2018-05-01 15:20:00

Papa Francisko ametoa hotuba kwa wakuu na wafanyakazi wa gazeti la Avvenire!


Wapendwa wa Avvenire, ninawasalimia walei wote ambao mnajikita kwa mantiki ya hali ya juu katika shughuli za kutangaza. Ninamsalimia Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Italia, Kardinali Gualtiero Bassetti na kumshukuru kwa maneno ya hotuba yake; salam kwa Katibu Mkuu Askofu Nunzio Galantino na Askofu Semeraro. Hizi ni salam za utangulizi wa Baba Mtakatifu Francisko siku ya Mei Mosi 2018, wakati alipokutana na viongozi na wafanyakazi wa Gazeti  Katoliki la Avvenire la Baraza la Maaskofu nchini Italia mjini Vatican.

Baba Mtakatifu anonesha furaha yake ya kushirikishana nao katika siku iliyotolewa na Mama Kanisa kuadhimisha sikukuu ya  Mtakatifu Yosefu Mfanyakazi. Akiendelea kufafanua anasema: ni rahisi zaidi kupenda sura ya Mtakatifu Yosefu na kumwomba maombezi yake, lakini, ili kuweza kuwa marafiki wake wa kweli, inahitaji kupita  katika hatua zake, ambazo ni mwanga na mtindo wa Mungu. 

Mtakatifu Yosefu ni mtu mkimya: Kwa mtazamo wa kwanza unaweza kufikiria kuwa siyo mtu wa kuongea, lakini ki ukweli, ukitazama kelele za dunia na mazungumzo mengi tuliyo nayo  ndipo unaweza kusema kuwa hupo umuhimu wa kusikiliza  na kukubali katika hali ya kila tangazo. Kwa njia hiyo ukimya wa Yosefu ni makao ya sauti ya Mungu na kuzaa ule utii wa imani ambao unapelekea kuvumilia na kuacha uongozwe na mapenzi yake.

Si kwa bahati mbaya Yosefu ni mtu ambaye anajua kukesha na kuamka wakati wa usiku, bila kukata tamaa pamoja na kuelemewa na uzito wa matatizo. Yeye anatambua kutembea  katika giza ambalo kwa wakati mwingine hakuwa anajua mwisho wake; yeye ni mwenye nguvu katika wito ambao unawekwa mbele ya fumbo,  lakini anaukubali na kuupokea kwa uhuru wake, akijikabidhi bila kubakiza!

Kwa maana hiyo Mtakatifu Yosefu ni mtu mwenye haki na mwenye uwezo wa kujikabidhi katika ndoto ya Mungu, kuanzia mbele ya ahadi. Ni mlinzi makini na mpole, ambaye anatambua kubeba hali halisi ya watu na maisha ambayo amekabidhiwa kuwajibika. Ni mwalimu bila kujidai lolote na kugeuka kuwa baba kwa neema ya uwepo wake; uwezo wake wa kusindikiza na kufanya makuzi ya maisha ambayo yanajionesha katika kazi. 

Baba Mtakatifu Francisko anasema:tunatambua wazi  jinsi gani ukuu wa kipengele hiki cha mwisho juu ya kazi, ndicho kinacho husiana na Sikukuu ya Mtakatifu Yosefu, na ni jinsi gani kilivyo muhimu. Kwa dhati, kazi inahusiana na hadhi ya mtu: Lakini hiyo si tu kwa ajili ya kuwa na fedha, hata kuweza kuonekana au kuwa na madaraka, bali inahusu kazi!. Kwa maana ya kazi ambayo inatoa hadhi kwa kila mtu  katika nafasi yoyote aliyo nayo  «actus personae» (cfr Enc. Caritas in veritate, 41), na mahali ambapo binadamu na familia wanabaki kuwa kiini zaidi ya ukosefu wa kazi yenyewe!

Kwa mtazamo wa haraka na mwema, Baba Mtakatifu anasema; uselemala wa Nazareth na ofisi ya gazeti la Avvenire ni hatua ambazo zinakwenda sambamba na wala haziachani umbali. Hiyo ni kutokana na kwamba, kwa hakika kabati ya  zana zao;  leo hii kuna vyombo vya kiteknolojia ambavyo vimebadilisha kwa kina utaalam, hata namna ya kusikiliza, kufikiria, kuishi na kutangaza, kutafsisri na kuhusiana.

Utamaduni wa kidigitali unataka mpangilio mwingine wa kazi pamoja na uwezekano, lakini badopia  ukuu wa kushirikiana kati yao na kuelewana na vyombo vingine  ni muhimu kwa maana ni sehemu ya  Baraza la Maaskofu Italia. Kwa mfano, amevitaja vyombo hivyo kuwa;  Shirika la Habari la Sir, Televisheni 2000 (Tv200) na Mzunguko wa Simu (InBlu). 

Sambamba na hilo, hata kile ambacho kinajitokeza katika mawasiliano ya Vatican, hatua za kukaribiana na kushirikiana ili kuwezesha jukwaa la digital ambalo lazima liwe na   mikakati  ya ushirikishwaji, ushirikiano na usimamizi mmoja. Lakini Baba Mtakatifu anabainisha yakuwa, mabadiliko haya yanahitaji mikakati ya mafunzo na sasisho za kila mara, katika utambuzi wa mashikilio ya kizamani ambayo yanaweza kuonesha kishawishi haribifu. Aidha amesema ya kuwa, wahudumu wa kweli katika utamaduni ni wale ambao wanafanya kumbukumbu na kutambua kung’amua ishara za nyakati  na kufungua hatua mpya za mwendo! (rejea Gaudium et spes, 11)

Sr Angela Rwezaula 

Vatican News

 








All the contents on this site are copyrighted ©.