandalizi ya mkutano wa kuangaliwa kataba kwa upya mwaka 2020 Vatican  ina matumaini kwamba, uchanya wa maendeleo  hayo utachangia kwa ujumla kutingisha au kuamsha dhamiri, ili kupenda matokeo ambayo yanatokana na msimamo wa nguvu ya kimataifa kuelekea katika kuangamiza ya moja kwa moja  silaha za kinyuklia na zile za maangamizi katika  ulimwengu mzima ikiwa ni katika kuthibitisha roho ya (Proliferation of Nuclear Weapons)  (NPT), ambayo ni kuzuia usambazaji wa nguvu za kinyuklia na ili kufikia mafanikio mema ya maangamizi yake.  NPT,ni Chombo ambacho  kipo chini ya IAEA ambacho ni kiini  cha shughuli nzima ya kuthibiti maeneo yote ya kiteknolojia, hata kuzuia  majaribio ya kinyuklia.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News








All the contents on this site are copyrighted ©.