2018-04-30 16:25:00

Tunaalikwa kukaa na Bwana kama mzabibu na matawi ili tuzae matunda!


Neno la Mungu hata katika Domenika ya tano ya Pasaka inaendelea kutuelekeza njia ya kuweza kuwa katika jumuiya moja ya Bwana Mfufuka. Domenika iliyopita ilikuwa inaonesha uhusiano kati ya waamini na Yesu chungaji mwema. Leo hii Injili inapendekeza kuona jinsi gani  Yesu anajiwakilisaha kama mzabibu wa kweli na kutualika kukaa ndani yake ili kuweza kuzaa matunda. (Yh 15,1-8). Mzabibu ni mmea ambao umeundwa moja kwa moja na matawi yake; na matawi hayo yanatoa matunda iwapo yameungana tu na mzabibu huo. Uhusiano huo ndiyo siri ya maisha ya kikristo na Mwinjili Yohane, ameendeleza kukazia na  kutumia neno “kukaa” kwa maana katika Neno la Injili ya siku ya leo , neno kukaa limerudiwa mara saba. Yaani kaendi ndani yangu nami ndani mwenu.” Ni utangulizi wa tafakari ya baba Mtakatifu Francisko, Doomenika ya tano ya Pasaka, wakati wa sala ya malkia wa Mbingu kwa waamini na mahujaji wote waliofika katika Kiwanjia cha Mtakatifu Petro mjini Vatican tarehe 29 Aprili 2018. 

Baba Mtakatifu Francisko akifafanua juu ya neno kukaa, anasema, hiyo inahusu kukaa na Bwana ili kuweza kupata ujasiri wa kuondokana ubinafsi, furaha zetu binafsi , nafasi zetu finyu na zinazolindwa, ili kuweza kukutana na bahari kubwa iliyofunguka ya mahitaji ya wengine na kutoa nafasi kubwa ya kupumua katika kutoa ushuhuda wa kikristo katika dunia. Ujasiri huo wa kujiondoa ubinafsi na kukutana na wengine unatokana na imani ya Bwana mfufuka na uhakika ambao Roho anatusindikiza katika historia. Moja ya matunda yaliyo komaa zaidi na ambayo yanatokana na muungano na Kristo ni kuwajibika kwa upendo kwa ajili ya jirani, kuwapenda ndugu bila kubakiza hadi hatima ya mwisho, kama Yesu alivyotupenda sisi. Tabia ya upendo wa mwaamini, siyo tunda litokanalo na mikakati, hata kutokana na msukumo wa nje, shughuli za kijamii au mawazo ya kiitikadi, bali mwendeno huo unazaliwa kutokana na kukutana na Yesu na kukaa na Yeye mwenyewe! Yeye kwa ajili yetu ni maisha ambayo yanatoa kiini, yaani maisha ya kupeleka katika jamii kwa namna tofauti ya kuishi na kutumia muda wetu wa kujikita katika nafasi ya kwanza kwa ajili ya walio wa mwisho.

Unapokuwa na uhusiano wa kina na Bwana, kama jinsi kama walivyo na uhusiano wa iina katu yao mzabibu na mataiwi , upo uwezekano wa kutoa matumanda ya maisha mapaya ya huruma haki na mamani ambayo inatokana Ufufuko wa Bwana.  Kama walivyofanya wayakatifu, watu ambao waliishi kwa utimilifu wa maisha ya kikrsto na kushuhudua upendo, kwasababu walikuwa matawi kweli kweli ya mzabibi wa Bwana. Ili kuwa Mtakatifu lakini siyo lazima uwe askofu, padre, mtawa wa kike au kiume (….).

Baba Mtakatifu amesema, wote wanaalikwa kuwa watakatifu katika kuishi maisha kwa upendo na kujisadaka kila mmoja , kwa kutoa ushuhuda binafsi kwa kila  nafasi ulipo kila siku; na ndiyo utakatifu upo,(rejea Wosia wa Gaudete et Exsultate, 14). Sisi sote tumeita kuwa watakatifu: tunapaswa kuwa watakatifu katika utajiri huu ambao tunaupokea kutoka kwa Bwana Mfufuka. Kila shughuli, iwe ya kazi na kupumzika; iwe maisha ya familia, kijamii na mazoezi ya uwajibikaji kisiasa, utamaduni na uchumi. Kila aina ya kazi kwa maana iwe ndogo au kubwa, lakini ya kuweza kuishi na muungano na Yese katika  tabia ya upendo na huduma, ni fursa ya kuishi kikamilifu Ubatizo na Utakatifu wa Injili!

Baba Mtakatifu Francisko akihitimisha tafakari lake anasema : Kwa msaada wa Maria, Malkia wa Watakatifu na mfano kamili wa muungano na Mwana wa Mungu, atufundishe kukaa ndani ya Yesu kama matawi na mzabibu na tusitengane kamwe katika upendo wake. Tunatambua wazi kwamba: pasipo Yeye hatuwezi kufanya lolote kwa maana maisha yetu ni Kristo aliye hai ambayo yupo katika Kanisa na katika dunia!

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.