2018-04-30 16:42:00

Mei Mosi Papa Francisko atasali Rosari kwa ajili ya Siria na Dunia nzima!


“Ndugu wapendwa, jana huko Krakow nchini Poland ametangazwa Mwenye heri Anna Chrzanowska, mwaamini mlei ambaye alijitoa maisha yake yote kuwawasaidia wagonjwa na kwa njia hiyo alikuwa akitazama uso wa Yesu mteswa". Tumshukuru Mungu kwa ajili ya ushuhudua wa mtume huyo wa kwa wagonjwa na mwa juhudu hiyo tuige nasi mfano wake! Ndiyo matashi mema aliyo anza nayo Baba Mtakatfu Francisko, mara baada ya sala ya Malkia mbingu katika uwanja wa Mtakatifu Petro Domenika ya tano ya Pasaka,tarehe  29 Aprili 2018.

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea na hotuba yake fupi amesema: anawasindikiza kwa sala kuhusu matokeo  chanya ya mkutano kati ya viongozi wa nchi mbili ya Korea ya Kusini na Kaskazini, ulifanyika Ijumaa  27 Aprili 201, na ujasiri wajuhui, uliotolea na viongozi wote wawili wa kutaka kutimiza mchakato wa mazungumzo ya wazi kwa ajili ya Peninsula ya Korea huru, bila kuwa na silaha za kinyuklia. Baba Mtakatifu anaomba Mungu ili matumaini ya wakati endelevu ya amani na undugu wa kirafiki yasiweze kukatisha tamaa; ili ushirikiano uweze kuendelea na kuzaa matunda kwa ajili ya wema wa watu wapendwa wa Korea na kwa ajili ya ulimwengu mzima!

Halikadhalika Baba Mtakatifu Francisko amekumbuka janga linaloendela kwa mara nyingine tana katika Kanisa la Nigeria, mahali ambapo amesema,shambulio la kikundi cha waamini katika Kanisa na kati yao mapadre wawili wamepoteza maisha Kwa njia hiyo anawakabidhi kwa huruma ya Mungu ndugu hao ili kweli aweze kuwasaidia hata jumuiya hiyo iliyojaribiwa namna hiyo wapate amani ya kweli.

Aidha amewasalimia makundi ya wahujaji wengi waliofika na ambao hasingeweza kuwataja wote majina bali baadhi kwa mfano kutoka Ureno, India, Pakistan na  Italia waliokuwa wengi sana. Wazo lake pia limewandea kwa namna ya pekee Jumuiya za vyama katoliki huko Asisi wakisindikizwa na  Askofu wao; kwa ajili vijana na wale ambao wanaudhuria mkutano wa kitaifa wa wakatekumeni , ulio andaliwa na Baraza la Maaskofu Italia. 

Kadhalika, Baba Mtakatifu ametoa taarifa kuwa Mei Mosi  mchana ataanza mwezi wa Bikira Maria kwa kutembelea Madhabahu ya Bikira Maria yaliyoko huko “Divino Amore” kando ya mji wa Roma. Kule ataungana na waumini wengine kusali Rosari kwa namna ya pekee kusali kwa ajili ya nchi ya Siria na Dunia nzima. Amewaalika wote kuungana naye kiroho katika mwezi mzima wa Mei kwa sala ya Rosari kwa ajili ya  kuomba amani. Na wote amewatakia matashi mema ya Domenika na kuwaomba wasisahau kusali kwa ajili yake.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.