Tarehe 4 Mei 2018 Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Kikosi cha Kipapa cha
Ulinzi na Usalama cha Uswiss mjini Vatican na wageni wao kufuatia na fursa ya kupata
kiapo chao kama walinzi wa kharifa wa mtume Petro. Katika hotuba yake, amewakaribisha
wote kwa namna ya pekee kikundi cha vikosi vya ulinzi na familia na marafiki wao ambao
wamependa kushiriki katika sikukuu yao kwa siku hizi. Aidha amewapa salama hata wawakilishi
wa madaraka kutoka nchini Uswis ambao pia wamefika katika afla hiyo.
Akiwageukia wanajeshi anasema, wao ni wenye uwezo wa kutoa huduma hiyo kwa kipindi
watakachokuwa mjini Roma, ili kuweza kufanya uzoefu wa aina yake katika chuo kikuu
cha Kanisa. Muda huo unaweza kuwa fursa kwao na kuwatia nguvu katika imani ya kukua
kwa maana ya kushiriki kikamilifu katika jumuiya ya kikristo. Shughuli yao inajikita
kabisa kwa ujasiri na uaminifu wa papa ambapo ilianzishwa mnamo tarehe 6 Mei 1527
ambapo walinzi kutoka Uswiss walitoa maisha yao kwa ajili ya kulinda Kanisa na Baba
Mtakatifu.
Akifafanua juu ya shughuli ya kikosi cha kipapa cha ulinzi na usalama kutoka Uswiss
kinachojikita katika shughuli za kila siku mjini Vatican Baba Mtakatifu amesema,
ni kikosi cha Ulinzi wa Kipapa ambacho kina dhamana na kuendelea kushuhudia ule utulivu
na furaha kwa wale wote wanaofika mjini Vatican ili kutembelea Kanisa kuu la Mtakatifu
Petro au kwa ajili ya kukutana na kuzungumza na Kharifa wa Mtakatifu Petro, kwa namana
hiyo anawapa mwaliko wa kuwa imara na thabiti katika imani, na kuwa wakarimu wenye
upendo wa dhati kwa wote wanaokutana nao!
Vilevile akiedelea na kueleza juu ya shughuli kikosi hiki tangu mwanzo kama mashujaa
ametoa mwaliko kwa wote kuendelea kuonesha thamani hiyo hiyo kwa amani na na msimamo
wa imani katoliki; utimilifu na urafiki na Yesu upendo kwa ajili ya Kanisa ; kuwa
na furaha katika shughuli zao zikiwa kubwa au ndogo za unyenyekevu kila siku. Ujasiri
na uvumilivu, ukarimu na mshikamano na wote, Baba Mtakatifu anasema ndizo fadhila
ambazo wao wanaalikwa kuzifanyia mazoezi watakapokuwa wanatoa huduma yao kwa ajili
ya ulinzi na usalama mjini Vatican, hata wakiwa nje ya mavazi yao. Kikosi cha Ulinzi
na usalama kutoka Uswiss, daima kinajulikana hivyo, wawe ndani ya huduma na hata wakiwa
nje ya huduma hiyo, Baba Mtakatifu anathibitisha.
Ni vizuri kuona kijana kama wao anaonesha umakini kwa wengine na uwezekaoa wa kusaidia wale ambao wanahitaji. Hiyo ni kwasababu Baba Mtakatifu anaongeza, siyo rahisi daima kutoa ushuhuda katika tabia ya namna hiyo, lakini kwa msaada wa Bwana inawezakana! Na zaidi Baba Mtakatifu anawaomba wasichoke kukutana na Bwana Yesu katika sala ya Jumuiya na binafsi, kusikiliza kwa makini Neno la Mungu na kushiriki kikamilifu Ekaristi Takatifu.
Siri ya kazi yao Vatican, hata katika mipangpo yao ya maisha inategemea zaidi kukutana na Kristo. Baba Mtakatifu pia anatumia fursa hiyo kurudia kwa upya, kuwashukuu Kikosi cha Ulinzi na Usalama cha Papa kutoka Uswiss. Anawapongeza kwa adabu yao hasa wakati wa kutoa huduma yao na kuonesha taaluma yao katika huduma hiyo na zaidi ule utulivu wanao uonesha kila siku wakati wa huduma mjini Vatican.
Anamshukuru Mungu kwa zawadi nyingi ambazo anawajalia kila mmoja na kuwaombea ili waweza kuimarika na kuzaa zaidi matunda. Na kwa njia ya maombi ya Bikira Maria ambaye anakimbiliwa katika mwezi wake wa Rosari na watakatifu wasimamizi wawalinde. Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu amewapa Baraka ya kitume kwa ajili ya ndugu jamaa na marafiki, hata kwa ajili ya nchi yao!
Sr Angela Rwezaula
Vatican News!
All the contents on this site are copyrighted ©. |