2018-05-02 15:38:00

Kumkataa shetani na kusadiki Mungu mmoja ndiyo ufunguo wa Ubatizo!


“Ndugu wapendwa, habarini za asubuhi; Kwa kufuata tafakari juu ya Ubatizo, leo hii ninataka kusimamia juu ya matendo misingi ya ibada inayotendeka katika kisima cha ubatizo”. Ndiyo maneno ya Baba Mtakatifu Francisko aliyoanza nayo wakati wa kutoa tafakari ya Katekesi yake, kwa mahujaji na waamini waliofika katika kiwanja cha Mtakatifu Petro Mjini Vatican tarehe 2 Mei 2018.

Akifafanua juu ya Sakramenti hii ya Ubatizo Baba Mtakatifu Francisko anasema, kwanza ni kutazama maji ambayo wanaanza kuomba Roho, ili aweza kutoa nguvu ya kuzaliwa na kupyaishwa (taz Yh 3,5 e Tt 3,5). Na maana hyo Maji ni mama wa maisha na ustawi, wakati huo huo, hukosefu wake unaweza kusababisha ukosfu wa kila aina ya kuzaa tunda, kama inavyojitokeza katika jangwa; lakini maji pia yanaweza kuwa sababu ya majanga ya kifo hasa kwa nguvu za mikondo yake, inaweza kupoteza kila kitu;  na mwisho maji yana uwezo wa kuosha na kusafisha.

Katika kupitia ishala hiyo ya kawaida katika ulimwengu inayojulikana, Biblia inaandika matukio mengi na ahadi za Mungu kwa njia ya ishala ya maji. Pamoja na hayo utashi wa kutenda dhambi hautokani na maji, kama alivyo fafanua Mtakatifu Ambrose, kwa wabatizwa: “Mmeona maji japokuwa siyo maji yote yanasafisha, kwa maana maji yanayosafisha ni yale yenye neema ya Kristo. (…) Kwa maana hiyo tendo ni maji kwa njia ya Roho Mtakatifu (De sacramentis 1,15). Baba Mtakatifu Francisko anaendelea kufafanua ya kwamba, Kanisa linaomba nguvu ya Roho Mtakatifu juu ya maji ili wale ambao watapokea Ubatizo waweze kuzikwa na Ktisto katika mauti na kufufuka katika maisha mapya ( taz katika lituruja ya ubatizo wa watoto n.60).

Katika maombi ya Baraka yanasema kuwa, Mungu ameandaa maji kuwa ishala ya Ubatizo na kukumbusha mambo msingi katika Biblia: kwa mfano katika asili ya uumbaji kulikuwa na Roho ya Mungu aliyetulia juu ya uso wa maji na kufanya maisha mapya. “Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.(Taz 1, 1-2); Maji ambayo yanatajwa katika ghalika kuu ishala ya mwisho wa dhambi na mwanzo wa maisha mapya (Mw 7,6-8,22); kupitia bahari ya shahamu walikombolewa watoto wa Ibarahii dhidi ya utumwa wa Misri” (taz Kut 14,15-31. Na Biblia ikielezea juu ya  uhusiano na Yesu Baba Mtakatifu amesema, tunakumbushwa Ubatizo wake katika mto wa Jordan, (taz Mt 3,13-17); damu  na maji yaliyo mwagika  kutoka ubavuni mwake (taz Gv 19,31-37) na  Yesu anawatuma mitume wake, wakabatize watu wote kwa jina la Utatu Mtakatifu (taz Mt 28,19). 

Kumbukumbu za nguvu hizi, ndizo zinaombwa kwa Mungu neema ya Kristo aliyekufana na kufufuka katika kisima cha maji, ( taz ibada ya ubatizo wa watoto wadogo 60). Kwa maana hiyo maji hayo yanabadilika kuwa neema ndani mwetu kwa nguvu ya Roho Mtakatifu. Na maji hayo yenye nguvu ya Roho Mtakatifu ndiyo yanabatiza watu wazima, watoto na wote.  Maji yakisha takatifuzwa katika kisima, lazima yawezeshe roho hiyo kupokelewa katika Ubatizo.
 
Lakini hiyo inajitokeza mara baada ya  kumkataa shetana na kukiri imani,matendo mawili  ambayo yanayounganika kati yao. Katika kipimo ambacho ninatamka ku wa “namkataa shetani na mambo yake yote, yaani yule ambaye anatengenisha, ndipo ninao  uwezo wa kusema “ndiyo” kwa Mungu anayeniita ili kufanana Naye kwa mawazo na matendo. Shetani anagawanya lakini Mungu naunganisha daima jumuiya na watu ili waweze kuwa wamoja. Huwezi kumpokea Kristo wakati unamwekea masharti anasisitiza Baba Mtakatifu. Inahitaji kuondokana na kila aina ya mahusiano mabaya,  ili uweze kukumbatia wengine kwa dhati; Na uchaguzi huo lazima kuufanya kwa dhati ambapo au uchague kuishi na Mungu vizuri  au unaishi vizuri na shateni. Kwa kuthibitisha hilo, tendo la kukataa shetani na tendo la kukiri imani vinakwenda sambamba. Ni  lazima kubomoa madaraja  ambayo siyo ya kweli na kuyaacha nyuma ya mabega ili kuanza njia mpya ambayo ni Kristo.

 Jibu linalotolewa katika swali la “ unamkataa shetani na mambo yake yote na ulaghai wake wote? , Baba Mtakatifu amefafanua , ni tabia au swali linalo mlenga mtu binafsi, ili kujibu “ninamkataa”. Na kwa namna hiyo ndipo inafuatia  tendo la kukiri imani ya Kanisa kwa kusema: “ninasadiki”. Mimi ninakataa shetani,  na nina ninasadiki. Kwa maana ndiyo msingi mkuu wa Ubatizo, Baba Mtakatifu anathibitisha.  Ni uchaguzi wa uwajibikaji ambao lakini unakutaka kuutafsiri katika matendo ya dhati ya imani kwa Mungu. Tendo la imani linakuwajibisha kwa shughuli yenyewe ya ubatizo na kukusaidia kutunza na kuwa na uvumilivu katika hali halisi  na majaribu ya maisha. Baba Mtakatifu Francisko anakumbusha hekima ya zamani ya Israeli:  “mwanangu, ukienda kumtumikia Bwana, uwe tayari kupata majaribu” (Sir 2,1), hiyo ikiwa inamaa anaongeza Baba Mtajkatifu Francisko, ni kujiandaa na mapambano, lakini  uwepo wa Roho Mtakatifu unatoa nguvu ya kupamba vema!

Amehitimisha Baba Mtakatifu Francisko  katekesi yake kuwa: tunapogusa na mikono  katika maji yaliyobarikiwa, wakati wa kuingi Kanisani, na kufanya ishala ya Msalaba, tufikirie kwa furaha na shukrani ya Ubatizo ambayo tumepokea, kwa maana maji hayo ya baraka yanatukumbusha Ubatizo na kupyaisha ubatizo wetu na kusema: “ninasadiki na kuwa na furaha ya kuogelea ndani ya upendo wa Utatu Mtakatifu”!

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News








All the contents on this site are copyrighted ©.